Katika jitihada za kuendelea kulea na kulinda watoto,Idara ya kichungaji ya AMECEA
imeandaa semina mbayo inalenga jinsi gani mkutano ya Baraza la Maaskofu Kitaifa na
majimbo wamekabiliana namna gani kujibu sula hli kwa miaka hii.
Ni wiki mbili za semina iliyo anza huko Malindi nchi Kenya kuanzia tarehe 12 hadi
25 Februari 2017. Semina hiyo ina washiriki 40 kutoka miongoni mwa nchi tano za AMECEA
ambao ni wajumbe kutoka Ethiopia,Kenya,Malawi, Sudani ya Kusini na Zimbabwe.Mkutano
huo pia unaudhuliwa na Sr Kayula Lesa mjumbe wa tume kwa ajili ya ulinzi wa watoto
Vatican, Askofu wa Jimbo la Malindi Emanuel Barbara, Askofu wa Jimbo la Nakuru Maurice
Muhatia na katibu Mkuu wa Amecea Padri Ferdinand Lugonza.
Katika lengo kuu la kuanzisha muongozo wa kina juu ya sera za ulinzi wa watoto ni
kwamba kila Baraza la maaskofu wa kila Jimbo watatakiwa kuchota taratibu na kanuni
za pamoja ambazo zitawawezesha kusaidia kulea, kuheshimu na kulinda watoto katika
malezi yao.Aidha mpango huo pia una lengo la kujenga mazingira mazuri kwa ajili ya
watu na kutafuta njia mbalimbali za kulinda watoto na watu wanao ishi katika mazingira
mangumu.Kwa njia hiyo hatimaye itawezesha Sekretarieti ya AMECEA kukusanya kutoka
katika mikutano ya Baraza juu ya maadili sahii ya ulinzi wa watoto kutokana na
kile ambacho watakuwa wamejifunza na kuchora ramani kamili ya sera zao watakazokuwa
wamekubaliana.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |