Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:
Radio Vatican

Maskani / Kanisa / Kanisa Ulimwenguni

Kongamano kuhusu Bikira Maria kufanyika Cebu nchini Ufillippini


Kongamano linalowakilisha Jubilei ya Mama Maria wa msaada limefunguliwa tarehe 16 Februari 2017 katika madhabahu kwanye  mji wa Cebu nchini Ufillippini chini ya usimamizi wa Mapadri wa Shirika la Redentoristi.Pamoja na Kongamano hilo mada zikazo  tolewa  hazitawasilisha mada za kirohotu peke yake, bali hata kujikita katika  mada nyeti  za kijamii , kama vile Kampeni ya Serikali ya Taifa kupinga madawa ya kulevya kwani inasemekana watu zaidi ya 7,600 wameathirika kwa kipindi cha miezi sita. Ni habari zilizo jaza kurasa za magazeti na kuleta mgawanyiko mkubwa  kati ya Kanisa Katoliki na Serikali ya Rais Duterte.Padre wa Shirika la Redentoristi  Cris Mostajo anaeleza hayo katika Shirika la Habari la fides akionesha pia ratiba kamili ya shughuliza za Kongamano linalo adhimisha miaka 150 tangu  kufika kwa picha ya mama Maria wa  msaada.


Ni  zaidi ya washiriki 700 katika Kongamano hilo ,japokuwa  Padre Cris anasema , hatuna furaha hata kama  waamini wa kifilipini ni wafuasi wa Bikira Maria, kwasababu hawajali juu ya utamaduni wa kifo. Anasema “leo hii tunajikuta mbele ya huzuni wa hali halisi ya nchi , ambapo mambo matakatifu na hasa ya maisha ya binadamu ni ukiukwaji tu , kwa kudai kwamba kufanya usafi  katika kuondoa  watu wasio tamaniwa, kwa njia hiyo bado kuna haja  ya imani ambayo iweze kujikita kwa kina ndani ya maisha ya waamini wa Ufillippini “.


Katika Kongamano pia mada nyingine itahusu nafasi ya wanawake katika Kanisa, na mapokeo ya mama Maria nchini Ufillippini.Hali kadhalika Padre Cris anasema, sakramenti ya kitubio inaweza kuwa kiini cha uongofu binafsi wa watu, kwa  mfano mtu mlevi na anayetumia madawa ya kulevya wakifika kuungama ni mojawapo ya njia ya kuanza hatua ya uponyaji na kujifunza.Anasema hayo kutokana na uzoefu kwani Mapadri hao wana andaa kozi mbalimbali za kuwasindikiza watu wanao pambana na udhaifu ili kuondokana na hali hiyo ya ulevi , madawa ya kulevya na kamali.Halikadhalika shuhuda kadhaa zitatolewa na mwamisionari, walimu na wenye ndoa.

 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican