Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:
Radio Vatican

Maskani / Kanisa / Kanisa Ulimwenguni

Pakistan: Wakristo na Waislam pamoja kuhamasisha amani!


Wakristo na Waislam nchini Pakistan wanataka kujenga amani ya jamii na kidini katika taifa na kwa pamoja wameanzisha Kampeni yenye kuwa na ishara ya mzeituni kuonesha dhamira ya pamoja kama ilivyo ripotiwa na Shirika la habari la Fides kutoka kwenye Tume kwa ajili ya Mazungmzo ya kiekumeni na Baraza la Maaskofu wa Pakistan, walio fanya mkutano hivi karibuni ambao umeongozwa na Askofu Mkuu Sebastian Francis Shaw.
Ili kuweza kutekeleza Kampeni hiyo ya kukuza na kuhamasisha amani na utulivu, wametuma katika majimbo yote ya Pakstani ishara ya miti wa mizeituni ili iweze  kupandwa katika mashule , makanisa , miskitini, madrasa, seminari , taasisi za kikristo na Kiislam.

Padre Francis Nadeen Katibu mtendaji wa Tume amesema kuwa, miti ya mizetuni daima ni miti ya kijani matawi yake ni ishara ya wingi , utukufu na amani. Ni ishara ya amani, hekima , utukufu uzazi , nguvu na usafi kwani katika historia ya Maandiko Matakatifu Njiwa alimletea tawi la mzeituni Nuhu kumuonyesha kwamba mafuriko yalikuwa yamekwisha. Mzeituni na mafuta ya mzeituni yametajwa mara saba katika Quran, vilevile mizeituni inasifiwa kama matunda yenye thamani .Padre Nadeen amesema, viongozi wa Kiislam walichangua mzeituni ili upandwe katika Seminari mbalimbali mahali ambapo wanafunzi wa kiislam  wanaweze kujifunza kuwa kila binadamu anataka amani.

Kwa maana hiyo tunataka, na pia tunaweza kuwafanya wawe na hamu ya kuona umuhimu wa kila binadamu kuishi kwa amani.Padre Nadden ameongeza, nia ni kutaka kukuza amani na utulivu hasa miongoni mwa watoto. Zaidi ya hayo, kama miti ya mizeituni itakavyokua  kila siku katika bustani ya Seminari, hivyo hivyo tunatarajia kwamba mitazamo na mahusiano ya upendo na amani vinaweza kukua.Padre amesema pia, ina maana kubwa kuona Kampeni hii imeanzishwa katika kipindi cha Kwaresima na itaendelea katika kipindi chote cha  Pasaka, aidha anabainisha kuwa Tume kwa sasa inazo shule angalau tano za Kiislam katika kila jimbo ambao wameunga mkono juu ya mapango huo.

Miongoni mwa matukio mengine yenye kuwa na sifa kati ya mahusiano ya kidini ,ni mwaliko wa Majlias Wahadat Muslimin ambalo ni Baraza la dini ya Kiislam yenye  tabia ya kijamii na kisiasa, walioshiriki katika tume ya Taifa ya mazungumzo ya kidini na kiekumeni , ambapo walitangaza mipango ya kuwawezesha kuwa na malengo ya mkutano wa kukuza mipango ya mazungumzo ya kudumu kati ya Wakristo na Waislam

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya radio Vatican