Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vitendo vya kigaidi

Kardinali Pietro Parolin katika ziara yake ya kikazi nchini Russia anakazia uhusiano wa kidiplomasia na majadiliano ya kiekumene katika damu na huduma

Kardinali Pietro Parolin katika ziara yake ya kikazi nchini Russia anakazia uhusiano wa kidiplomasia na majadiliano ya uekumene wa damu na huduma makini kwa maskini na wahitaji zaidi.

Yanayojiri katika ziara ya kizazi ya Kardinali Parolin nchini Russia

23/08/2017 10:24

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kuanzia tarehe 20 hadi 24 Agosti 2017 anafanya hija ya kihistoria nchini Russia ili kukuza na kudumisha uhusiano wa kidiplomasia ili kukabiliana na changamoto mamboleo leo pamoja na kukuza majadiliano ya uekumene wa damu na huduma makini!

Papa Francisko ana laani vitendo vyote vya kigaidi kwani ni kinyume kabisa cha utu wa binadamu.

Papa Francisko ana laani kwa nguvu zote vitendo vya kigaidi ambavyo ni kinyume cha utu na heshima ya binadamu!

Papa Francisko alaani vitendo vya kigaidi huko Barcellona

18/08/2017 14:08

Shambulio la kigaidi lililotokea huko Barcellona, tarehe 17 Agosti 2017 limesababisha watu zaidi ya 13 kupoteza maisha, wengine 90 kujeruhiwa vibaya na kati yao kuna watu 15 ambao hali zao ni mbaya sana! Baba Mtakatifu Francisko analaani kwa nguvu zote vitendo vya kigaidi kwani ni kinyume cha utu!

Papa Francisko asikitishwa sana na mauaji ya waamini waliokuwa wanasali, Jumapili tarehe 6 Agosti 2017 huko Ozubulu, Nigeria.

Papa Francisko asikitishwa sana na mauaji ya waamini waliokuwa wanasali kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Filipo, huko Ozubulu, Kusini mwa Nigeria.

Papa Francisko asikitishwa na shambulizi dhidi ya Wakristo Kanisani!

07/08/2017 14:53

Wakati wa maadhimisho ya Siku kuu ya Kung'ara Bwana, Jumapili tarehe 6 Agosti 2017 waamini wa Kanisa la Mtakatifu Filipo, Jimbo Katoliki Nnewi, nchini Nigeria walijikuta wanashambuliwa kwa risasi, hali iliyosababisha watu 11 kupoteza maisha na wengine 18 kujeruhiwa vibaya sana!

Tarehe 31 Julai 2017 ni Siku ya Mashahidi wa Imani kwa Makanisa ya Mashariki

Tarehe 31 Julai 2017 ni Siku ya Mashahidi wa Imani kwa Makanisa ya Mashariki, kumbu kumbu endelevu ya Mwaka wa Mashahidi wa Imani kwa Makanisa ya Mashariki.

31 Julai 2017 Siku ya Mashahidi na Wafiadini wa Makanisa ya Mashariki

31/07/2017 10:05

Waamini wa Makanisa ya Mashariki kuanzia sasa kila mwaka ifikapo tarehe 31 Julai watakuwa wanaadhimisha Siku ya Mashahidi wa Imani kwa Makanisa ya Mashariki, kama sehemu ya kumbu kumbu endelevu ya maadhimisho ya Mwaka wa mashahidi wa imani na wafiadini kutoka Makanisa ya Mashariki.

Papa Francisko anasema, utume ni kiini cha imani ya Kikristo!

Papa Francisko anasema, utume ni kiini cha imani ya Kikristo!

Papa Francisko asema, utume ni kiini cha imani ya Kikristo!

04/06/2017 14:51

Baba Mtakatifu Francisko amechapisha ujumbe wa Siku ya Kimissionari Duniani inayoadhimishwa na Mama Kanisa, Jumapili ya mwisho wa Mwezi Oktoba ya kila mwaka. Kwa mwaka 2017 kauli mbiu ni " Utume ni kiini cha imani ya Kikristo". Anamwomba Roho Mtakatifu kuendelea kulienzi Kanisa lake!

Sherehe ya Pentekoste imekuwa ni fursa kwa Kanisa kusali kwa ajili ya mahitaji ya familia ya Mungu sehemu mbali mbali za dunia.

Sherehe ya Pentekoste imemkuwa ni fursa ya kusali kwa ajili ya kuombea mahitaji ya familia ya Mungu, sehemu mbali mbali za dunia!

Sala ya Kanisa kwa ajili ya mahitaji ya familia ya Mungu!

04/06/2017 14:36

Katika maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya Sherehe ya Pentekoste kwa Mwaka 2017, Waamini wamesali kwa ajili ya kuliombea Kanisa, viongozi wa Jumuiya ya Kimataifa ili waweze kutafuta na kudumisha misingi ya haki na amani ya kweli, wamewakumbuka waamini wanaoteseka pia!

Watu zaidi ya 80 wamefariki dunia na wengine 350 kujeruhiwa vibaya kutokana na shambulizi la kigaidi huko Kabul, Afghanistan.

Watu zaidi 80 na wengine 350 wamejeruhiwa vibaya kutokana na shambulizi ya kigaidi huko Afghanistan.

Papa Francisko asikitishwa sana na shambulizi la kigaidi huko Kabul!

31/05/2017 15:28

Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa sana na mauaji ya watu zaidi ya 80 na wengine 350 kujeruhiwa vibaya kutokana na shambulizi la kigaidi lililotokea huko mjini Kabul, nchini Afghanistan. Anapenda kuwaombea marehemu wote pumziko la milele na majeruhi kupona na kurejea tena katika shughuli zao.

Viongozi mbali mbali wa Makanisa na Kijamii wanalaani mauaji ya kigaidi yaliyotokea nchini Misri.

Viongozi mbali mbali wa Makanisa na Jamii wanalaani majuaji ya kigaidi yaliyotokea huko Misri

Papa: Shambulizi la kigaidi huko Misri ni kitendo cha kinyama sana!

27/05/2017 15:10

Baba Mtakatifu Francisko anaungana na viongozi mbali mbali wa Makanisa kulaani kwa nguvu zote kitendo cha kigaidi kilichopelekea mauaji ya watu 28 kuuwa kikatili na wengi wao walikuwa ni watoto waliokuwa wanakwenda kusali. Anaombe mchakato wa haki, amani na maridhiano nchini Misri.