Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Uekumene wa kiroho

Patriaki Bartolomeo wa kwanza anawapongeza viongozi wa Makanisa walioanzisha mchakato wa uekumene miaka 50 iliyopita!

Patriaki Bartolomeo wa kwanza anawapongeza viongozi wa Makanisa walioanzisha mchakato wa majadiliano ya kiekumene miaka 50 iliyopita.

Miaka 50 ya mchakato wa majadiliano ya kiekumene ndani ya Kanisa!

26/07/2017 14:39

Mwenyeheri Paulo VI anasema, mwanga wa upendo wa Wakristo na udugu walionao wao kwa wao, unawasaidia kutambua umuhimu wa imani yao kwa Kristo na Kanisa lake. Patriaki Athenagora anahimiza viongozi kujitahidi kuunganisha kile ambacho kimetenganishwa kwa kukazia imani na uongozi.

Damu ya mashuhuda wa imani ni mbegu ya Ukristo sehemu mbali mbali za dunia

Damu ya mashuhuda wa imani ni mbegu ya Ukristo sehemu mbali mbali za dunia.

Mitume Petro na Paulo ni mashuhuda wa imani walioyamimina maisha yao!

29/06/2017 15:27

Mababa wa Kanisa wanasema, damu ya mashuhuda wa imani ni mbegu ya Ukristo sehemu mbali mbali za dunia. Hii ndiyo dhamana iliyotekelezwa na Watakatifu Petro na Paulo, miambana na mihimili ya imani, walioyamimina maisha yao kwa ajili ya Kristo na Kanisa lake wakawa mbegu ya Ukristo!

Karama zote za Roho Mtakatifu ni kwa ajili ya umoja na huduma kwa familia ya Mungu!

Karama zote za Roho Mtakatifu ni kwa ajili ya umoja wa Kanisa na huduma kwa familia ya Mungu.

Yote ni kwa ajili ya umoja na huduma katika Roho Mtakatifu

07/06/2017 09:10

Maadhimisho ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican yaliliwezesha Kanisa kushuhudia kwa namna ya pekee uwepo wa Roho Mtakatifu miongoni mwa watoto wake! Huu ukawa ni mwanzo wa kuibuka kwa vyama mbali mbali vya kitume ili kushuhudia imani inayomwilishwa katika: Neno na Huduma makini!

Chama cha Uhamsho wa Kikatoliki Duniani kinaadhimisha Jubilei ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwake!

Chama cha Uhamsho wa Kikatoliki, Wakarisimatiki Wakatoliki, kinaadhimisha Jubilei ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwake. Baba Mtakatifu Francisko anawapongeza kwa kuendelea kuwa ni "majembe ya nguvu" katika mchakato wa majadiliano ya kiekumene.

Chama cha Uhamsho wa Kikatoliki ni jembe la uekumene duniani!

02/06/2017 16:18

Jubilei ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Uhamsho wa Kikatoliki Duniani ni muda wa sala, tafakari, makongamano, toba na wongofu wa ndani, tayari kuandika ukurasa mpya wa majadiliano ya kiekumene yanayofumbatwa katika huduma, damu, maisha ya kiroho na sala!

Kardinali Leonardo Sandri katika hija yake ya kikazi nchini Australia anakazia uekumene wa huduma na maisha ya kiroho; majadiliano ya kidini na amani!

Kardinali Leonardo Sandri katika hija yake ya kitume nchini Australia anaendelea kukazia umuhimu wa uekumene wa huduma na maisha ya kiroho sanjari na majadiliano ya kidini ili kudumisha misingi ya haki , amani na maridhiano kati ya watu!

Hija ya mshikamano wa upendo na waamini wa Makanisa ya Mashariki

09/05/2017 14:39

Hija ya Kardinali Leonardo Sandri, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki nchini Australia inapania kuimarisha umoja, upendo na mshikamano na Wakristo wa madhehebu mbali mbali nchini Australia sanjari na kukoleza mchakato wa majadiliano ya kidini na Waislam!

Papa Francisko wakati akirejea kutoka Misri, tarehe 29 Aprili 2017 amepata nafasi ya kuchinga na waandishi wa habari kuhusu masuala ya kimataifa!

Papa Francisko alipokuwa anarejea mjini Vatican baada ya kuhitimisha hija yake ya kitume nchni Misri tarehe 29 Aprili 2017 alipata nafasi ya kuchinga na waandishi wa habari kuhusiana na masuala ya kitaifa na kimataifa.

Papa Francisko achonga na waandishi wa habari wakati akirejea Vatican

01/05/2017 12:29

Baba Mtakatifu Francisko wakati akirejea mjini Vatican baada ya kuhitimisha hija ya kitume ambayo imeacha "gumzo kubwa" nchini Misri amepata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu: majadiliano, diplomasia, amani, wahamiaji, majadiliano ya kidini na kiekumene; na umuhimu wa ushuhuda!

Baba Mtakatifu Francisko na Papa Tawadros II wametia sahihi kwenye Tamko la pamoja kuhusu mchakato wa uekumene kati ya Makanisa haya mawili.

Baba Mtakatifu Francisko na Papa Tawadros II wametia sahii katika tamko la pamoja kuhusu mchakato wa majadiliano ya kiekumene katika sala na maisha ya kiroho; katika damu na huduma makini kwa watu wa Mungu.

Tamko la Pamoja kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Papa Tawadros II

30/04/2017 12:10

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa hija yake ya kitume nchini Misri ametia sahihi tamko la pamoja na Papa Tawadros II wa Kanisa la Kikoptik la Misri juu ya umuhimu wa kuendeleza majadiliano ya kiekumene yanayojikita katika sala na maisha ya kiroho; katika damu na huduma makini kwa watu wa Mungu!

Uekumene wa damu uwafungamanishe Wakristo kushuhudia imani yao, kutetea haki, amani na maridhiano kati ya watu!

Uekumene wa damu uwafungamanishe wakristo kusimama kidete kushuhudia imani yao, kutetea haki msingi za binadanu na kudumisha amani duniani.

Uekumene wa damu udumishe umoja na mshikamano wa Wakristo duniani!

29/04/2017 15:33

Wakristo wanaunganishwa kwa namna ya pekee katika imani moja inayobubujika kutoka katika Sakramenti ya Ubatizo! Uekumene wa damu uwajenge na kuwaimarisha Wakristo katika kumshuhudia Kristo na Kanisa lake sanjari na kusimama kidete kulinda haki msingi za binadamu na amani duniani!