2017-04-18 15:49:00

Askofu Mkuu Pizzaballa:kuwa jasiri kutetea imani ya Kristo mfufuka!


Maisha tunayo adhimisha pamoja na wasiwasi na kiburi kionekanacho na kudhalilishwa huko Syria, Iraq, Yemen, Misri na nchi Takatifu, ni kumbukumbu ya hali ya zote za misukosuko inayotuzunguka. Haya ni maneno kutoka katika mahubiri ya Sikukuu ya Pasaka Jumapili tarehe 16 Aprili 2017 katika Kanisa Kuu la Kaburi Takatifu Yerusalem kwenye ibada ya misa Takatifu iliyo adhimishwa na Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa Msimamizi wa Kitume katika maeneo Matakatifu. Askofu Mkuu amehubiri juu ya ufufuko wa Kristo kwa kujikitandani ya  matukio ya mashambulizi ya kigaidi na hivyo amesema kuwa hakuna sehemu yoyote ambapo huwezi kutokukutana na Mungu katika historia yetu ya maisha. Lakini kukutana na Mungu hakutolei kufanya uzoefu wa majaribu, uchungu au giza. Kwa kutambua hilo amesema inatosha kutazama kando kando yetu , kuona wasiwasi unaotuzunguka kwenye sehemu nyingi ambapo zinaonesha kwamba kuna miiba mingi iliyochomoza ya vifo vya kutaka ushindi.

Amesema hayo kutokana na kukumbuka mashambulizi yaliyofanyika huko Misri , Tanta na Alexandria, na kuongeza kuwa, hii ni hali ya vifo vya wengi katika nchi yetu, ambapo unaweza kufikiri kuwa wengi wanayo kiu ya kifo; lakini kwa bahati nzuri ndugu zetu wako wazi, wametulia, wanayo matumaini , wanashirikiana na wengine , bila kuwa na chuki na wala kutoa kashfa. Hawana hali ya kutaka vurugu wala kulipiza kisasi, bali utulivu, lakini ni wazi kwamba utashi wa kutendewa haki upo. Askofu Mkuu Pizzaballa amesema pamoja na kifo cha mashahidi hao hakikufuta nguvu ya maisha ya jumuiya kuendelea kwasababu siku ya Jumapili ya Matawi kwao ilikuwa tayari ni sikukuu ya Pasaka.Aidha maeongeza kusema “Pamoja na hayo pia hata hapa katika nchi takatifu, hapakosekani vivuli vya mauti, majeraha  kijiografia ya nchi na  katika maisha ya watu wengi ni mengi, na hivyo kusababisha  haki na amani kuonekana ni sauti za maneno yasiyo aminika tena na pia familia kugawanyika.

Akiongea  juu ya matumaini, amesema utafikiri ni jambo lisilo kuwa na maana,na utafikiri ni neno nje ya wakati, na zaidi ya yote hofu na kutokuaminiana vinazidi kupamba moto kati ya imani za kidini tofauti, kati ya jumuiya tofauti, hata ndani ya jumuiya zetu binafsi na katika famiia zetu, bado mgawanyiko wa kila aina kujitokeza. Vitendo hivyo vinatokana na msingi wa  hofu, ni hofu ya kupoteza jambo. Hofu ya kufa na hofu ya  kutoa maisha,Askofu anaonya akisema kufanya hivyo tunajikabidhi katika kifo na nguvu yake. Lakini kama tunaamini kweli katika ufufuko, kama kweli tunamkabidhi hali zote hizi, kama tunafanya ziwe sala, ziwe kilio , kwa namna moja hali hizi zinaweza kugeuka kuwa mwelekeo wa maisha .

Kwa njia hiyo Askofu Mkuu anatoa wito ya kwamba, “tusijifungie katika hofu zetu , tusiruhusu kifo mbele ya watesi wanao ogopesha. Kufanya hivyo ni kukana maisha na imani ya ufufuko!“,na kwamba  “tusiache kamwe kwenda katika kaburi Takatifu ambalo ni wazi”, Kwasababu  Ufufuko ni tangazo la furaha inayo vunja mipaka ya dunia, ili isibaki imefungwa mahali hapa, bali kutoka hapa iwafikie wote”. 
Amesema Askofu Mkuu Pizzaballa Msiamamizi wa Kitume katika Maeneo Matakatifu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.