Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Tafakari ya Neno la Mungu Jumapili X ya Mwaka

Mwanadamu ana lazima ya kufuataq sheria maadili inayomsukuma kutenda jema na kuepuka ovu. Sheria hii inaongea ndani kabisa ya dhamiri ya mtu!

Mwanadamu ana lazima ya kufuata sheria ya maadili inayomsukuma kutenda jema na kuepuka ovu. Sheria hii yaongea ndani kabisa ya dhamiri ya mwanadamu!

Dhambi na matokeo ya ufunuo wa mpango wa ukombozi wa mwanadamu

09/06/2018 16:39

Mwenyezi Mungu ni mwingi wa huruma na mapendo, mambo yanayojionesha tangu pale Adamu na Eva walipoanguka dhambini na kujikuta wako watupu, kwa kupoteza: urafiki na Mwenyezi Mungu; Uhuru wa kweli; Wema na utakatifu wa maisha! Lakini Mungu anawaahidia ukombozi!

Yesu anaonesha kuwa ana nguvu ya kuvunjilia mbali utawala wa Ibilis, shetani na kwamba, ndugu zake ni wale wote wanaosikia na kutekeleza Neno lake!

Yesu anaonesha kuwa ana nguvu ya kuweza kuvunjilia mbali utawala wa Ibilisi, shetani na kwamba, ndugu na jamaa zake ni wale wote wanaosikia na kumwilisha Neno lake katika uhalisia wa maisha yao!

Dhamiri ni mahali patakatifu panapopaswa kuheshimiwa!

07/06/2018 14:59

Dhamiri ni hukumu ya akili ambamo mwanadamu hutambua sifa adilifu ya tendo halisi analoelekea kulitenda, angali akilifanya au amekwisha kulitekeleza. Mwanadamu anapaswa kufuata kile ambacho ni haki na sahihi na kwamba, mwanadamu anaweza kutambua sheria ya Mungu kwa njia ya dhamiri nyofu!

 

Maisha yote ya Kristo Yesu ni Fumbo linalomrejeshea mwanadamu wito wake wa asili, yaani ile sura na mfano wa Mungu.

Maisha yote ya Kristo Yesu ni fumbo linalomrejeshea tena mwanadamu ule wito wake wa asili, yaani sura na mfano wa Mungu

Maisha yote ya Kristo Yesu ni Fumbo kuu!

06/06/2018 15:09

Mama Kanisa anafundisha kwamba, maisha yote ya Kristo Yesu ni fumbo linalojumlisha yote. Yote Yesu aliyofanya, kutenda na kuteseka yalikuwa na lengo la kumrudisha mtu aliyeanguka katika wito wake wa awali; yaani kwa kuwa ni sura na mfano wa Mungu pamoja na kuwarejeshea tena ushirika na Mungu!