Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:
Radio Vatican

Maskani / Vatican / Hotuba

Zinahitajika nguvu za pamoja kukabiliana na changamoto ya wahamiaji!


Hotuba ya Askofu mkuu Bernadito Auza mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Umoja wa Mataifa, New York kuhusu mada ya Wahamiaji  tarehe 18 Aprili 2017 katika sehemu ya kwanza , ameanza kukumbusha juu ya Mkataba wa Kimataifa wa kutoa nafasi katika agenda ya 2030. Amesema kuwa wakati wa hotuba kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliofanyika tarehe 25 Septemba 2015 Baba Mtakatifu Francisko alieleza kupitishwa kwa agenda ya 2030 ya Maendeleo endelevu kama ishara muhimu ya matumaini.Kwa kuzingatia mwaka 2016 Vatican inakumbusha kuhusiana na Agenda hiyo, pia Vatican inayo matumaini kwamba mambo yatakwenda barabara.Lakni iwapo Agenda ni ya kweli na haki na kwa ufanisi wa utekelezaji kwa wote ikiwa ni pamoja na wahamiaji.

Katika Agenda kipengele (n.10,7) kinatoa wito wa uwezeshaji, utaratibu , usalama wa mara kwa mara na uwajibika katika uhamiaji  na wahamiaji wa watu. Hiyo pia ikiwa ni pamoja kwa utekelezaji wa sera za mipango na kusimamia vizuri suala la uhamiaji. Hivyo matokeo haya yanahitaji hata hivyo uchambuzi wa kina, pamoja  na utambuzi ili kuleta ufanisi wa kuchukua hatua za  mikakati dhidi ya vitendo vinavyo sabisha uhamiaji, vilevile kushughulikia wale wanao endesha uhamiaji wa kulazimishwa kutokana na mapendekezo  agenda ya 2030.Kwa sababu hiyo, Papa Francisko ametoa wito kwa viongozi wote wa serikali kuchukua hatua  mara moja ya  ufanisi na kufanya vitendo  halisi katika hatua za kuhifadhi na kuboresha mazingira ya asili na hivyo kukomesha haraka iwezekanavyo uzushi wa kutengwa kijamii na kiuchumi.

Katika sula la  uhamiaji wa kulazimishwa hii inasababishwa naukosefu wa mshikamano na mara nyingi kwa makusudi katika kupuuza mahitaji ya msingi ya majirani zetu, kama vile upatikanaji wa elimu bora, kazi nzuri, nyumba za kutosha na msingi wa afya. 
Mahitaji haya ambayo hayajafikiwa ni chanzo cha machafuko ya kimataifa na madhara yake ni mabaya kwani husababisha mfumko wa kuhama kwa binadamu, biashara haramu, masoko ya viungo vya binadamu ,unyonyaji biashara ya jinsia moja,  utumwa wa kazi , ikiwa ni pamoja na ukahaba, madawa ya kulevya na biashara ya silaha, ugaidi na ualifu unao andaliwa kimataifa.

Hii ndiyo sababu ya kazi yetu ya kwanza msingi, kwani lazima kujibu mahitaji ya msingi ya ndugu zetu na kuhakikisha amani na usalama nyumbani. Hii pia ni kusudi la msingi wa Malengo yaliyowekwa na sisi wenyewe kufikia  Agenda ya 2030. Eneo moja la ziada na lenye kuwa na wasiwasi mkubwa na kuhitaji umakini wa kuzingatia wakati wa mazungumzo  haya, ni juu ya idadi kubwa ya wahamiaji wasio sindikizwa, yaani watoto na kutengwa.Askofu Mkuu Auza amesema kuhusiana  hilo, ujumbe wake ungependa kurudia maneno ya hivi karibuni ya Baba Mtakatifu Francisko akitoa wito kwa dhati ya kwamba hili ni tatizo la muda mrefu ambalo linatakiwa kutafuta ufumbuzi na ubunifu ili kuingizwa katika mkataba wa makubaliano.

Hata kabla ya kushughulikia ufumbuzi, kama vile kuungana na familia, suala la wahamiaji la mtoto lazima kukabiliana kuanzia chanzo chake. Hii inahitaji hawali ya yote, ahadi ya jamii nzima ya kimataifa ili kuondoa migogoro na vurugu ambayo hulazimisha watu kukimbia au kutanguliza watoto wao mbele kwa matumaini kuwa watapata usalama na hatimaye maisha bora. Wenye kuona mbali mitazamo hiyo, wanaalikwa wote, na wenye uwezo wa kutoa programu za kutosha kwa ajili ya maeneo ya kuondoa udhalimu mbaya zaidi na pia migogoro ili kupata maendeleo halisi ambayo yanaweza kuleta uhakika kwa wote . Mtazamo huu lazima pia kuwajulisha watoa programu, huduma na ulinzi wa wahamiaji, siyo tu wakati wako safarini bali hata baadaya kufika katika nchi wanazo pitia au kwenda.

Sehemu ya Pili ya Hotuba ya Askofu mkuu Bernadito Auza mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Umoja wa Mataifa

Suala linalogusa uhamiaji haliwezi kushughulikiwa na waziri mmoja au idara moja katika serikali. Majibu ya kina ya uhamiaji yanahitaji  mfumo mzima wa serikali, sababu moja ni kwamba  mitazamo ya wizara mbalimbali na viongozi, ni ambayo uonesha asili muhimu ya binadamu na inatambua haja ya kukabiliana kwa kawaida na utata wake wa uhamiaji.  Kwa njia hiyo ni kweli jitihada za uratibu zinahitajika kuwashirikisha, zaidi  serikali, jamii ya kisiasa, vyama vya kiraia, mashirika ya kimataifa, na taasisi za kidini. Kama Baba Mtakatifu  Francisko anavyo sisitiza juu ya utetezi wa wahamiaji.Kwamba ili kuweza kupata haki msingi na kuhakikisha uhuru wao msingi na kuheshimu utu wao, ni wajibu na wala hakuna mtu anayeweza kusamehewa juu ya hilo.

Kuheshimu, kulinda na kukuza haki za binadamu ya wahamiaji, bila kujali hali yao ya uhamiaji, ni amri ya kimaadili, ambayo ni lazima kutafsiriwa katika vyombo kitaifa na kimataifa, kisheria na utekelezaji wa haki mbalimbali ili kufikia maamuzi ya kisiasa na kwamba inapewa kipaumbele cha mchakato wa kujenga na kupata matokeo na ufumbuzi wa  haraka ya makubaliano.Askofu Mkuu Auza amesema, katika mjadala huu, Baba Mtakatifu Francisko ameanzisha dhana mpya  ile ya "wajibu wa ustaarabu," ambao unaonekana kuwa muhimu kabisa kwa lengo la mjadala huu. Mbinu hii haina maana tu katika juhudi za serikali lakini pia ni wajibu wa wahamiaji, wakati wanaendelea kuwa hazina ya maadili yao wenyewe kutokana na  utamaduni wao wa asili, kuheshimu sheria na mila za nchi, kuzipokea na kuvutiwa nazo.

Kuna uhusiano dhahiri kati ya uhamiaji na maendeleo. Uhamasishaji juu  binadamu kuhama na familia zao ni lazima kuanzia katika jamii zao asili, ili kuweza kukomesha  na kufikia mwisho wake. Ni lazima kutia moyo jitihada na kuendeleza ushirikiano wa kimataifa katika mipango ya kimataifa ya maendeleo, bila kuwapa maslahi wanao endelea kukuza mgogoro huo; na pia kuwashirikisha wahamiaji kama wahusika wakuu wa kazi. Amemaliza hotuba yake  Askofu Mkuu Auza akisema, majibu zaidi na ya kina yanatokana na fursa za changamoto za uhamiaji ambazo yanawezekana kukabiliana nazo iwapo jumuiya ya kimataifa itafanya kazi pamoja kuanzia na mahitaji ya msingi ya wahamiaji  wote kutoka pande zote mbili, wanakotoka  na wanapofikia.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.