Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Siku ya Kuombea Amani Duniani 2018

Wakristo kwa muda wa Siku 40 wamesafiri katika Jangwa la Maisha yao ya Kiroho, sasa ni wakati wa kudumisha ile neema ya utakaso waliojichotea!

Wakristo kwa muda wa Siku 40 wamesafiriki katika Jangwa la Maisha yao ya kiroho, sasa ni wakati wa kuendelea kuhifadhi ile neema ya utakaso waliojichotea wakati wa Kwaresima!

Dumisheni neema ya Kipindi cha Kwaresima ili kukuza utakatifu!

28/03/2018 09:38

Kwa muda wa siku 40 Wakristo wamefanya safari ya kiroho katika jangwa la maisha yao kwa kufunga na kusali; kwa toba na wongofu wa ndani; kwa kusoma, kutafakari na kumwilisha Neno la Mungu katika matendo ya huruma: kiroho na kimwili! Huu ni muda muafaka wa kuendeleza neema ya utakaso!

Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani linawaalika waamini kushiriki safari ya mateso na matumaini ya wakimbizi na wahamiaji duniani!

Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani linawaalika waamini na watu wenye mapenzi mema kushiriki katika mateso na matumaini ya wakimbizi na wahamiaji duniani.

Waamini onjeni mateso na matumaini ya wakimbizi na wahamiaji duniani!

11/01/2018 15:43

Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani, kuanzia tarehe 03 hadi 13 januari 2018 linaadhimisha Juma la Wakimbizi na Wahamiaji nchini humo kwa kuongozwa na mwaliko kwa waamini na watu wote wenye mapenzi mema kushiriki kikamilifu katika mateso na matumaini ya wakimbizi na wahamiaji duniani!

Ratiba elekezi ya Ibada za kufunga na kufungua mwaka inaonesha kuwa Papa Francisko atashiriki kikamilifu!

Ratiba elekezi ya Ibada za kufunga na kufungua Mwaka mpya 2018 inaonesha kwamba, Papa Francisko atashiriki kikamilifu.

Ibada za kufunga mwaka 2017 na kufungua Mwaka 2018 mjini Vatican

30/12/2017 08:33

Ibada ya Masifu ya kwanza ya jioni kama sehemu ya maadhimisho ya Sherehe ya Bikira Maria Mama wa Mungu, Jumapili tarehe 31 Desemba 2017 itapambwa kwa utenzi wa shukrani na Ibada ya Kuabudu Ekaristi Takatifu. Tarehe Mosi, Januari, 2018 Papa ataongoza Ibada ya Misa mjini Vatican.