Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Tarehe 23 Feb. 2018: Kufunga na Kusali

Vatican inaendelea kufuatilia kwa karibu sana hali ya kisiasa na kijamii nchini DRC!

Vatican inaendelea kufuatilia kwa karibu sana hali tete ya kisiasa na kijamii nchini DRC.

Papa Francisko anaendelea kufuatilia kwa karibu hali tete nchini DRC

14/04/2018 16:31

Baba Mtakatifu Francisko kwa nyakati mbali mbali ameonesha masikitiko makubwa pamoja na kuguswa na hali tete ya wananchi wa DRC wanaoendelea kuteseka kutokana na vita pamoja na mpasuko wa kisiasa na kijamii. Vatican inaiomba Jumuiya ya Kimataifa kusimamia mchakato wa uchaguzi DRC.

Wakristo kwa muda wa Siku 40 wamesafiri katika Jangwa la Maisha yao ya Kiroho, sasa ni wakati wa kudumisha ile neema ya utakaso waliojichotea!

Wakristo kwa muda wa Siku 40 wamesafiriki katika Jangwa la Maisha yao ya kiroho, sasa ni wakati wa kuendelea kuhifadhi ile neema ya utakaso waliojichotea wakati wa Kwaresima!

Dumisheni neema ya Kipindi cha Kwaresima ili kukuza utakatifu!

28/03/2018 09:38

Kwa muda wa siku 40 Wakristo wamefanya safari ya kiroho katika jangwa la maisha yao kwa kufunga na kusali; kwa toba na wongofu wa ndani; kwa kusoma, kutafakari na kumwilisha Neno la Mungu katika matendo ya huruma: kiroho na kimwili! Huu ni muda muafaka wa kuendeleza neema ya utakaso!

Caritas Internationalis inasema, hali ni tete sana nchini DRC, kunahitajika msaada wa dharura ili kuokoa maisha ya watu wanaoendelea kuteseka.

Caritas Internationalis insema, hali ni tete sana nchini DRC kuna watu wanauwawa kila siku na watoto wengi wanaishi katika mazingira hatarishi.

Caritas Internationalis: DRC. Hali ni tete sana!

01/03/2018 10:23

Shirikisho la Mashirika ya Misaada ya Kanisa Katoliki Kimataifa, Caritas Internationalis linasema kwa sasa hali ni tete sana nchini DRC kutokana na vita, ghasia, kinzani na mipasuko ya kijamii kiasi kwamba, kuna maelfu ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na watu wanaendelea kuuwawa!

Papa Francisko na Sekretarieti kuu ya Vatican wameitumia tarehe 23 Feb. 2018 kufunga na kusali kwa ajili ya kuombea amani duniani.

Papa Francisko pamoja na wajumbe wa Sekretarieti kuu ya Vatican baada ya kuhitimisha mafungo yao kama sehemu ya maandalizi ya adhimisho la Fumbo la Pasaka, wameendelea pia kusali na kufunga kwa ajili ya kuombea amani duniani.

Mwendelezo wa sala na kufunga kwa ajili ya amani duniani!

24/02/2018 08:16

Baba Mtakatifu Francisko pamoja na wajumbe wa Sekretarieti kuu ya Vatican baada ya mafungo ya Kwaresima kama sehemu ya maandalizi ya adhimisho la Fumbo la Pasaka, tarehe 23 Februari 2018 wameungana na familia ya Mungu sehemu mbali mbali za dunia ili kuombea amani duniani!

Maaskofu Katoliki Sudan: Fungeni na kusali ili kuombea haki, amani, msamaha na upatanisho wa kitaifa!

Maaskofu Katoliki Sudan: Fungeni na kusali ili kuombea haki, amani na upatanisho wa kitaifa!

Baraza la Maaskofu Katoliki Sudan: Fungeni na kusali kuombea amani

21/02/2018 11:52

Baraza la Maaskofu Katoliki Sudan linawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kutumia kikamilifu Kipindi cha Kwaresima kwa kutubu na kuongoka; kusali na kufunga pamoja na kulitafakari Neno la Mungu linalomwilishwa katika matendo ya huruma; haki, amani na upatanisho wa kitaifa.

WCC: Linawataka Wakristo kushiriki kikamilifu katika Siku ya kusali na kufunga kwa ajlili ya kuombea amani nchini DRC na Sudan ya Kusini.

WCC: Linawaalika Wakristo sehemu mbali mbali za dunia kushirikiana kwa dhati ili kufunga na kusali kwa ajili ya kuombea haki, amani na maridhiano nchini DRC na Sudan ya Kusini.

WCC: Ushuhuda wa Injili ya Amani unafumbatwa katika sala na kufunga

18/02/2018 07:30

Baraza la Makanisa Ulimwenguni linawaalika Wakristo wote sehemu mbali mbali za dunia kufunga na kusali 23 Feb. 2018 kwa ajili ya kuombea: haki, amani na maridhiano huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo pamoja na Sudan ya Kusini. Hiki ni kielelezo cha ushuhuda wa Injili ya Amani Duniani.

Serikali ya Rais Joseph Kabila wa DRC inashutumiwa kwa kuvunja haki msingi za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria.

Serikali ya Rais Joseph Kabila wa DRC inashutumiwa kwa kuvunja haki msingi za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria.

DRC: Haki msingi za binadamu na utawala wa sheria viko mashakani!

14/02/2018 08:09

Serikali ya Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Watu wa Congo imeshindwa kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kati yake na vyama vya upinzani nchini humo kuhusu mustakabali wa nchi hiyo na matokea yake haki msingi za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria vinaendelea kuvunjwa kila kukicha!

Tazama na mimi ninajiandikisha kwa njia ya Intaneti kuudhuria Siku ya Vijana duniani huko Panama 2019

Tazama na mimi ninajiandikisha kwa njia ya Intaneti kuudhuria Siku ya Vijana duniani huko Panama 2019

Kuzindua kujiandikisha kwa njia ya Intaneti katika Siku ya Vijana duniani!

12/02/2018 16:07

Leo hii unazinduliwa mchakato wa kujiandikisha kwa Siku ya Vijana Duniani ambayo inatafanyika Panama mwezi Januari 2019.Hata mimi kwa uwepo wa vijana wawili,ninajiandikisha kwa njia ya Interneti.Papa anaongeza kusema,tazama nimejiandikisha sasa kama mhujaji wa Siku ya Vijana Duniani.