Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:
Radio Vatican

Maskani / Kanisa

Askofu mstaafu Fortunatus Lukanima amefariki dunia


Askofu mkuu Yuda Thaddaeus Ruwa'ichi wa Jimbo kuu la Mwanza, Tanzania, anasikitika kutangaza kifo cha Askofu mstaafu Fortunatus Lukanima wa Jimbo kuu la Arusha kilichotokea Jumatano tarehe 12 Machi 2014 katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza. Mipango ya mazishi inaendelea kufanywa Jimbo Kuu la Mwanza.

Marehemu Askofu mstaafu Fortunatus Lukanima alizaliwa tarehe 8 Desemba 1940 huko Irondo, Ukerewe. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu la Upadre hapo tarehe 8 Desemba 1968. Mwenyeheri Yohane Paulo II akamteua kuwa Askofu wa Jimbo la Arusha kunako tarehe 6 Machi 1989 na kuwekwa wakfu kuwa Askofu wa Jimbo la Arusha hapo tarehe 13 Agosti 1989. Askofu Lukanima akajiuzuru kutoka katika uongozi wa Jimbo la Arusha hapo tarehe 20 Julai 1998.

Raha ya milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele, umwangazie. Apumzike kwa Amani Amina.