Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Umoja wa kitaifa

Papa Francisko anasema Chuo Kikuu ni mahali pa kukuza na kudumisha mchakato wa mabadiliko unaofumbatwa katika majadiliano na watu kukutana!

Papa Francisko anasema, Chuo Kikuu kinapaswa kuwa ni sehemu ya mchakato wa mabadiliko yanayofumbatwa katika majadiliano ya dhana ya watu kukutana.

Papa: Dhamana ya Chuo Kikuu ni kufundisha, kufikiri na kutenda

18/01/2018 08:36

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Chuo Kikuu ni mahali ambapo watu wanajifunza kufikiri na kutenda kama sehemu ya mchakato endelevu wa maisha ya mwanadamu. Chuo Kikuu kinapaswa kuwa ni sehemu ya mchakato wa mabadiliko yanayofumbatwa katika majadiliano na utamaduni wa watu kukutana!

Papa Francisko anawataka wananchi wa Chile kuwa ni mashuhuda na vyombo vya Injili ya haki, amani na upatanisho wa kitaifa!

Papa Francisko anawataka waanchi wa Chile kuwa ni mashuhuda na vyombo vya haki, amani na upatanisho wa kitaifa!

Papa: Heri wapatanishi na wenye kiu ya haki, wataitwa wana wa Mungu!

16/01/2018 15:49

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika wananchi wa Chile kuwa ni vyombo na mashuhuda wa upatanisho ili kujenga amani na umoja wa kitaifa, chemchemi ya kweli katika maisha. Wale wote wanaotamani amani, wanapaswa kujizatiti kuitafuta na kuimwilisha katika haki inayozingatia utu na heshima ya binadamu!

Maaskofu Katoliki Tanzania wanaitaka familia ya Mungu nchini humo kujenga na kudumisha misingi ya haki, amani, upendo na mshikamano wa kitaifa!

Maaskofu Katoliki Tanzania wanaitaka familia ya Mungu nchini humo kujenga na kudumisha misingi ya haki, amani, upendo na mshikamano wa kitaifa!

Changamoto kutoka kwa Maaskofu kwa familia ya Mungu nchini Tanzania

09/01/2018 10:30

Maaskofu Katoliki nchini Tanzania katika kipindi cha Noeli na Mwaka Mpya 2018 wametumia fursa hii kuitaka familia ya Mungu nchini Tanzania kujenga na kudumisha misingi ya haki, amani, upendo, na umoja wa kitaifa; kwa kukazia kanuni maadili, malezi na utu wema; pamoja na kudumisha majadiliano.

Askofu mkuu Anthony Muheria wa Jimbo Kuu la Nyeri, Kenya anawataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kudumisha upendo, umoja na amani!

Askofu mkuu Athony Muheria wa Jimbo Kuu la Nyeri, Kenya anawataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kujenga na kudumisha umoja, upendo, mshikamano na amani kama njia muafaka ya kuadhimisha Noeli ya Bwana!

Ujumbe wa Noeli kwa Mwaka 2017 kutoka kwa Askofu mkuu Muheria, Kenya

23/12/2017 08:49

Katika Sherehe ya Noeli, Mama Kanisa anaadhimisha kwa shangwe kubwa Fumbo la Umwilisho, Neno wa Mungu, Nafsi ya Pili ya Fumbo la Utatu Mtkatifu alipofanyika mwili kwa njia ya Roho Mtakatifu kwake Bikira Maria. Huu ni muungano wa ajabu wa asili ya Kimungu na asili ya kibinadamu ndani ya Kristo Yesu

Watanzania wametakiwa kudumisha na kuenzi muungano kaqma njia ya kuwaenzi waasisi wa Tanzania!

Watanzania wametakiwa kudumisha na kuenzi muungano kama njia halisi ya kuwakumbuka na kuwaenzi waasisi wa Tanzania.

Watanzania wametakiwa kudumisha na kuenzi muungano!

07/04/2017 14:50

Hostoria ya Tanzania inawakumbuka kwa namna ya pekee kabisa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na  Sheikh Abeid Amani Karume kama waasisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, dhamana ambayo watanzania wanapaswa kuivalia njuga, ili kuimarisha muungano na umoja wa kitaifa!

 

Ndoto ya kupata serikali ya Umoja wa Kitaifa DRC inafifia baada ya Baraza la Maaskofu Katoliki kujitoa kutokana na wanasiasa kushindwa kuonesha utashi

Baraza la Maaskofu Katoliki DRC limeamua kujitoa kwenye mchakato wa upatanisho wa kisiasa nchini humo baada ya wanasiasa kushindwa kuonesha utashi wa kisiasa wa kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Maaskofu DRC wajitoa katika mchakato wa utekelezaji wa mkataba wa 2016

29/03/2017 09:35

Ndoto ya familia ya Mungu nchini DRC kupata serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo ingekuwa na dhamana ya kuandaa uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge, imetoweka baada ya Baraza la Maaskofu Katoliki DRC kujitoa katika mchakato wa upatanisho wa kisiasa baada ya utekelezaji wake kukwamishwa!

Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo Mombasa: Umoja, Haki, Amani na Maridhiano!

Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo Jijini Mombasa: Umoja, Haki, Amani na Maridhiano kati ya wananchi wa Kenya kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wengi!

Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo Mombasa: Umoja na Mshikamano

17/01/2017 10:53

Familia ya Mungu Jijini Mombasa katika maadhimisho ya Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo Duniani kwa Mwaka 2017 inajielekeza zaidi katika mchakato wa ujenzi wa umoja unaowaambata watu wote, ili kudumisha misingi ya haki, amani, ustawi na maridhiano hasa wakati huu wa mchakato wa Uchaguzi mkuu.

Familia ya Mungu nchini Gambia inatakiwa kujikita katika haki, amani, umoja na mshikamano wa kitaifa hasa wakati huu wa machafuko ya kisiasa!

Familia ya Mungu nchini Gambia inatakiwa kujikita katika misingi ya haki, amani na umoja wa kitaifa hasa wakati huu wa machafuko ya kisiasa.

Gambia dumisheni amani na umoja wa kitaifa ili kuokoa maisha!

11/01/2017 11:35

Familia ya Mungu nchini Gambia inatakiwa kukuza na kudumisha misingi ya haki, amani, upendo, maridhiano na umoja wa kitaifa hasa wakati huu wa machafuko ya kisiasa baada ya Rais Yahya Jammeh kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwaka 2016.