
Papa Francisko anawataka wakleri na watawa kuwa na utambuzi binafsi wa wito wao; kutambua na kuthamini mwaliko wa maisha na utume wao pamoja na kuhakikisha kwamba, wanawashirikisha wengine ile furaha ya kukutana na Kristo Yesu.
Wakleri na watawa: zingatieni: utambuzi binafsi, mwaliko na furaha!
Baba Mtakatifu Francisko anawataka wakleri na watawa kukazia ile furaha ya utambuzi wa mtu binafsi kile anachotenda; pili watambue na kuthamini muda wa mwaliko wa kumfuasa Kristo kwani hii ni kumbu kumbu endelevu katika kumfuasa Kristo na kwamba, wajitahidi kushirikisha furaha ya Injili.
Mitandao ya kijamii: