Baba Mtakatifu Francisko amepokea zawadi ya sweta nyekundu na mifuko midogo zaidi
ya 1,000 zilizotengezwa kwa ajili ya usafi binafsi kwa ajili ya wahitaji kutoka kwa
wajasiriamali wa Baa za ufukweni.
Ni mpango ulio anzishwa kwa ajili ya kiangazi mwaka huu kwa mshikamano kwa ajili ya
watoto na watu wenye kuwa na hali ngumu.
Zaidi ya wajasiriamali 1,500 wenye baa fukweni kutoka nchini kote Italia wakifuatana
na familia na wafanyakazi wao walikuwepo katika viwanja vya Mtakatifu Petro kusikiliza
katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko.
Makutano hayo yaliandaliwa na (S.I.B.) chama cha utetezi wa baa za baharini nchini
Italia , pamoja na chama cha biashara (FIPE ) na kwa ushirikiano wa umoja wa wasafirishaji
wa wagonjwa nchini Italia huko Lourdes na madhabahu ya kimataifa.(UNITALISI.
Uwanja wa Mtakatifu Petro ulifurika kwa rangi nyekundu za masweta walikuwa wamevaa
waamini kutokana na uwepo wao kwa mara ya kwanza Vatican.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |