Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:
Radio Vatican

Maskani / Kanisa / Kanisa Ulimwenguni

Mkutano wa Maaskofu Marekani kuhusu uhuru wa dini na wahamiaji


Kuteswa kwa dini, wahamiahi na vijana ndiyo mada muhimu katika Mkutano wa Baraza la maaskofu wa Marekani utakao fanyika tarehe 14-15 Juni 2017 huko Indianapolis. Baraza la Maskofu wa Marekani wataunganika katika mkutano wa mwaka ambapo wanasema kuwa kutakuwepo na mada kama vile za maendeleo ya mpango kuhusu afya uliyo kiukwa na Donald Trump,pia itakuwa mkutano wa kwanza katika kufanya maandalizi ya Sinodi ijayo ya maaskofu iliyoitishwa na Baba Mtakatifu Francisko Oktoba 2018 kuhusu vijana.

Hotuba ya Askofu wa Las Cruces wa Mexco mpya na Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Haki na Amani Oscar Cantu’ itawakilisha hali halisi ya kunyanyaswa kwa dini,mauaji na ukiukwaji wa haki za kibinadamu katika nchi za  Mashariki ya kati. Kwa mantiki hiyo maaskofu watatathimini uwezekano wa kuunda lakini baada ya  kupiga kura Kamati ya Kudumu ya Baraza  la uhuru wa dini katika umbu la Baraza la Maaskofu. Zaidi ya hayo kamati hiyo itaandaa maelezo mafupi wakiwa  na wataalamu wa kimataifa kujadili matatizo ya wahamiaji kwa utambuzi wa sera mpya za kisiasa zilizochukuliwa na Serikali mpya ya Marekani.

Watakao ongoza majadiliano kuhusu Sinodi ya Maaskofu itakayofanyika 2018, kuongea masuala ya vijana na mang’amuzi ya miito ni askofu wa Philadelphia na Rais wa Kamati ya  Walei, Ndoa, Familia na Vijana Kard Askofu Charles Chaput,  Askofu wa Newark na Rais wa Kamati ya Wakleli, maisha ya kitawa na miito Kard Joseph Tobin. Mada nyingine zitakazotolewa katoka Mkutano mkuu wa mwaka zinahusu mwelekeo wa maadhimisho ya Sakramenti ya wagonjwa na walemavu na mkusanyiko wa sala za baraka katika lugha ya kihispania.

Jibu na wito wa Baba Mtakatifu Francisko utatolewa  Jumatano jioni ya tarehe 14 Juni 2017, Maaskofu wakiwa katika sala na kutubu katika Siku ya Kimataifa ya kuombea waathirika wadogo wa unyanyaswaji wa kijinsia. Mwaka jana Septemba wakati wa Mkutano wa mwaka wa Kamati ya Baraza la  Kipapa kwa ajili ya utetezi wa watoto, Baba Mtakatifu Francisko aliomba taasisi  kwa upande wa Baraza la maaskofu ifanyike Siku ya sala kwa ajili ya waathirika na waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican