Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:
Radio Vatican

Maskani / Kanisa Barani Afrika / Amani

Ujumbe wa Pasaka 2017 kutoka Baraza la Maaskofu Afrika ya Kusini


Tumekuwa na misukosuko kwa wiki tatu nchini Afrika ya Kusini na kuna wasiwasi mwingi kuhusu hali ya baadaye  na siyo tu kuhusu wasiwasi wa kiuchumi. Mara nyingi kinacho tokea Afrika Kusini huathiri vibaya hata nchi ya Botswana na Swaziland. Hali ya kutokuwa na uhakika  pia ukosefu wa kuaminiana,huo ni uzoefu karibu unao ikumbuka dunia nzima, kwa namna hiyo hata kama faraja ni ndogo,sisi hatuko peke yetu kwa jambo  hili.
Huu ni ujumbe wa Pasaka  kwa mwaka 2017 wa Baraza la Maaskofu wa Afrika ya kusini unao wapa matumaini waamini wake wote  kwa kipindi hiki chenye msukosuko ya nchi,Maaskofu wamesema, ni vigumu kuishi bila kuwa na uhakika kwa maana hali hiyo uongeza wasiwasi ambao unaweza kugeuka na kuathiri vibaya uhusiano kwa watu wengine.

Kwa njia hiyo ujumbe wa Pasaka unaeleza kwamba, waamini watambue kuwa  hawapo peke yao kwa sababu Kristo yuko pamoja nao. Yeye kamwe hawaachi watu wake, anatembea nao wakati wote kuhimarisha na kufariji.Kwa njia hiyo Maaskofu wamesema, kamwe watu wasikate tamaa .Pasaka ni sherehe inayo kumbusha kwamba "sisi ni Pasaka ya watu, yaani watu wenye kuwa na matumaini na  walio jazwa na maisha ya Roho Mtakatifu wa Mungu.Ni katika furaha na katika  matatizo yetu, na katika matatizo yetu ndimo Bwana amefufuka ; Kristo ni mshindi , Kristo ni Mfalme pia Kristo ni mtawala”! (Christus vincit! Christus regnat! Christus imperat!).Ushindi wake tumepewa sisi  ili tuweza kuutoa kwa watu wangine, ule mwanga wa matumaini na furaha ambayo uangaza katika giza na vivuli!.

Ujumbe ulio sahini wa na Rais wa Baraza la Maskofu wa Afrika  ya Kusini ,Askofu Mkuu Stephen Brislin, unasema ,kwa niaba ya Baraza la Maaskofu wa Afrika ya Kusini ,wanawatakia  Baraka na Heri ya Pasaka Takatifu  watu wote wa Botswana,Afrika ya Kusini na Swaziland. Mungu abariki  familia zao na kuwapa neema  ili uwepo  umoja na maelewano katika familia zao. Wawe na furaha na utulivu kwa wakati huu ambao ni uthibitisho wa matumaini.Ujumbe unahitimisha na maneno ya kufariji kupitia maneno ya Nabii  Isaya yasemayo “Basi,usiogope, mimi nipo pamoja nawe.Usifadhaike, mimi ni Mungu wako.Nitakuimarisha na kukusaidia;nitakulinda kwa mkono wangu wa ushindi”. (Isaya 41:10)

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican