Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:
Radio Vatican

Maskani / Baba Mtakatifu Francisko / Hotuba

Ongozweni na unyenyekevu, ukimya na mifano bora ya maisha!


Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa Jumuiya ya Shirika la Wamaristi kutokana na kuwadhimisha tukio la Miaka 200 tangu kuanzishwa kwa Shirika hilo, maadhimisho yatakayofanyika nchini Colombia.Baba Mtakatifu amesema kuwa wamependelea kuandaa tukio hilo kwa kauli mbiu ya mwanzo mpya , ambao unajieleza kikamilifu katika mpango wao kutazama  kwa upya  na kutoa shukrani kwa wakati uliopita, uliopo na kufanya mang’amuzi ya wakati ujao kwa matumaini.Shukrani za kwanza ni zile zitokazo rohoni, Baba Mtakatifu Francisko anaandika; na tabia hiyo ya utambuzi ni ya lazima kwasababu ya  kuweza kutathimini mambo makuu aliyo fanya Mungu kwa njia yenu. Pamoja na kusema asante ni jambo jema la kawaida kwetu sisi. Kwasababu  husaidia kutambua hata mambo madogo mbele ya macho ya Bwana; Asante pia ni deni la utamaduni tuliopewa zawadi  bila sisi kufanya lolote .

Mwanzilishi wenu  anatoka katika familia tajiri na yenye ushuhuda  kiasi cha kutoa maisha yake kwa ajili ya Mungu na kwa jirani, katika roho ya kindugu ambayo ndiyo tabia halisi ya ya shirika lenu.Katika mihongo hii miwili ya maisha ya Shirika, imegeukwa kuwa historia kubwa ya watoto na vijana walio kubali wito katika mabara matano ya dunia  wakaunda na kutengeneza uzalendo wema na zaidi kuwa wakristo wema. Matendo hayo ni kelelezo cha wema na huruma ya Mungu , pamoja na kwamba kuna udhaifu, mapungufu na vinyongo vyetu   lakini  Mungu hasahau kamwa watoto wake.Jambo jema la roho, ndiyo lilimfanya mwanzulishi wenu awe wa namna ya pekee :kwa maana ya kwamba ;kuitwa kwa ajili ya kwenda kulima, inahitaji hawali ya yote wakulima wenyewe. Mtawa  anayefundisha ni kutazama ndani ya shamba, rasilimali za binadamu na za  kiroho, ni lazima aondoke kwenda hadi katika shina na kutibu  ardhi ambayo amekabidiwa.  Watawa wanawajibika  kuwa na utambuzi wa  muundo wa ardhi wanayo fanyia kazi kuwa ni takatifu, wakitazama ndani yake upendo na muhuri wa Mungu. Ni kwa wajibu huo wa nguvu na uaminifu wa utume walio pokea unaoweza kuchangia kazi ya Mungu ambayo inawaalika kuwa vifaa rahisi katika mikono yao.

Baba Mtakatifu Francisko aidha  anawatia moyo wawe wazi katika matumaini ya wakati ujao na pia kuwa  wapya katika safari ya kiroho. Amesema hiyo siyo njia tofauti bali ni kuifanya iwe mpya kiroho. Jamii ya sasa inahitaji watu wanye nguvu katika misingi ya ujenzi wa dunia iliyo bora kwa ajili ya wote, na kushuhudia kile wanacho amini. Katika dira ya Mwongozo wa Shirika la ndugu Marists, Baba Mtakatifu Francisko amesema , tayari kuna mpango wa maisha usemao Yote kwa ajili ya Yesu kwa njia ya Maria, Yote ni kwa Maria kwa ajili ya Yesu.Na hivyo  kwa kuongozwa na matumaini, na mama Maria  katika unyenyekevu, kutoa  huduma , kujikabidhi haraka na kuwa kimya ni tabia ni njema ambazo kila mtawa na mwalimu lazima kuwa nazo ili kuzionesha kama mfano.Kutokana mifano hiyo, vijana wanatambua kwa namna yao, au jisni walivyo na kutenda ya kwamba kuna jambo la pekee na kutambua jinsi ilivyo na haja ya kujifunza thamani hizo na hasa zaidi kuziweka ndani ya mioyo yao na kuiga.

Mama Maria ndiye anasindikiza lengo hili na kwa karibu atazidisha miito ili kuchangia kuunda ubinadamu mpya kutoka kwa walio athirika, walio baguliwa na kukosa upendo. Huo ndio wakati endelevu tunao uota na wala siyo udanganyifu .Ujenzi huo uanze lei hii kwa kusema ndiyo mapenzi yako Mungu yatimie ; kwa hakika kama Baba wa kweli anasikiliza matumaini haya kamwe hatapuuza.Amemalizia Baba Mtakatifu Francisko katika Ujumbe wake akishukuru Bwana na Maria ,na pia mwanzilishi wa Shirika la Marists Mtakatifu Marcellino, na kwamba alipenda kuelezea kuwa uwepo wa miito na utume wa Kanisa ,ni kuomba zawadi ya Roho Mtakatifu maana kwa njia yake, inawezekana kufanya hudma ya watoto na vijana na kama ilvyo kwa wote wenye kuwa na mahitaji ili wawe karibu na ukarimu wa Mungu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican