2017-03-18 16:48:00

Mons. Andrzej Jozwowicz ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Rwanda


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Andrzej Jozwowicz kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Rwanda na kumpandisha hadhi ya kuwa Askofu mkuu. Askofu mkuu mteule Andrzej Jozwowicz alizaliwa kunako tarehe 14 Januari 1965. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 24 Mei 1990 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre, Jimbo Katoliki Lowicz, nchini Poland. Ana shahada ya uzamivu katika sheria. Taarifa zinaonesha kwamba, alianza utume wa masuala ya kidiplomasia mjini Vatican tarehe 1 Julai 1997 na tangu wakati huo, ametekeleza dhamana na utume wake nchini Msumbiji, Thailand, Hungaria, Syria, Iran na Russia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.