Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:
Radio Vatican

Maskani / Vatican / Hotuba

Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kufikisha miaka 90 kuzaliwa


Tarehe 17 Aprili 2017 ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI ,sherehe za kukumbuka sikukuu yake, zilifanyika mjini Vatican, akiwa na ndugu jamaa na marafiki kutoka  nchini kwake Ujermani. Wakati wa tukio la sikuu ya , Maria Galgano mwandishi wa Habari wa Radio Vatican, alipata fursa ya kuongea naye, na kumpatia matashi mema kutoka kwa wasikilizaji wote wa Radio Vatican kwa ajili ya kufikisha miaka 90. Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI alijibu akisema kwamba, anawashukru sana kwa ukarimu wao.

Aidha katika maelezo Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI katika lugha ya Kijermani anashukuru Mungu kumpatia maisha mazuri, japokuwa maisha ni milima na mabonde,lakini pamoja na hayo anajisikia furaha kubwa na kujisikia nyumbani kama vile nyumbani kwake Baviera, mahali ambapo kuna mandhali nzuri na kutaja pia hanga la blu Roma likiwa na mawingu meupe yanayomkubusha daima bendera ya eneo lake Baviera , na mwisho anatoa baraka kwa wote.

Halikadhalika katika tukio la mika 90 ya kuzaliwa,toleo jipya la kitabu kinachoeleza maisha yake kwa picha limetolewa katika sukukuu hizi za Pasaka.
Katika toleo jipya la kitabu , linaelezea ushuhuda wa kibinadamu,Kitabu chenye kichwa "Bededetto XVI picha na maisha”.
Mtunzi wa kitabu hicho amesema wazo kuu limetokana kitabu cha Hekima ya Yoshua bin Sira, kwamba ukiwa mwenye hekima unaweza kuruka kwa njia yake haraka ngazi hadi ufiki juu.Mwandishi wa kitabu hicho Maria Giuseppina Nuonanno amesema, ni kutaka watu watambue kwa njia rahisi  
kwa kila mmoja anayetaka kujua ushuhuda wa imani ya muhongo huu. Kwa njia hiyo kitabu hicho kinaelezea kwa njia ya picha zenye kuelezea kila tendo la Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI.

Katika utangulizi wa kitabu hicho Padre Federico Lombardi ambaye ni Mwanzilishi wa Chama cha Ratzinger , ameandika kuwa macho ya Baba Mtakatifu Benedikto XVI ni yale yanayotafuta ukweli na utambuzi kwasababu mtazamo wake unakwenda zaidi ya upeo ambao unatazama tayari mwanga,na mwanga mkubwa wa ufufuko. Hiyo ni kwasababu Ratzinger alizaliwa Jumamosi Kuu na akbatizwa katika maji mapya ya usiku wa Pasaka , anaishi katika matatizo, furaha na uchungu kila siku lakini tayari yuko katika kile tunachokiona yaani ule mwanga wa ufufuko.

Halikadhalika katika sura ya nne inayoelezea juu ya mahusiano ya Baba Mtakatifu Francisko kwa miaka minne pamoja na Baba Mtakatifu Mstaafu, amesema kuwa picha ni nzuri zinazo onesha hali halisi ya mahusiano hasa zaidi ya undugu kati yao, kwasababu wao ni mfano wa wakfu wa kiaskofu kindugu na pia kwa kila binadamu. Baba Mtakatifu Francisko, anamwona Baba Mtakatifu Mstaafu kama babu , mwenye hekima katika nyumba. Na Baba Mtakatifu Benedikto mstaafu anatambua hawali ya yote  kwamba Baba Mtakatifu Francisko juu ya furaha yake , matendo yake anayo yaonesha na kwa wengi .

Katika kitabu ipo pia sehemu aliyo andika George Ratzinger ambaye ni kaka yake  Baba Mtakatifu Mstaafu benedikto XVI , akisema kwamba watu wengi wanakutana na maneno ya Baba Mtakatifu Mstaafu, ambayo ni maneno ya kutia moyo na nguvu mpya ya mwelekeo.Kwa maana ni kweli kwamba Benedikto XVI anao uwezo mkubwa kiakili ni tunda la utamaduni wa ulaya ,anonesha  namna ya kuendelea  kutafuta bila kuchoka uso wa Mungu kwa njia ya mafunzo ya kiteolojia, na unaozidi kutajirisha wasikilizaji watakao endelea kupanda mbegu ili iweze kutoa matunda kwa muda mrefu wa Kanisa.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican