Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Uhuru wa kuabudu

Jumuiya ya Kimataifa haina budi kufanya maamuzi magumu ili haki, amani na maridhiano yarejeshwe tena huko Mashariki ya Kati

Jumuiya ya Kimataifa haina budi kufanya maamuzi magumu ili haki, amani na maridhiano kati ya watu yarejee.

Changamoto ya ulinzi na usalama Mashariki ya Kati na Palestina

26/07/2017 14:59

Vita, vurugu, ghasia na mipasuko ya kijamii huko Mashariki ya Kati inaendelea kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Jumuiya ya Kimataifa haina budi kusaidia mchakato wa majadiliano kati ya Israeli na Palestina ili amani, utulivu na maendeleo ya kweli yaweze kupatikana nchini humo!

Vatican itaendelea kusimama kidete kulinda, kudumisha na kutetea uhuru wa kuabudu sehemu mbali mbali za dunia.

Vatican itaendelea kusimama kidete kulinda, kutetea na kulinda uhuru wa kuabudu sehemu mbali mbali za dunia kama sehemu ya haki msingi za binadamu.

Uhuru wa kidini ni kitochu ya haki msingi za binadamu!

15/07/2017 14:11

Ni wajibu na dhamana ya viongozi wa kidini kuwaelimisha na kuwafunda waamini kutambua na kuthamini uhuru wa kidini unaotafsiriwa katika uhuru wa kuabudu kama njia ya kukuza na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu. Hiki ni kiini cha haki zote msingi za binadamu.

Papa Francisko amekutana na kuzungmza na rais Donald Trump wa Marekani mjini Vatican tarehe 24 Mei 2017

Papa Francisko amekutana na kuzungumza na Rais Donald Trump wa Marekani tarehe 24 Mei 2017.

Rais Donald Trump akutana uso kwa uso na Papa Francisko!

24/05/2017 14:04

Baba Mtakatifu Francisko amemzawadia Rais Donald Trump wa Marekani Nyaraka zake za kitume: Furaha ya upendo ndani ya familia; Furaha ya Injili na Sifa iwe kwako juu ya utunzaji wa nyumba ya wote pamoja na medali ya tawi la mzeituni, linalomkumbusha dhamana ya amani duniani!

Papa Francisko anakwenda nchini Misri kama mjumbe wa amani, haki na matumaini miongoni mwa familia ya Mungu nchini Misri!

Papa Francisko anakwenda nchini Misri kama mjumbe wa amani, haki na matumaini miongoni mwa familia ya Mungu nchini Misri.

Papa Francisko mjumbe wa amani nchini Misri!

27/04/2017 15:43

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anasema, Baba Mtakatifu Francisko anatambua fika changamoto za ulinzi na usalama; majadiliano ya kidini na kiekumene; misimamo mikali ya kidini na kiimani iliyoko nchini Misri ndio maana ameamua kwenda huko kama mjumbe wa amani na matumaini!

RECOWA-CERAO: changamoto kubwa: hali tete ya kisiasa; misimamo mikali ya kidini na majanga asilia.

RECOWA-CERAO: changamoto kubwa: hali tete ya kisiasa, kiuchumi na kijamii; misimamo mikali ya kidini na kiimani pamoja na athari za majanga asilia.

RECOWA-CERAO na changamoto zake Afrika Magharibi!

19/04/2017 11:12

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Magharibi linasema, linapenda kushirikiana kwa dhati na Jumuiya ya Uchumi Afrika Magharibi,ECOWAS ili kukabiliana na changamoto zinazoendelea kujitokeza katika Nchi wanachama wa RECOWA-CERAO hasa: vitendo ya kigaidi na misimamo mikali ya kidini

Viongozi mbali mbali wa kidini wamelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea nchini Misri, Jumapili ya Matawi, 9 Aprili 2017.

Viongozi mbali mbali wa kidini na kisiasa wamelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea nchini Misri, Jumapili ya Matawi 2017.

Mshikamano na uekumene wa damu na Wakristo nchini Misri!

10/04/2017 14:54

Mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika nchini Msiri Jumapili ya Matawi na kupelekea watu kadhaa kufariki dunia na wengine wengi kupata majeraha ni kinyume cha haki msingi za binadamu, uhuru wa kuabudu; umoja, mshikamano na mafungamano ya kijamii nchini Misri. Tukio hili linalaaniwa na wengi!

 

Askofu Mkuu IvanJurkovic anasema, kutokana na athari zinazojitokeza za dini, uchaguzi na mazoezi ya imani ya mtu lazima iwe huru bila vikwazo au kutum

Askofu Mkuu IvanJurkovic anasema, kutokana na athari zinazojitokeza za dini, uchaguzi na mazoezi ya imani ya mtu lazima iwe huru bila vikwazo au kutumia nguvu.

Uhuru wa dini ni haki kwa kila binadamu kuabudu bila vikwazo!

09/03/2017 16:53

Tunaishi wote duniani kwa kile kinachoitwa utandawazi wa dhana ya teknolojia ambayo kwa uangalifu wake inalenga juu ya mshikamano au mwelekeo mmoja na inataka kuondokana na tofauti zote za mila na desturi katika jitihada za umoja wa juu juu tu. Hivyo dini inayo wajibu wa kuweka wazi....

 

 

Patriaki Bartholomeo wa kwanza anawaalika waamini kuutukuza Msalaba kwa njia ya ushuhuda wenye mvuto na mashiko!

Patriaki Batolomeo wa kwanza anawaalika waamini wote kuutukuza Msalaba kwa njia ya ushuhuda wenye mvuto na mashiko kwa watu.

Tambueni dhambi na madhara yake; ukuu, huruma na upendo wa Mungu

04/03/2017 14:22

Patriaki Bartholomeo wa kwanza wa Kanisa la Kiorthodox la Costantinopoli anawataka waamini kufunga, kusali, kutafakari na kumwilisha huruma na upendo wa Mungu katika ushuhuda wenye mvuto na mashiko kwa njia ya huduma makini! Waamini wautukuze Msalaba wa Kristo Yesu kwa njia ya ushuhuda!