Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Uinjilishaji

Papa Francisko ameyataka Makanisa Barani Afrika kushikamana kwa ajili ya kutangaza na kushuhudia Injili katika uhalisia wa maisha ya watu wao.

Papa Francisko ameyataka Makanisa Barani Afrika kushikamana kutangaza na kushuhudia Injili katika uhalisia wa maisha ya watu wao.

Papa Francisko: Makanisa Barani Afrika shikamaneni kwa dhati!

23/06/2018 16:21

Baba Mtakatifu Francisko amewaambia wajumbe wa Muungano wa Makanisa Huru Barani Afrika kushikamana ili kutangaza na kushuhudia Injili inayomwilishwa katika uhalisia wa maisha na vipaumbele vya watu, kwa kulinda, kutetea na kudumisha haki msingi za binadamu, umoja na upendo.

Ufalme wa Mungu hukua polepole na kuzaa matunda kwa wakati wake!

Ufalme wa Mungu hukua pole pole na kuzaa matunda kwa wakati wake, kila mwamini anaalikwa kushiriki katika ujenzi wake.

Ufalme wa Mungu: Unakua pole pole na kuzaa matunda kwa wakati wake!

15/06/2018 08:09

Mwenyezi Mungu anawaalika waja wake kushiriki katika mchakato wa ujenzi wa Ufalme wa Mungu unaosimikwa katika: kweli na uzima; utakatifu na neema; haki, upendo na amani. Ufalme hukua pole pole lakini uzaa matunda kwa wakati wake. Jambo la msingi ni kila mwamini kushiriki kikamilifu kuujenga!

 

Hati ya Maandalizi ya Sinodi ya Maaskofu wa Amazonia inalitaka Kanisa; Kuona, Kung'amua na Kutenda.

Hati ya Maandalizi ya Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia, inalitaka Kanisa: Kuona, Kung'amua na Kutenda kwa ari na moyo mkuu.

Hati ya Maandalizi ya Sinodi ya Amazonia: Kuona, Kung'amua na Kutenda

09/06/2018 15:50

Maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia yatakayofanyika mjini Vatican mwezi Oktoba 2019 kwa kuongozwa na kauli mbiu "Amazonia: njia mpya ya Kanisa na kwa jili ya ekolojia endelevu". Hati ya maandalizi ya Sinodi ya Amazonia inakazia umuhimu wa: kuona, kung'amua na kutenda!

Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Ukanda wa Amazonia ni mbinu mkakati wa shughuli za kichungaji katika ukanda huu.

Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Ukanda wa Amazoni ni mbinu mkakati wa shughuli za kichungaji kwa ajili ya ukanda huu.

Sinodi ya Maaskofu wa Amazonia 2019 ni mbinu mkakati wa uchungaji

30/04/2018 07:54

Maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Ukanda wa Amazoni kwa mwaka 2019 yanapania kuibua mbinu mkakati wa shughuli za kichungaji zinazofumbatwa katika: uinjilishaji na utamadunisho; ekolojia na utunzaji bora wa mazingira; utu, haki msingi za binadamu na mendeleo endelevu.

Mwenyezi Mungu ameweka Agano Jipya na la Milele kwa njia ya Damu Azizi ya Kristo Yesu Mkombozi wa Ulimwengu.

Mwenyezi Mungu ameweka Agano Jipya na la milele kwa njia ya Damu Azizi ya Kristo Yesu!

Ubatizo ni nguvu ya Kristo inayookoa na kutakasa!

17/02/2018 15:25

Sakramenti ya Ubatizo ni msingi wa maisha yote ya Kikristo, lango la kuingilia "uzima wa milele katika Roho". Huu ni mlango unaomwezesha mwamini kupata Sakramenti nyingine za Kanisa. Ubatizo unamwezesha mwamini kuzaliwa upya katika maisha na kuanza kutembea katika Mwanga wa Kristo Mfufuka!

Papa Francisko analitaka Shirika la Madonda Matakatifu kuwasha moto wa upendo na imani kwa njia ya huduma makini kwa maskini.

Papa Francisko analitaka Shirika la Madonda Matakatifu kuwasha moto wa imani na upendo kwa njia ya huduma makini kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii.

Wamissionari washeni moto wa imani na huduma kwa maskini duniani

10/02/2018 16:23

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wamissionari wa Shirika la Madonda Matakatifu kuwasha moto wa imani na huduma kwa watu wanaowainjilisha kwa njia ya ushuhuda unaofumbatwa katika furaha ya Injili wanayoitangaza na kuishuhudia katika upendo wa kidugu katika maisha ya kijumuiya!

 

Ushindi wa Kristo juu ya dhambi na mauti unafumbatwa katika unyenyekevu, mateso, kifo na ufufuko!

Ushindi wa Kristo Yesu juu ya dhambi na mauti unafumbatwa katika unyenyekevu, mateso, kifo na ufufuko kutoka wafu na wala hakuna njia ya mkato!

Ushindi wa Kristo Yesu unafumbatwa katika Fumbo la Msalaba!

03/02/2018 08:26

Mama Kanisa anatumwa kutangaza Habari Njema ya Wokovu na kuendeleza ile kazi ya ukombozi iliyoanzishwa na Kristo Yesu kwa njia ya Fumbo la Pasaka yaani: mateso, kifo na ufufuko wake. Kanisa linaendeleza kazi ya uinjilishaji inayofumbatwa katika huduma ya elimu, afya na maendeleo endelevu!

Mama Kanisa ni ushuhuda wa uwepo wa Ufalme wa Mungu: Anatumwa kuinjilisha, kuganga na kuwaponya watu wa Mungu.

Mama Kanisa ni ushuhuda wa uwepo wa Mungu. Anatumwa kuwaondolea watu dhambi zao, kuwaganga na kuwaponya magonjwa na udhaifu wao wa mwili, tayari kushiriki katika ujenzi wa Ufalme wa Mungu.

Mama Kanisa anainjilisha, ana ganga na kuwatakasa watu wa Mungu!

02/02/2018 07:26

Kanisa ni kielelezo makini cha uwepo wa Ufalme wa Mungu kati ya watu wa Mataifa. Linatumwa kuwa ni shuhuda wa kazi na utume ulioanzishwa na Kristo Yesu hapa duniani kwa kuwatangazia watu Habari Njema ya Wokovu, kwa kuwaondolea dhambi na kuwaponya magonjwa na udhaifu wao wa kibinadamu.