Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:
Radio Vatican

Maskani / Baba Mtakatifu Francisko / Katekesi siku ya Jumatano

Mkristo huongozwa na saburi na faraja ili awe mfereji wa tumaini


Sisi tulio imara katika imani tunapaswa kuwasaidia wale walio dhaifu wayakabili matatizo yao.Kila mmoja anapaswa kumpendeza jirani yake ili huyo apate kujijenga katika imani. Maana yote yaliyoandikwa yameandikwa kwa ajili ya kutufundisha sisi ili kutokana na saburi na faraja tupewayo na hayo maandiko Matakatifu ili tupate kuwa na matumaini. Mungu aliye msingi wa saburi na faraja yote awajalieni nyinyi kuwa na msimamo mmoja kufuatana na mfano wake Kristo Yesu.(Rm 15,1-2.4-5) Wiki kadhaa zilizopita , Mtakatifu Paulo ametusaidia kuelewa vizuri ni jambo gani linahitajika katika matumaini. Leo hii anaonesha mambo mawili msingi ambayo yanagusa maisha yetu na uzoefu  wetu katika imani,yaani saburi na faraja (Rm 15,4-5). Katika barua ya Warumi yamesomeka , maneno hayo mara mbili, yakielezea kwanza neno na baadye Mungu mwenyewe.Je ina maana gani ya kina na ya kweli ?.Je, inaangaza namna gani katika hali halisi ya matumaini?

Ni maneno ya utangulizi wa mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake Jumatano 22 Machi 2017 katika viwanja vya Mtakatifu Petro mjini Vatican.Baba Mtakatifu anachambua kuwa;saburi tunaweza kuielezea kama vile subira , ni uwezo wa kutahimili hadi kubaki mwaminifu , hata kama mzigo ni mkubwa kiasi cha kushindwa kuubeba na pale unaposhawishika  kuachilia mbali kwa njia zozote .Na kwa upande wa faraja tunaweza kuielezea kama neema na kutambua kuipokea kwa kuionesha hata pale penye kukatisha tamaa, au kuna mateso na hivyo faraja ni uwepo wa matendo ya huruma ya Mungu.Hivyo Mtakatifu Paulo anatukumbusha ya kwamba saburi na faraja vinaoneshwa na kwa namna ya pekee katika neno yaani yaliyoandikwa yameandikwa. Kwa hakika Neno la Mungu hawali ya yote linatufanya kumtazama Yesu, kumtambua vema ili kufananishwa na yeye zaidi na daima.

Pili  Neno la Mungu  linaonesha kwamba Bwana kweli ni Mungu aliye msingi wa saburi na faraja , ambaye anabaki daima mwaminifu katika upendo wake kwa ajili yetu , yeye anatutunza, anafunika majeraha kwa ukarimu ,wema na  huruma yake. Kwa mantiki hiyo unaweza kutambua zaidi uthibitisho wa mtume anaposema sisi tulio imara katika imani tunapaswa kuwasaidia wale dhaifu na tusijipendelee sisi wenyewe. Msemo huo wa “sisi tulio imara”, unaweze kuonekana  kama kujidai kidogo, lakini kwa mantiki ya Injili tunatambua kwamba siyo hivyo, ni kinyume kabisa , kwasababu imara wetu hautokani na sisi wenyewe, bali unatoka kwa Bwana. Anayefanya uzoefu binafsi wa maisha yake ya upendo mwaminifu katika Mungu na faraja anao uwezo huo, zaidi analazimika kukaa karibu na ndugu wadhaifu pia  kubeba mizigo yao. Anaweza kufanya hivyo bila kujipendelea binafsi,bali kijisikia rahisi kama vile mfereji unao toa zawadi za Bwana,kugeuka kwa dhati kuwa mpanzi wa matumaini.

Matunda ya mtindo wa aina hii ya maisha ,Baba Mtakatifu Francisko anasema  siyo kusema ni jumuiya baadhi kama vile wa kuita  daraja A , maana yake imara na wengine wenye daraja B, maana yake ni wadhaifu. Kinyume chake ni kwamba  ni tunda   kama vile Paulo  asemavyo, “kuwa na msimamo mmoja kufuatana na mfano wa Yesu Kristo” .Neno la Mungu lina rutubisha matumaini, ambayo ugeuka kwa dhati katika kushirikishana na kutoa huduma wenyewe kwa wenyewe. Hiyo ni kwasababu aliye imara ndiyo wa kwanza  kufanya uzoefu wa udhaifu na hata yeye kuwa na mahitaji ya kuwasaidia wengine.Pia hata katika udhaifu unaweza  kujitoa hata kitu rahisi kama vile tabasamu, au mkono kwa ndugu mwenye matatizo. Katika mtindo huo ndipo jumuiya “inakuwa na nia moja na sauti moja, kumtukuza  Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo” (Rm 15,6). Hayo yote yanawezekana iwapo Yesu na Neno lake ndivyo  kiini  cha maisha. Ni yeye aliye peke yake ndugu  imara , anayemtuza kila mmoja wetu, kwasababu sote pamoja tunayo mahitaji ili aweze kutubebwa katika mabega  ya Mchungaji mwema na kwamba tujisikie kuzungukwa na mtazamo wake wa upendelevu na uangalifu.

Amemalizia Baba Mtakatifu Francisko; haitakuwa rahisi kumshukuru Mungu vya kutosha  kwa ajili ya zawadi ya Neno lake. Yeye anaonekana katika maneno yake matakatifu.Yeye anajionesha katika Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na kutuonesha kama Mungu wa saburi na faraja. Ni hapo tunapoweza kuwa  na utambuzi ya kwamba matumaini yetu hayajengwi juu ya  misingi yetu,uwezo wetu,na nguvu zetu , bali ni kutoka katika misingi wa Mungu na katika uaminifu wa upendo.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.