2017-02-16 15:15:00

Mashirika ya watawa Malawi tambueni mabadiliko ya jamii ya sasa


Askofu George Desmond Tambala wa Jimbo la Zomba na Rais wa umoja wa watawa wa kike na kiume  nchini Malawi, amewataka watawa kujikita katika mabadiliko ya  Jamii , kiuchumi na kisiasa kwamba ni kuingia katika uzoefu wa ulimwengu ikiwemo nchi ya Malawi.
Askofu Tambala aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa  57 wa mwaka wa Umoja wa watawa Katoliki nchini Malawi, ambapo siku nne za mkutano huo zilifanyikia mjini Lilongwe. Askofu anasema kwasasa jamii ya Malawi inaendelea kubadilika kwa kina ambapo watawa wa kike na kiume hawana budi kwa makini kupokea mabadiliko hayo.


Jamii inabadilika, na hasa kuona namna ya kumfikiria Mungu, na maadili, ni mabadiliko ya kutokumjua Mungu katika maisha ya raia, kwenye mtazamo wa kumuondolea mtu haki zake, uhuru wake, hadi kufikia kupoteza maana ya historia na maendeleo endelevu ya mtu.Anasema Askofu Tambala.Askofu huyo ambaye pia ni mtawa wa Shirika la Wakarmeli, anasema,sera za kisiasa kwa upande wa wanasisa na vyama pia vina changia suala hili,badala ya siasa kujikita katika kueneza na kuendeleza  mabadiliko chanya ya jamii.
Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa watawa Sr Mary Madalen Ndawala, anasema katika Mkutano wenye kauli mbiu “ kuingia kwa mabadiliko ya Ulimwengu ndani ya maisha ya kitawa”, umekuwa ni muhimu sana kwa kuudhuliwa na wakuu wa mashirika 28 kutoka katika mashirika mbalimbali ya wanawake wanao hudumia Bwana katika majimbo mbalimbali nchini Malawi.


Na kwamba lengo kubwa ni kuwahimarisha watawa kwa kile ambacho tayari ulimwengu umepokea, kwani wakuu wa mashirika ni viongozi ambao wanapaswa kujua mabadiliko ya ulimwengu wa sasa na kwa njia hiyo waweze kufanya uzoefu  kama viongozi wa mashirika yao.Hali kadhalika kama kiongzoi ndani ya Jumuiya anapaswa kuwa mtaalamu wa uchumi, jamii na  mabadiliko ya kisiasa yanayotokea na kwa njia hiyo anahitaji kubadilsiaha uzoefu wake na wengine kwa kile ambacho amekipokea kutoka katika mkutano huu na hivyo  anasema ,tunatarajia viongozi wa mashirika walio udhuria mkutano huo wapate kuwashirikisha watawa wenzao mara warudipo katika jumuiya zao.


Aidha anasema kwa upande wa mabadiliko ya uchumi , tunataka hawali ya yote iwe chemichemi katika uendeshaji na kujitegemea,pia katika mabadiliko ya kijamii, ni lazima kukumbatia aina mpya za kiteknolojia , lakini kuifanya kwa uangalifu na uwajibika kama njia mojawapo ya kwanza ya uinjilishaji katika jamii.Sr Ndawala pia anasema pamoja na kwamba sisi siyo wasaidizi lakini pia ni jukumu letu kushauri wanasiasa inapobidi ushiriki wetu katika siasa.Kati ya waliondesha mkutano wa mwaka ni pamojana na  Padre  Andrew Kaufa, kutoka katika Shirika la wamisionari wa Montfort (SMM) na Mkurugenzi wa Televisheni ya Luntha Padre Emmanuel Chikaya wa Shirika la Kitawa la Wakarmeli


Na  (Prince Henderson in Malawi)

 








All the contents on this site are copyrighted ©.