Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Tafakari Neno la Mungu Jumapili ya XIV ya Mwaka

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Fumbo la Umwilisho lilikuwa ni kashfa kubwa ya Yesu kukataliwa nyumbani kwao Nazareti.

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Fumbo la Umwilisho lilikuwa ni kashfa kubwa iliyomfanya Kristo Yesu kukataliwa nyumbani kwao!

Kashfa ya Fumbo la Umwilisho, sababu ya Yesu kukataliwa nyumbani kwao

09/07/2018 08:32

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Kashfa ya Msalaba ilikuwa ni sababu kuu ya wananchi wa Nazareti kuvutwa kumsikiliza, wakamshangaa, wakaona mashaka, wakashindwa kumwamini na hatimaye, wakamtakaa katu katu! Kwa hakika, Nabii hakosi heshima isipokuwa kwa watu wake mwenyewe!

Mwenyezi Mungu anatumia watu, mazingira na historia kufikisha ujumbe wa Habari Njema kwa waja wake!

Mwenyezi Mungu anatumia watu, mazingira na historia ili kuweza kufikisha ujumbe wa habari Njema kwa waja wake.

Tafakari ya Neno la Mungu: Ujumbe wa Mungu si rahisi sana kupokelewa!

07/07/2018 07:26

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili XIV ya Kipindi cha Mwaka B wa Kanisa inaonesha jinsi ambavyo ni vigumu sana kupokea Habari Njema ya Wokovu, lakini Mwenyezi Mungu anatumia watu, historia na matukio mbali mbali katika maisha ya mwanadamu ili kufikisha ujumbe wake kwa binadamu!

Kristo Yesu ni kielelezo cha hekima, nguvu na uweza wa Mungu wa kumwongoa mwanadamu kutoka katika lindi la dhambi na mauti!

Kristo Yesu ni kielelezo cha hekima, nguvu na uweza wa Mungu wa kumwongoa mwanadamu kutoka katika lindi la dhambi na mauti!

Tafakari ya Neno la Mungu: Hekima ya Mungu iwe dira na mwongozo wetu!

06/07/2018 07:07

Mungu Baba Mwenyezi amefunua uweza wake wote kwa namna ya ajabu sana kwa kujinyenyekesha kwa hiari na kwa Ufufuko wa Mwanawe, ambao kwa huo alishinda ubaya. Hivyo Kristo Msulubiwa ni nguvu na hekima ya Mungu. Kwa njia ya Fumbo la Pasaka, Mungu ameonesha nguvu na uweza wake!

Papa Francisko anawaalika watu wote kumwendea Kristo Yesu ili awafariji, awapumzishe na kusaidia kubeba mizigo na changamoto zao za maisha!

Papa Francisko anawaalika watu wote kumwendea Kristo Yesu, ili awafariji, awapumzishe na kusaidia kuibeba mizigo na changamoto za maisha!

Papa Francisko: Nendeni nyote kwa Yesu atawapumzisha na kuwafariji!

10/07/2017 09:13

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika watu wote kumwendea Yesu ili aweze kuwapumzisha na kuwafariji katika shida na mahangaiko yao; Yesu anataka kuwakirimia nguvu na uthabiti wa moyo ili kukabiliana vyema na changamoto za maisha; anataka kuwasaidia kubeba mizigo yao ili iwe ni miepesi zaidi!

Wanafunzi wa Yesu wanahamasishwa na Kristo mwenyewe kujifunza kutoka kwake, ili kweli waweze kuwa ni vyombo na mashuhuda wa Injili ya upendo na huruma

Wanafunzi wa Yesu wanahamasishwa kujifunza kutoka kwake, ili waweze kuwa kweli ni vyombo na mashuhuda wa Habari Njema ya Wokovu kati ya watu wa Mataifa.

Jifunzeni kwa makini kutoka kwa Yesu, ili muwe mashuhuda amini!

08/07/2017 17:03

Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili ya XIV ya Kipindi cha Mwaka A wa Kanisa ni mwaliko kwa waamini kumjifunza Kristo na kuchota fadhila na karama mbali mbali kutoka katika mafundisho, lakini zaidi ushuhuda wa maisha yake, ili wao pia waweze kuwa ni vyombo vya utangazaji na ushuhuda wa Injili!

Yesu anawaalika wafuasi wake ili kujitenga na malimwengu wapate nafasi ya kupumzika na kujifunza kutoka kwake.

Yesu anawaalika wafuasi wake kujitenga na malimwengu ili waweze kupata nafasi ya kupumzika na kujifunza kutoka kwake kwani yeye ni mpole na mnyofu wa moyo!

Jifunzeni kutoka kwa Kristo kuwa wanyenyekevu wa moyo!

06/07/2017 16:38

Liturujia ya Neno la Mungu linawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kwenda kwa Yesu ili waweze kujifunza kutoka kwake pamoja na kupata pumziko, tayari kutweka hadi kilindini katika kuendeleza mchakato wa uinjilishaji mpya unaojikita katika ushuhuda wenye mvuto na mashiko!

 

Fadhila za kimungu na kibinadamu ziwawezeshe waamini kutenda mema!

Fadhila za kimungu na kibinadamu ziwawezeshe waamini kutenda mema kwa ajili ya ujenzi wa ufalme wa Mungu.

Mwilisheni fadhila ya unyenyekevu katika huduma kwa watu wa Mungu!

06/07/2017 16:14

Fadhila ni tabia ya kawaida na imara ya kutenda mema na inamwezesha mtu kutoa kilicho chema kabisa kutoka katika undani wa nafsi yake. Mtu wa fadhila huelekea mema kwa hisi zake zote na nguvu za kiroho. Ni mtu anayejibidisha kutafuta mema na kuyachagua kwa matendo halisi!