Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:
Radio Vatican

Maskani / Kanisa Barani Afrika / Maisha Ya Kanisa Afrika

Maandalizi ya Mashahidi wa Uganda yanazidi kupamba moto !


"Mbaki kidete  katika imani mliyopewa” ni kauli mbiu ya maadhimisho haya katika  madhabahu ya Namugongo , itakayo adhimishwa tarerhe 3 Juni 2017 kwa ajili ya mashahidi wa Uganda.Hayo ni maadhimisho ya kumbukumbu ya mashahidi , 45 wote wakiwa na Wakatoliki na Waanglikani walio chomwa moto kwa agizo la  mfalme Kabaka Mwanga II na baadaya Mfalme wa Buganda kati ya mwaka 1885 na 1887 wakitetea Imani yao kwa Mungu. Mashahidi 20 walitangazwa wenye heri  tarehe 6 Juni 1920 na Baba Mtakatifu Benedikto wa XV na tarehe 18 Oktoba 1964,Baba Mtakatifu Paul VI akawatangaza kuwa watakatifu, wawili kati yao ni Mtakatifu Andrea Kaggwa na Mtakatifu Anatoli Kiriggwajjo wakiwa wote wawili kutoka katika Jimbo la Hoima.

Madhabahu hayo ya mashahidi yako km chache kutoka Kampala mjini ambayo ni moja na ya kituo kikubwa cha mahujaji  wengi kutoka kila kona  ya ndani  na nje ya nchi kudhulia sikukuu hiyo ya mwaka huu tayari ipoti ya tarehe 21 Machi takwimu ya walio kwisha jiandikisha kutoka nje ya nchi ni 200 na kati yao mahujaji kutoka nchi ya Zambia na Malawi. Takwimu za Amecea na vyama vya baraza la maaskofu wa Afrika ya mashariki , takwimu ya wahujaji ya 2016 ;waamini 4.961 kutoka Tanzania, mahujaji 4,000 kutoka Kenya , 800 kutoka Congo , 300 Rwanda , 712 kutoka Burundi na 105 kutoka Sudan ya Kusini , lakini pia hata mahujaji wengine kutoka katika mabara mengine.

Ikumbukwe madhabahu hayo yalitembelewa hata  Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi 28 Novemba 2015 kwenye tukio la kilele cha Jubilei ya miaka 50 tangu Mashahidi wa Uganda kutangazwa watakatifu  tarehe 18 Oktoba 1964 wakati huo huo ziara yake  nchini Kenya na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Baba Mtakatifu Francisko alisema kumbu kumbu ya mashuhuda wa imani ni changamoto ya kuendelea kumshuhudia Kristo katika medani mbali mbali za maisha kama vile majumbani, kwa majirani, katika maeneo ya kazi na katika jamii kwa ujumla wake. Eneo hilo pia limebahatika kutembelewa na Mwenyeheri Paulo VI na Mtakatifu Yohane Paulo II.

Sr Angella Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican