Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Upatanisho

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania linaitaka familia ya Mungu nchini Tanzania kuwa ni mashuhuda na vyombo vya haki na amani!

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania linaitaka familia ya Mungu nchini Tanzania kuwa ni mashuhuda na vyombo vya haki na amani, ili kujenga na kudumisha umoja, udugu na maridhiano kati ya watu!

Ujumbe wa Maaskofu Katoliki Tanzania: Iweni wakala wa haki na amani!

28/12/2017 15:01

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania katika ujumbe wake ulioandikwa na Askofu John Christostom Ndimbo wa Jimbo Katoliki Mbinga linaitaka familia ya Mungu nchini Tanzania kuwa ni vyombo na mashuhuda wa tunu msingi za haki na amani, ili kudumisha upendo, umoja na mshikamano wa kitaifa!

 

Papa Francisko anawataka wananchi wa Colombia kujipatanisha na Mungu na jirani zao, kukubali ukweli, kutubu na kuongoka!

Papa Francisko anawaka wananchi wa Colombia kujipatanisha na Mungu, Jirani na Mazingira! Kukubali ukweli ili kupokea na kutoa msamaha!

Tafakari ya Papa Francisko katika Liturujia ya Upatanisho wa Kitaifa

09/09/2017 14:07

Baba Mtakatifu Francisko anapenda kuwaalika watu wa Mungu nchini Colombia kujipatanisha na Mungu pamoja na jirani zao! Wasiogope ukweli na haki; kupokea na kutoa msamaha; kujipatanisha; kwa kujikita katika toba na wongofu wa ndani ili kujenga na kudumisha amani, haki, utu na heshima ya binadamu.

Upatanisho ni mlango unaomwezesha mwamini kugusa na kuonja huruma ya Mungu katika maisha yake na jirani zake!

Upatanisho ni mlango unaomwezesha mwamini kuonja huruma na upendo wa Mungu katika maisha!

Mchakato wa upatanisho wa upendo na kidugu!

08/09/2017 16:29

Baba Mtakatifu Francisko anasema, upatanisho ni mchakato unaomwezesha mwamini kushinda kishawishi cha ubinafsi na kutaka kujichukulia sheria mkononi kwa kulipiza kisasi. Ni njia ya kuonja tena na tena huruma na upendo wa Mungu katika maisha ya mwanadamu, ili kujenga amani ya kweli!

Maaskofu wa Jimbo Kuu la Owerri Nigeria wanasema hiki ni kipindi cha toba na wongofu wa ndani; amani, msamaha na upatanisho.

Maaskofu wa Jimbo kuu la Owerri, Nigeria wanasema hiki ni kipindi cha toba na wongofu wa ndani; msamaha, haki, amani na upatanisho wa kweli!

Nigeria ni wakati wa toba na wongofu wa ndani; msamaha na upatanisho

28/08/2017 09:19

Maaskofu wa kutoka Jimbo kuu la Owerri, Nigeria wanasema, sasa ni wakati wa toba na wongofu wa ndani; msamaha na upatanisho ilikujenga amani, ustawi na maendeleo ya wengi: kiroho na kimwili. Ni wakati wa kuganga na kuponya madhara ya vita, ghasia, chuki na uhasama kwa kukumbatia amani na utulivu.

Huruma na msamaha wa Mungu ni kielelezo cha upendo na mahangaiko ya Mungu kwa binadamu!

Huruma na msamaha wa Mungu ni kielelezo cha upendo na mahangaiko ya Mungu kwa binadamu!

Iweni na huruma na msamaha kama Baba yenu wa mbinguni!

22/07/2017 08:42

Kusamehe na kusahau ni kielelezo makini cha upendo wenye huruma, wajibu ambao unafungamana na maisha ya Wakristo! Baba Mtakatifu Francisko anasema, msamaha ni changamoto kwa binadamu kuwa na moyo mkunjufu kwa kuachilia: hasira, ghabu, ukatili na kisasi. Huruma ni jina la Mungu!

Baraza la Makanisa Ulaya, CEC linapinga Umoja wa Ulaya Kuanzisha Mfuko wa Ulinzi na badala yake fedha hii itumike kwa ajili ya upatanisho na maendeleo

Baraza la Makanisa Ulya, CEC linapinga Umoja wa Ulaya kutaka kuanzisha Mfuko wa Ulinzi Barani Ulaya na badala yake, fedha hii itumike kwa ajili ya kukuza mchakato wa upatanisho na maendeleo endelevu ya watu!

Umoja wa Ulaya wekezeni katika mchakato wa haki, amani na upatanisho!

12/07/2017 14:27

Baraza la Makanisa Ulaya, CEC, linautaka Umoja wa Ulaya kuwekeza zaidi katika shughuli za ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu kwa kuachana na sera za kutoa ruzuku na kugharimia tafiti za kijeshi pamoja na utengenezaji wa silaha Barani Ulaya, kwani itakuza utamaduni wa kifo!

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wananchi wa Colombia kuwa i vyombo na mashuhuda wa amani na upatanisho.

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wananchi wa Colombia kuwa ni mashuhuda na vyombo vya haki na amani.

Hija ya Papa Francisko inapania kupyaisha maisha ya watu wa Colombia

07/07/2017 15:40

Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kujipambanua kuwa ni mmissionari wa: haki, amani na upatanisho, changamoto na mwaliko kwa familia ya Mungu nchini Colombia kupiga moyo konde nakuanza kuchukua hatua ya kwanza katika mchakato wa upatanisho, haki, amani na maridhiano kati ya watu!

Baraza la Maaskofu Katoliki Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati wanaendelea kuhimiza kuhusu amani nchini mwao!

Baraza la Maaskofu Katoliki Jamhuri ya Watu wa Afrika ya kati linaendelea kuhimiza amani miongoni mwa wananchi wake.

Maaskofu Katoliki Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati wanataka amani!

03/07/2017 10:05

Haki, amani na upatanisho wa kweli ni juhudi za majadiliano katika ukweli na uwazi, kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wengi. Amani ya kweli inafumbatwa katika misingi ya: ukweli, uhuru, haki na upendo; mambo ambayo hadi sasa yanasua sua miongoni mwa watu wa Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati!