Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:
Radio Vatican

Maskani / Baba Mtakatifu Francisko / Katekesi siku ya Jumatano

Baba Mtakatifu Francisko ametoa wito wa kusaidia Sudan kusini


Mara baada ya katekesi yake , Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 22 Februari 2017 kama kawaida yake aliwasalimia mahujaji wote kutoka pande zote dunia waliofika kwenye viwanja vya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro kumsikiliza,pamoja na salam hizo bado ametoa wito wa nguvu kwa nchi ya Sudan ya Kusini inayokabiliwa na migogoro ya kivita  na kusababisha watu wengi waendelee kuteseka na baa la njaa. Kwa mujibu wa habari za Umoja wa Mataifa zinasema ni mamilioni ya wameathirika kwa ukosefu wa chakula katika ukanda wa pembe ya Afrika, kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anataka utolewe msaada wa dhati kwa ajili ya watu hao.

"Ni wasi wasi na uchungu wa kusikia habari kutoka katika nchi Sudan ya kusini , ambako kumekuwa na migogoro ya kivita, na kuongezeka pia ukosefu mkubwa wa chakula, na kusababisha vifo vya mamilioni ya watu, ikiwa ni pamoja na watoto wengi. Kwa wakati huu ni muhimu zaidi  kuwajibika wote bila kusimama mbele ya kauli tu , kwa njia ya matendo ya dhati ili kutoa misaada ya chakula na kufanya kwamba hiyo misaada inawafikia watu wanaoteseka. Bwana awadumishe ndugu zetu na wale ambao wanafanya kazi kuwasaidia.

 

Akiwasalimia vijana wote, wagonjwa na wana ndoa wapya , anawakumbusha juu ya sikukuu ya Ukulu wa Petro mtume , ambayo imeangukia siku ya katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko siku ya Jumatano 22 Februari 2017, anasema ni siku ya pekee kwa waamini wote wakiwa na Khalifa wa Mtakatifu Petro kwenye Makao yake makuu. Na hivyo, anawatia moyo vijana kujikita kwa kina katika sala zao kwa ajili ya utume wake .Na Wagonjwa anawashukuru kwa ushuhuda wa maisha yao wanayo toa katika mateso kwaajili ya ujenzi wa jumuiya ya Kanisa, vilevile kwa wana ndoa wapya anasema wajenge familia zao katika upendo ule ule unao waunganisha na Bwana Yesu na Kanisa lake.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.