Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:
Radio Vatican

Maskani / Kanisa / Kanisa Ulimwenguni

Kard.J.Savino wa Venezuela ametoa wito wasipoteze matumaini!


"Tunalazimika kuzuia na kulinda nchi polepole katika kutafuta maelewano na wengine,ujumbe huo pia tuliwaleza mara baada ya mkutano ulio pita  wa Baraza la Maaskofu, kwamba tunapaswa kulinda haki zetu na za wengine lakini bila kutumia nguvu na vurugu kwa kufuata katiba na sheria". Ni maneno ya Kardinali Jorge Urosa Savino,Askofu Mkuu wa Caracas,nchini Venezuela  aliyotamkwa tarehe 09 Aprili 2017 wakati wa Mahubiri ya Jumapili ya siku kuu ya Matawi kwenye Kanisa Kuu la Mji Mkuu wa Venezuela.Kanisa lilikuwa limefurika umati wa watu ambao haujawahi kutokea hivyo. Askofu Mkuu pia amewaalika waamini wasipoteze matumaini mbele ya hali mbaya inayo endelea katika nchi yao.

Kardinali pia ametoa wito kwa waamini wote wasikose kuudhuria maadhimisho yote ya wiki Kuu Takatifu katika Makanisa yote ya Venezuela ili  kusali kwa ajili ya Amani ya nchi yao inayo endelea kuwa mbaya.Kwa bahati mbaya mvutano katika nchi ya  Venezuela hautulii, na kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na maandamano kadhaa katika maeneo mbalimbali ya nchi, baadhi yao kuleta hata vurugu. Kwa sasa wapinzani wamewaalika makundi ya maandamano 23 ya mji kutoa msaada katika mchakato wa kundoa majaji saba wa Mahakama Kuu wanao tuhumiwa kuandaa mapinduzi ya nchi.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican