Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:
Radio Vatican

Maskani / Baba Mtakatifu Francisko / Mahubiri

Papa Francisko anawataka vijana kuthubutu kuota ndoto!


Mtakatifu Yosefu awawezeshe vijana kuwa na uwezo wa kuota ndoto,wa kujiweka katika hatari katika kukabiliana na mazoezi magumu wanayo yaona katika ndoto zao.Haya ni matashi mema ya Baba Mtakatifu Francisko aliyoyatoa kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha kilichoko mjini Vatican wakati wa misa ya asubuhi Jumatatu 20 Machi 2017 Baba Mtakatifu katika mahubiri yake, anaelezea sura ya Mtakatifu Yosefu msimamizi katika udhaifu na katika ndoto ya Mungu. Kanisa katoliki likiwa linafanya kumbukumbu yake badala ya tarehe 19 kutokana na kwamba  ilikuwa tarehe 19 Machi 2017 iliangukia  Jumapili ya tatu ya kwaresima.

Mtakatifu Yosefu alitii amri ya Malaika aliye mtokea katika ndoto na kumchukua mchumba wake Maria akiwa na mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kama Injili ya Mathayo isemavyo.Ni mwanaume mkimya na anatii.Yosefu ni mwanaume anayebeba mabegani ahadi ya uzao, ahadi ya urithi,ahada ya ubaba  wa mtoto  ambayo ilikuwa imeshatabiriwa na kupangwa .Baba Mtakatifu Francikos anasema , mwanaume huyo ,mwotaji ana uwezo wa kukubali zoezi hilo. Zoezi ambalo tayari linaweza kutufundisha jambo fulani kwetu sisi katika kipindi cha nguvu kwa maana ya uyatima. Mwanaume huyo anachukua ahadi ya Mungu na kuipeleka mbele  kwa ukimya na kwa nguvu, anaipeleka mbele kwasababu ni ule utashi wa Mungu anaotaka utimilizike.
Mtakatifu Yosefu ni mtu anayeweza kutueleza mambo mengi lakini haongei, ni mtu anaye jificha, ni mtu mkimya , ambaye anayo madaraka makubwa kwa wakati huo, lakini hauoneshi. Baba Mtakatifu Francisko anachambua kwamba mambo ambayo Mungu anamwaminisha  katika moyo wa Yosefu , ni mambo madhaifu ya ahadi ambayo ni ahadi ya dhaifu .Kam vile kuzaliwa kwa mtoto, kukimbilia Misri,haya ni mambo ya hali ya udhaifu. Lakini Yosefu anayachukua katika moyo wake na kuendelea mbele, mambo hayo madhaifu. Je ni namna gani ya kupeleka mbele mambo madhaifu? Anasema ni kwa njia ya kubembeleza  kama vile umchukuavyo mtoto mdogo mikononi.

Ni mtu asiye ongea bali yeye anatii, ni mtu mwema ni mtu mwenye uwezo wa kuchukua mbele ahadi kwasababu iweze kuwa imara na salama, ni mtu anaye hakikishia msimamo wa Ufalme wa Mungu, ubaba wa Mungu , ni sehemu ya kuwa watoto wake kama vile mtoto wa Mungu.
Baba Mtakatifu Francisko anasema kwamba, anataka kufikiria Yosefu kama kwamba ni msimamizi wa wadhaifu , yaani  udhaifu wetu pia kwani na pia nao uwezo wa kuzaa mambo mengi mazuri kutoka katika katika yale madhaifu yetu, ambazo ni dhambi zetu. Yosefu ni msimamizi wa udhaifu wetu ili imani yetu iweze kuwa imara. Yosefu ni mtu wenye uwezo wa kuota, anachambua Baba Mtakatifu , na hivyo  yeye ni msimamizi wa ndoto ya Mungu. Kwa maana ndoto ya Mungu  ni kuwakoa wote,na  kukomboa ndiyo kazi aliyo kabidhiwa.Fundi Seremala huyo ni mkubwa! Anasema Baba Mtakatifu Francisko, kwani katika ukimya, anafanya kazi, analinda, na kuchua mbele udhaifu kwani anao uwezo wa kuota ndoto.Kwa njia hiyo ni Yosefu ni sura yenye kutoa ujumbe kwa watu wote.

Anamaliza akisema, ni kumuomba  Yosefu aweze kutupatia uwezo wa kuota kwasababu tukiota mambo makubwa , mambo mema, tunakaribia ndoto ya Mungu ,kwa maana ndiyo ndoto ya Mungu anayoota kwa ajili yetu.Na kwa ajili ya Vijana kama vile alivyo kuwa naye kijana  awawzeshe uwezo wa kuota kujihatarisha na kuchua wajibu wa mazoezi magumu ambayo wameona katika ndoto zao.
Na kwa wote Mtakatifu Yosefu aweze kutusaidie tuwe  waaminifu  ambao tukuze mitindo ya haki, kwasababu yeye alikuwa mwenye haki , na kuishi katika ukimya , kuwa na maneno machache, kukua katika ukarimu na uwezo wa kutunza udhaifu wetu binafsi na hata wa wengine.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahuli ya Radio vatican