Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Uinjilishaji mpya: ushuhuda na upendo

Shirika la Roho Mtakatifu lilianzishwa kunako tarehe 27 Mei 1703 na kujiweka wakfu chini ya Roho Mtakatifu na Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili.

Shirika la Roho Mtakatifu lilianzishwa kunako tarehe 27 Mei 1703 katika Sherehe ya Pentekoste na kujiweka chini ya ulinzi na tunza ya Roho Mtakatifu na B. Maria Mkingiwa Dhambi ya asili.

Miaka 315 ya maisha na utume wa Shirika la Roho Mtakatifu!

21/05/2018 15:14

Roho Mtakatifu ni Nafsi ya tatu katika Fumbo la Utatu Mtakatifu. Ni Bwana mleta uzima; atokaye kwa Baba na Mwana. Anayeabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana: Aliyenena kwa vinywa vya Manabii. Shirika la Roho Mtakatifu, Sherehe ya Pentekoste 27 Mei 1703 likaanzishwa, huko Ufaransa.

Vyombo vya mawasiliano ya jamii vina wajibu wa kujenga na kudumisha: utu, heshima, udugu na haki msingi za binadamu.

Vyombo vya mawasiliano ya jamii vinayo dhamana na wajibu wa kulinda, kutetea utu, heshima na haki msingi za binadamu sanjari na ujenzi wa udugu na utu wema.

Vyombo vya mawasiliano vilinde na kudumisha utu na heshima ya binadamu

12/05/2018 16:20

Baba Mtakatifu Francisko anasema, vyombo vya mawasiliano ya jamii vina dhamana na wajibu wa kulinda, kutetea na kudumisha utu na heshima ya binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Vijenge jamii inayomsikwa katika udugu na utu kadiri ya moyo wa Mwenyezi Mungu

Sherehe ya Kupaa Bwana Mbinguni inawaachia wakristo wajibu wa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu!

Sherehe ya Kupaa Bwana Mbinguni inawachia Wakristo wajibu na dhamana ya kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu hadi miisho ya dunia.

Leo mnatumwa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu!

11/05/2018 16:11

Ee Mungu Mwenyezi, utufanye tuwe na furaha takatifu na shukrani; kwa maana kupaa kwake Kristo Yesu, Mwanaoni mfano wetu; na huko alikotangulia yeye kichwa chetu, ndiko tunakotumaini kufika sisi tulio mwili wake. Leo ubinadamu wetu umetukuzwa mbinguni!

Yesu alipaa mbinguni, amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi.

Yesu alipaa mbinguni, amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi.

Kristo Yesu akishakuinuliwa juu, atawavuta wote kwake!

10/05/2018 16:31

Kristo Yesu peke yake ndiye aliyetoka kwa Baba na anaweza kurudi tena kwa Baba. Hakuna mtu aliyepaa mbinguni ile Yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani Mwana wa mtu! Ubinadamu ukiachiwa katika nguvu zake za maumbile hauwezi kufika kwenye nyumba ya Baba, kwenye uzima na furaha ya milele!

 

Masista Wamisionari Wabenediktini wa Tutzing wanapania kumhudumia mtu mzima: kiroho na kimwili kama sehemu ya ushuhuda wa furaha ya Injili!

Masista Wamisionari Wabenediktini wa Tutzing wanapania kumhudumia mtu mzima: kiroho na kimwili kama sehemu ya ushuhuda wa furaha ya Injili inayomwilishwa katika matendo!

Maisha na utume wa Masista wa Tutzing, Ndanda, Mtwara, Tanzania!

05/05/2018 15:23

Shirika la Masista Wamisionari Wabenediktini wa Tutzing lilianzishwa mwaka 1884 huko nchini Ujerumani na Padre Andreas Amrhein ili kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu kama sehemu ya mchakato wa uinjilishaji wa kina unaogusa mahitaji mtu mzima: kiroho na kimwili!

Mheshimiwa Abate Mstaafu Alcuin Maurus Nyirenda, OSB ametetea kazi yake ya shahada ya uzamivu, Chuo Kikuu cha Kipapa la Urbaniana.

Mheshimiwa Abate Mstaafu Alcuin Maurus Nyirenda, OSB ametetea kazi yake ya uzamivu Chuo Kikuu cha Kipapa la Urbaniana, kilichoko mjini Roma.

Abate mstaafu Alcuin Maurus Nyirenda, OSB aibuka kidedea!

04/05/2018 14:28

Mheshimiwa sana Abate Mstaafu Alcuin Maurus Nyirenda, OSB kutoka Monasteri ya Hanga, Jimbo kuu la Songea, Tanzania kwa utulivu, hali ya kujiamini huku akiwa amebeba uzoefu na mang'amuzi ya maisha na kimonaki, ametetea kazi yake kwa ufundi mkubwa kiasi cha Jopo la Maprofesa kushika tama!

Papa amewashauri mapadre wa Chama cha Prado watoe ushuhuda kama mwanzilishi wao, Mwenyeheri Padre Chevrier

Papa amewashauri mapadre wa Chama cha Prado watoe ushuhuda kama mwanzilishi wao, Mwenyeheri Padre Chevrier

Papa anawashauri Chama cha Mapadre wa Prado kuongea juu ya Yesu Kristo!

07/04/2018 17:17

Tarehe 7 Aprili 2018  Papa Francisko amekutana na Jumuiya ya familia ya mapadre wa Prado kutoka Ufaransa, katika Ukumbi wa mkutano mjini Vatican Papa Francisko anasema: Hata nyakati zetu,zinatambua umaskini wake ambao ni wa zamani na mpya kwa mfano wa mwanzilishi wao Padre Chevrier! 

 

Tarehe 7 Aprili 2018 Papa amekutana na Jumuiya ya Emanuele kutoka Ufaransa

Tarehe 7 Aprili 2018 Papa amekutana na Jumuiya ya Emanuele kutoka Ufaransa

Papa:Jumuiya ya Emanueli iwe na msingi wa kutafakari fumbo la Kristo !

07/04/2018 16:20

Papa Francisko amekutana na Jumuiya wa Emanueli kutoka nchini Ufaransa katika ukumbi wa Clementina Mjini Vatican,Jumamosi 7 Aprili 2018.Papa anasema,hija hii ni ishara kamili ya kushiriki katika Jumuiya ya Emanueli na umoja wa Kanisa zima Katoliki.Anawasifu wa ushuhuda na uaminifu wao.