Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Tume huru ya uchaguzi na Mipaka ya Kenya, IEBC

Maaskofu Katoliki Kenya: Kwaresima ni fursa ya kujikita katika ukweli na haki kwa wote; kwa kukuza majadiliano na upatanisho wa kitaifa.

Maaskofu Katoliki Kenya: Kwaresima ni wakati muafaka wa kujikita katika ukweli na haki kwa wote ni muda muafaka wa kukuza na kudumisha majadiliano na upatanisho wa kitaifa!

Kenya: Huu ni wakati wa ukweli, haki, majadiliano na upatanisho!

17/02/2018 08:10

Baraza la Maaskofu Katoliki Nchini Kenya linaialika familia ya Mungu nchini humo kujenga na kudumisha mchakato wa majadiliano katika ukweli na uwazi ili haki iweze kupatikana kwa wote! Changamoto na kinzani zilizojitokeza nchini Kenya zipatiwe ufumbuzi kwa njia ya majadiliano, amani na utulivu!

Maaskofu Katoliki Kenya wasema, hotuba za chuki na uchochezi hazina mashiko wala mvuto kwa ustawi, maendeleo na mafao ya wananchi wa Kenya!

Maaskofu Katoliki Kenya wasema, hotuba za chuki, uhasama na uchochezi hazina mvuto wa la mashiko kwa ustawi, maendeleo na mafao ya wananchi wa Kenya!

Maaskofu Katoliki Kenya: Dumisheni majadiliano! Vurugu hazina tija!

29/09/2017 13:50

Familia ya Mungu nchini Kenya inataka kuona nchini inayosimamia: ukweli, inayotetea haki na kukemea maovu bila ya kumung'unya mung'unya maneno! Kipindi cha mpito kuelekea uchaguzi wa marudio hapo tarehe 26 Oktoba 2017 ni wakati wa kushikamana katika na kujenga umoja wa kitaifa!

Sakata la uchaguzi mkuu nchini Kenya limechukua sura mpya baada ya Tume Huru ya Uchaguzi mkuu pamoja na baadhi ya viongozi wa upinzani kuchunguzwa.

Sakata la uchaguzi mkuu nchini Kenya limeanza kuchukua sura mpya baada ya IEBC kuanza na viongozi wawili wa upinzani kuanza kuchunguzwa na Jeshi la Polisi na Tume ya Kupambana na rushwa.

Uchaguzi mkuu nchini Kenya kwa Mwaka 2017 wachukua sura mpya tena!

25/09/2017 12:21

Mwendesha mashtaka mkuu wa Serikali ya Kenya Bwana Keriako Tobiko ameamuru Tume ya Kupambana na Rushwa pamoja na Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya Tume Huru ya Uchaguzi na Miapaka IEBC pamoja na maafisa wawili wa muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya.

 

Maaskofu Katoliki Kenya: Jengeni utamaduni wa kuheshimu utawala wa sheria!

Maaskofu Katoliki Kenya: Jengeni utamaduni wa kutekeleza kwa dhati na kwa hiyari utawala was sheria.

Familia ya Mungu nchini Kenya jengeni utamaduni wa utawala wa sheria

07/09/2017 16:33

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya linawaalika wadau mbali mbali nchini Kenya kuhakikisha kwamba, wanatekeleza uamuzi wa Mahakama kuu ili kufanikisha uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 17 Oktoba 2017! Wazingatie sheria, kanuni na taratibu ili uchaguzi mkuu uwe ni huru na wa haki.

Bwana Raila Odinga apinga tarehe mpya ya uchaguzi wa marudio nchini Kenya kwa kutaka maofisa wa tume ya uchaguzi kufukuzwa kazi na kushitakiwa!

Bwana Raila Odinga apinga tarehe mpya ya uchaguzi nchini Kenya, yaani tarehe 17 Oktoba 2017 kwa kuweka sharti kwamba, maafisa wa Tume ya Uchaguzi kufukuzwa kazi na hatimaye kushitakiwa.

Raila Odinga aweka pingamizi la uchaguzi mkuu tarehe 17 Oktoba 2017

05/09/2017 14:09

Tume huru ya uchaguzi na Mipaka nchini Kenya, IEBC imetangaza kwamba, uchaguzi mkuu wa Rais, utarudiwa tena tarehe 17 Oktoba 2017, tarehe ambayo imepingwa na Bwana Raila Odinga kutoka chama cha upinzani anayetaka maafisa wote wa Tume ya uchaguzi nchini Kenya kufukuzwa kazi na kushitakiwa.