Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Utunzaji bora wa mazingira

Bara la Afrika halina budi kuwekeza katika mchakato wa maendeleo endelevu na fungamani ya binadamu!

Bara la Afrika halina budi kuwekeza katika mchakato wa maendeleo endelevu na fungamani ya binadamu.

AMECEA: Wekezeni katika mchakato wa maendeleo endelevu na fungamani

22/07/2018 14:32

Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Endelevu na Fungamani ya Binadamu linawataka Mababa wa AMECEA kuhakikisha kwamba, wanawekeza zaidi katika sera na mikakati ya shughuli za kichungaji inayojikita katika huduma ya maendeleo endelevu na fungamani kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wengi.

Waraka wa kitume wa Papa Francisko "Laudato si" ni mwongozo na dira katika mchakato wa utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote.

Waraka wa Kitume wa Papa Francisko "Ladato si" ni dira na mwongozo wa utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote.

Kumbu kumbu ya miaka mitatu ya "Laudato si" dira na mwongozo wa maisha

05/07/2018 14:11

Waraka wa Baba Mtakatifu Francisko "Laudato si" umejikita katika ekolojia fungamanishi ninayowataka watu kuishi kwa furaha na katika ukweli, kwa kutambua kwamba, kuna uhusianoi wa karibu sana kati ya mazingira, haki kwa maskini, amani na utulivu wa ndani; kilio cha mama dunia ni kilio cha maskini.

Nishati mpito na utunzaji bora wa mazingira ni mjadala unaojikita katika umuhimu, changamoto, hatari na mbinu mkakati wa kuendeleza nishati rafiki!

Nishati mpito na utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote ni mjadala unaopania kupembua umuhimu, fursa, changamoto, sera na mikakati ya nishati bora zaidi kwa ajili ya maendeleo endelevu ya binadamu.

Umuhimu wa nishati mpito, changamoto na fursa za maendeleo endelevu!

09/06/2018 16:18

Nishati mpito na utunzaji wa mazingira nyumba ya wote: mjadala kuhusu hatari, fursa, changamoto na njia muafaka za utekelezaji ni mambo msingi yaliyojadiliwa kwenye kongamano la kimataifa lililoandaliwa na Baraza la Kipapa la huduma ya maendeleo endelevu ya binadamu na Nostre Dame.

Hati ya Maandalizi ya Sinodi ya Maaskofu wa Amazonia inalitaka Kanisa; Kuona, Kung'amua na Kutenda.

Hati ya Maandalizi ya Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia, inalitaka Kanisa: Kuona, Kung'amua na Kutenda kwa ari na moyo mkuu.

Hati ya Maandalizi ya Sinodi ya Amazonia: Kuona, Kung'amua na Kutenda

09/06/2018 15:50

Maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia yatakayofanyika mjini Vatican mwezi Oktoba 2019 kwa kuongozwa na kauli mbiu "Amazonia: njia mpya ya Kanisa na kwa jili ya ekolojia endelevu". Hati ya maandalizi ya Sinodi ya Amazonia inakazia umuhimu wa: kuona, kung'amua na kutenda!

Patriaki Bartolomeo wa kwanza: Changamoto za kiekolojia zinahitaji umoja na mshikamano wa Jumuiya ya Kimataifa.

Patriaki Bartolomeo wa kwanza: Changamoto za kiekolojia zinahitaji umoja na mshikamano wa Jumuiya ya Kimataifa ili kuzipatia ufumbuzi.

Patriaki Bartholomeo: Athari za kiekolojia zinahitaji majibu ya pamoja

07/06/2018 11:13

Patriaki Bartolomeo wa kwanza wa Kanisa la Kiorthodox  la Costantinopol anasema, athari za kiekolojia zinatishia umoja na mafungamano ya kiuchumi na kijamii na kwamba, waathirika wakuu ni maskini na wale wote wanasukumizwa pembezoni mwa jamii. Changamoto hii inahitaji mshikamano wa dhati!

Papa Francisko: Utunzaji bora wa mazingira ni dhamana na wajibu wa kila binadamu. wote

Papa Francisko asema. utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote ni dhamana na wajibu wa kila mtu.

Papa Francisko: Mediterrania imegeuka kaburi la wakimbizi na wahamiaji

07/06/2018 10:49

Baba Mtakatifu Francisko anasikitika kusema kwamba, pamoja na uzuri wote wa Bahari ya Mediteraniani, lakini sasa imegeuka kuwa ni kaburi lisilo na alama kwa wahamiaji na wakimbizi. Uchafu na uharibifu wa mazingira ni dalili za kukengeuka kwa mwanadamu katika imani, maadili na utu wema!

 

Papa Francisko akutana na kuzungumza na Waziri mkuu wa Poland Bwana Mateusz Morawiecki mjini Vatican.

Papa Francisko akutana na kuzungumza na Waziri mkuu wa Poland Bwana Mateusz Morawieck mjini Vatican.

Waziri mkuu wa Poland akutana na Papa Francisko mjini Vatican

05/06/2018 09:29

Uhusiano mwema wa kidiplomasia kati ya Vatican na Poland, Ushirikiano kati ya Kanisa na Serikali katika huduma kwa watu wa Mungu na changamoto ya wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji ni kati ya mambo ambayo Papa Francisko na Balozi wa Poland wamejadili katika mazungumzo yao!

Patriaki Bartolomeo wa kwanza anasema, mafao ya wengi ni ajenda na kiekumene!

Patriaki Bartolomeo wa kwanza anasema, mafao ya wengi ni ajenda ya kiekumene.

Patriaki Bartolomeo wa kwanza: Mafao ya wengi ni ajenda ya kiekumene

26/05/2018 14:55

Patriaki Bartolomeo wa kwanza anasema, mafao ya wengi ni ajenda ya pamoja kwa wakristo wote ili kusaidia maboresho katika sekta ya uchumi na ekolojia; sayansi na teknolojia; jamii na siasa; kwa kusimama kidete: kulinda na kutetea utu, heshima, ustawi, maendeleo na mafao ya wengi!