Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:
Radio Vatican

Maskani / Kanisa

TANZIA: Askofu mstaafu Raymond Mwanyika wa jimbo Katoliki Njombe afariki dunia


Askofu mstaafu Raymond Mwanyika wa Jimbo Katoliki Njombe, amefariki dunia tarehe 24 Oktoba 2013, akiwa na umri wa miaka 83. Alizaliwa kunako mwaka 1930. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 11 Oktoba 1959.

Baba Mtakatifu Paulo wa sita, akamteua kuwa Askofu tarehe 16 Januari 1971 na hatimaye kuwekwa wakfu hapo tarehe 25 Aprili 1971. Baada ya kuwatumikia Watu wa Mungu, Jimbo Katoliki la Njombe kwa moyo na akili zake zote, akang'atuka kutoka madarakani hapo tarehe 8 Juni 2002.

Marehemu Askofu Raymond Mwanyika atakumbukwa na wengi kutokana na mchango wake mkubwa wa maendeleo endelevu kwa wananchi wa Njombe. Anatarajiwa kuzikwa hapo tarehe 29 Oktoba 2013.