Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Utume kwa vijana

Papa Francisko anawaalika viongozi wa Kanisa kujisadaka bila ya kujibakiza ili kulinda, kutetea na kudumisha utu na heshima ya binadamu.

Papa Francisko anawaalika viongozi wa Kanisa kujisadaka bila ya kujibakiza ili kulinda, kutetea na kudumisha utu na heshima ya binadamu.

Papa Francisko: Injili ya Kristo iwe ni chachu ya kulinda utu wa watu

20/06/2017 17:05

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika viongozi wa Kanisa kujitoa bila ya kujibakiza kwa ajili ya Kristo na Kanisa lake; kwa njia ya huduma makini kwa waamini katika mahitaji yao msingi ili hatimaye, kusimama kidete: kulinda na kutetea utu, heshima na haki msingi za binadamu na hasa maskini zaidi!

 

Utume ni kiini cha imani ya Kikristo ndiyo kauli mbiu inayoongoza ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya 91 ya Kimissionari Duniani.

Utume ni kiini cha imani ya Kikikristo ndiyo kauli mbiu inayoongoza maadhimisho ya Siku ya 91 ya Kimissionari Duniani kwa mwaka 2017.

Ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya 91 ya Kimissionari Duniani 2017

06/06/2017 14:33

Utume wa Kanisa unaelekezwa kwa watu wote wenye mapenzi mema na unasimikwa katika msingi wa Injili inayoleta mabadiliko; inayoshirikisha furaha kwani ni chemchemi ya maisha mapya yanayobubujika kutoka kwa Kristo Mfufuka aliyewapelekea Roho Mtakatifu, hivyo Yesu ni njia, ukweli na uzima!

Kardinali Bagnasco anasema, vijana wana imani na matumaini ya Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Kardinali Angelo Bagnasco anasema, vijana wana imani na matumaini kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Vijana wana imani na matumaini kwa Kanisa la Kristo!

28/05/2017 14:00

Kardinali Angelo Bagnasco, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la genova, Italia anasema kwamba, vijana wengi wa kizazi kipya Jimboni mwake wana imani na matumaini kwa Khalifa wa Mtakatfu Petro na Kanisa la Kristo na kwamba, wanataka kujenga mshikamano wa dhati katika maisha na utume wao.

Papa Francisko anawaalika vijana kujitahidi kukutana na Kristo Yesu katika maisha yao ili awagange na kuwaponya katika mahangaiko yao.

Papa Francisko anawaalika vijana wa kizazi kipya kujitahidi kukutana na Kristo Yesu katika hija ya maisha yao ili aweze kuwaganga na kuwaponya katika shida na mahangaiko yao.

Wosia wa Baba Mtakatifu Francisko kwa vijana wa kizazi kipya!

28/05/2017 13:44

Baba Mtakatifu Francisko anawataka vijana wa kizazi kipya kujenga na kudumishaz utamaduni wa sala, tafakari na matendo ya huruma kwa jirani zao! Ikiwa kama kweli wanataka kuwa ni wamissionari wanapaswa kuwapenda, kuwathamini na kujisadaka kwa ajili ya vijana wenzao wenye shida na mateso!

Katika Kanisa la Mtakatifu Mama  Maria Msaada wa Wakristo huko Torino nchini Italia, 24 Mei 2017 Misa Takatifu imeongozwa na  Askofu Mkuu C.Nosiglia

Katika Kanisa la Mtakatifu Mama Maria Msaada wa Wakristo huko Torino nchini Italia, 24 Mei 2017 Misa Takatifu imeongozwa na Askofu Mkuu Cesare Nosiglia wa Jimbo Kuu la Torino.

Mahubiri ya 24 Mei 2017, Sikukuu ya Mama Maria Msaada wa Wakristo!

24/05/2017 15:10

Askofu Mkuu wa Torino amemkabidhi mama Maria vijana, familia,wagonjwa,wanaoteseka ambao daima wako rohoni mwake Mama wakati wa mahubiri yake kwenye Kanisa Kuu Mtakatifu Maria Msaada wa Wakristo tararehe 24 Mei 2017 wakati Kanisa Katoliki linaafanya kumbukumbu ya Mama Maria. 

 

Papa Francisko, tarehe 22 Mei 2017 amekutana na kuzungumza na Rais Michael D. Higgins wa Ireland.

Papa Francisko, tarehe 22 Mei 2017 amekutana na kuzungumza na Rais Michael D. Higgins wa Ireland.

Jumuiya ya Kimataifa iwekeze matumaini kwa vijana na familia!

22/05/2017 16:03

Kuna haja ya kwa Jumuiya ya Kimataifa kusimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha ustawi, maendeleo na mafao ya wengi; kwa kulinda utu, heshima na haki msingi za binadamu katika hatua zake zote za maisha! Haya ni kati ya mambo msingi yaliyojadiliwa na Papa Francisko pamoja na Rais wa Ireland.

 

Vijana, Imani na Mang'amuzi ya Miito & Furaha ya upendo ndani ya famili; ni msingi wa Sinodi ya Maaskofu 2018.

Vijana, Imani na Mang'amuzi ya Miito ni msingi wa maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu wa Vijana kwa mwaka 2018, ili kuwasaidia vijana kufanya maamuzi magumu katika maisha yao"!

Kardinali Baldisseri: maadhimisho ya Sinodi kwa jicho la kichina!

18/05/2017 10:27

Wosia wa Kitume wa Baba Mtakatifu Francisko "Furaha ya upendo ndani na familia" na Kauli mbiu ya maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana yaani "Vijana, Imani na Mang'amuzi ya Miito" ni nyenzo msingi katika maandalizi ya maisha na utume wa vijana wa kizazi kipya kwa sasa!

Baba Mtakatatifu anashutumu biashara ya madawa ya kulevya ambayo yanaharibu maisha ya vijana wengi.

Baba Mtakatatifu anashutumu biashara ya madawa ya kulevya ambayo yanaharibu maisha ya vijana wengi.

Vijana wasiwe na hofu ya kukabiliana na utamaduni wa uharibifu!

07/05/2017 09:32

Baba Mtakafu Francisko anabainisha mada ambayo mara nyingi amekuwa akisistiza kwa wote inayohusu masengenyo na kurudia kusema ni ugaidi wa kweli! kwani ni uharibifu wa watu, kwa maana hiyo anawashauri vijana wajiume midomo yao kabla ya kutoa maneno ya kusema wengine vibaya