Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Ufilippini

Kard.Tagle:Tuwe chombo cha utetezi wa maisha,tumezaliwa na tutakufa bila uwezo!

11/01/2018 14:36

Maisha hayategemei kuwa tu na vitu na uwezo,kwani tumezaliwa bila kuwa na uwezo na wala kitu,hata tutakapokufa hatutachukua jambo lolote.Na kwa njia hiyo tujaribu kutafuta kuwa chombo cha utatezi wa maisha kwa ajili ya wengine.Ni maelezo ya Kardinali Luis A.Tagle Askofu Mkuu wa Jimbo la Manila 

 

Padre Teresito Chito Soganub Katibu wa Askofu Marawi Ufillippini ameachiwa huru baada ya kutekwa nyara kwa miezi kadhaa

Padre Teresito Chito Soganub Katibu wa Askofu Marawi Ufillippini ameachiwa huru baada ya kutekwa nyara kwa miezi kadhaa na magaidi

Ufilippini:Padre Chito ameachiwa huru baada ya kutekwa nyara na magaidi

19/09/2017 13:57

Padre Chito alitekwa nyara pamoja na kundi la waamini tarehe 23 Mei 2017 huko Marawi Kusini mwa Ufilippini. Pade Chito amewekwa huru kwa njia ya operesheni kali ya wanajeshi karibu na Msikiti wa Bato moja ya ngome kubwa ya kikundi cha magaidi cha Maute wanao husika na utekaji nyara

 

Askofu mkuu Giuseppe Pinto ameteuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Croatia.

Askofu mkuu Giuseppe Pinto ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Croatia.

Askofu mkuu Giuseppe Pinto ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican Croatia!

01/07/2017 18:36

Askofu mkuu Giuseppe Pinto aliyezaliwa kunako mwaka 1952 huko Noci, Italia, akapadrishwa mwaka 1978 na kuteuliwa kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu mwaka 2002 ameteuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Croatia. Kabla ya hapo alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Ufilippini.

 

Waamini na watu wote wenye mapenzi mema mema wanapaswa kubomoa kuta za utengano kwa njia ya toba na msamaha wa kweli!

Waamini na watu wote wenye mapenzi mema wanaweza kubomoa kuta za utengano kwa njia ya toba na msamaha wa dhambi zao.

Msamaha na upatanisho wa kweli uvunje kuta za utengano kati ya watu!

08/06/2017 12:12

Waamini wanapaswa kumwomba Roho Mtakatifu ili aweze kuwakirimia ujasiri na kipaji cha nguvu ili kuvunjilia mbali kuta za utengano zinazoendelea kujengwa miongoni wa watu wa mataifa kutokana na vita, kinzani na mipasuko ya kidini, kisiasa, kikabila na kijamii, inayojenga hofu na mashaka!