Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Wakimbizi na wahamiaji

Bara la Afrika halina budi kuwekeza katika mchakato wa maendeleo endelevu na fungamani ya binadamu!

Bara la Afrika halina budi kuwekeza katika mchakato wa maendeleo endelevu na fungamani ya binadamu.

AMECEA: Wekezeni katika mchakato wa maendeleo endelevu na fungamani

22/07/2018 14:32

Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Endelevu na Fungamani ya Binadamu linawataka Mababa wa AMECEA kuhakikisha kwamba, wanawekeza zaidi katika sera na mikakati ya shughuli za kichungaji inayojikita katika huduma ya maendeleo endelevu na fungamani kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wengi.

Baba Mtakatifu Francisko asikitishwa na vifo vya wakimbizi na wahamiaji kwenye Bahari ya Mediterrania.

Baba Mtakatifu Francisko asikitishwa sana na vifo vya wakimbizi na wahamiaji kwenye Bahari ya Mediterrania aitaka Jumuiya ya Kimataifa kutenda kwa nguvu na ushupavu ili kuokoa maisha ya watu.

Papa Francisko awalilia wahamiaji wanaoendelea kufa maji baharini!

22/07/2018 14:14

Baba Mtakatifu Francisko anasikitika kuona kwamba, bado kuna wahamiaji na wakimbizi wanaendelea kufa maji huko kwenye Baharini ya Mediterrani, na hivyo anaitaka Jumuiya ya Kimataifa kutenda kwa nguvu na ushupavu ili kukomesha majanga haya ambayo kwa sasa yanaonekana kuzoeleka!

Baraza la Maaskofu Katoliki Italia linaitaka Serikali kujenga utamaduni wa ukarimu badala ya hofu!

Baraza la Maaskofu Katoliki Italia linaitaka Serikali na wadau mbali mbali kujenga utamaduni wa ukarimu kwa wakimbizi na wahamiaji badala ya hofu.

Tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki Italia kuhusu wahamiaji!

20/07/2018 15:08

Baraza la Maaskofu Katoliki Italia linaitaka Serikali pamoja na wadau mbali mbali kujenga utamaduni wa ukarimu, upendo na mshikamano kwa kuwakarimu wakimbizi na wahamiaji kama njia ya kupambana na utamaduni wa kifo unaofumbatwa katika mchakato mzima wa wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji.

VATICAN: Utu, heshima na haki msingi za binadamu zinapaswa kulindwa na kudumishwa.

VATICAN: Utu, heshima na haki msingi za binadamu zinapaswa kulindwa na kudumishwa.

Wakimbizi na wahamiaji: Usalama, utu, heshima na haki zao msingi!

20/07/2018 10:39

Jumuiya ya Kimataifa haina budi kujikita katika kutafuta kiini cha wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji duniani, ili kuweza kuibua mbinu mkakati utakaosaidia kwanza kabisa: kulinda na kudumisha: usalama, utu, heshima na haki msingi za wakimbizi na wahamiaji sehemu mbali mbali za dunia!

Mkataba wa Usalama wa Wahamiaji wa Mwaka 2018 uzingatie: utu, heshima na haki msingi za binadamu!

Mkataba wa Usalama wa Wahamiaji wa Mwaka 2018 uzingatie: haki msingi za binadamu, utu na heshima yao bila kujali mahali wanakotoka, dini au rangi yao.

Mkataba wa Usalama wa Wahamiaji 2018: Utu, heshima na haki msingi!

11/07/2018 16:27

Mkataba wa Usalama wa Wahamiaji Kimataifa wa Mwaka 2018 unapaswa kuboreshwa zaidi kwa kuzingatia: utu, heshima na haki msingi za binadamu kwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji wote bila ubaguzi, changamoto ambayo imetolewa na Askofu mkuu Bernardito Auza, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican, UN.

Papa Francisko: Changamoto ya wakimbiziishughulikiwe kwa njia ya mshikamano unaoongozwa na kanuni auni.

Papa Francisko: Changamoto ya wimbi kubwa la wakimbizi ishughukiwe kwa njia ya mshikamano unaoongozwa na kanuni auni.

Papa Francisko: Lampedusa: Changamoto ya Wakimbizi na Wahamiaji

06/07/2018 15:37

Baba Mtakatifu Francisko katika kumbu kumbu ya miaka mitano tangu alipotembelea Kisiwa cha Lampeduda, Kusini mwa Italia anakazia umuhimu wa Jumuiya ya Kimataifa kushikamana kwa kuongozwa na kanuni auni ili kukabiliana na wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji duniani kwa wakati huu.

Papa Francisko tarehe 8 Julai 2013 alitembelea Kisiwa cha Lampedusa, Kusini mwa Italia! Imegota miaka mitano tangu wakati huo!

Papa Francisko tarehe 8 Julai 2013 alitembelea Kisiwa cha Lampedusa, sasa imegota miaka 5 tangu atembelee Kisiwani hapo!

Papa Francisko: Miaka 5 tangu atembelee Kisiwa cha Lampedusa

05/07/2018 08:45

Baba Mtakatifu Francisko tangu mwanzo wa utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro ameguswa sana na mahangaiko ya wakimbizi na wahamiaji kiasi cha kuanzisha kitengo maalum kwa ajili ya kushughulikia changamoto hii kwa kujikita katika: Kuwapokea, Kuwalinda, Kuwaendeleza na Kuwahusisha!

Maskini wapamba sherehe ya kumpongeza Kardinali Konradi Krajewski, mtunza sadaka mkuu wa Kipapa!

Maskini wapamba sherehe ya kumpingeza Kardinali Konrad Krajewski, Mtunza sadaka mkuu wa Kipapa.

Papa Francisko aungana na maskini kumpongeza Kardinali Konrad

30/06/2018 16:15

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 28 Juni 2018 ameungana na maskini, wakimbizi, wahamiaji na wafungwa waliomaliza adhabu zao kumpongeza Kardinali mpya Konrad Krajewski, Mtunza sadaka mkuu wa Papa, kama alama ya sadaka na majitoleo kwa ajili ya wanaotengwa na jamii!