Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Siku kuu ya Tokeo la Bwana

Kardinali Polycarp Pengo anawataka waamini lakini zaidi wakleri kutekeleza mapenzi ya Mungu katika maisha na utume wao.

Kardinali Polycarp Pengo anawataka waamini, lakini zaidi wakleri kutekeleza mapenzi ya Mungu katika maisha yao.

Kardinali Pengo: Jitahidini kutekeleza mapenzi ya Mungu katika maisha

11/01/2018 16:35

Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam anawataka waamini, lakini kwa namna ya pekee kabisa Wakleri kuhakikisha kwamba, wanajitahidi kutekeleza mapenzi ya Mungu katika maisha na utume wao, vinginevyo wanaweza kujikuta wakiogelea kwenye dimbwi la maafa!

 

Sherehe ya Tokeo la Bwana pia ni Noeli kwa Makanisa ya Mashariki na Siku ya Utoto Mtakatifu ili kuimarisha ari na moyo wa kimissionari.

Sherehe ya Tokeo la Bwana pia ni Noeli kwa Makanisa ya Mashariki, ni Siku ya Utoto Mtakatifu, maalum kwa ajili ya kuhamasisha ari, moyo na upendo wa kimissionari.

Sherehe ya Tokeo la Bwana: Watu walimtafuta, hawakumjali, wakamwogopa

06/01/2018 12:13

Baba Mtakatifu Francisko anasema Kristo Yesu alipojifunua kwa watu wa Mataifa kama Mwana wa Mungu, Masiha na Mwanga wa Mataifa; Mamajusi kutoka Mashariki ya mbali walithubutu kwenda kumtafuta, wakuu wa makuhani na waandishi wa watu hawakujali; Mfalme Herode na Yerusalemu wakaingiwa hofu!

Papa Francisko: Sherehe ya Tokeo la Bwana iwe ni fursa ya kutembea, kuinua macho juu angani na kumtolea Mungu hazina kwa njia ya matendo ya huruma.

Papa Francisko: Sherehe ya Tokeo la Bwana ni fursa kwa waamini kutembea, kuinua macho yao angani na kumtolea Mungu hazina ya maisha yao kwa njia ya matendo ya huruma.

Papa: Sherehe ya Tokeo la Bwana: Kuona nyota, kutembea na kutoa hazina

06/01/2018 12:00

Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake wakati wa maadhimisho ya Sherehe ya Tokeo la Bwana, maarufu kama Epifania, amewataka waamini kujitahidi kuina nyota ya Mtoto Yesu katika maisha yao, kuifuata kwa kuthubutu kutembea na kumtolea hazina inayofumbatwa katika matendo ya huruma.

Sherehe ya Tokeo la Bwana ni nafasi ya kutangaza maadhimisho ya Mafumbo ya Kanisa yanayopata chimbuko lake katika Fumbo la Pasaka!

Sherehe ya Tokeo la Bwana ni nafasi ya kutangaza maadhimisho ya Mafumbo ya Kanisa yanayopata chimbuko lake kutoka katika Fumbo la Pasaka.

Mbiu ya Mwaka wa Bwana 2018: Maadhimisho ya Mafumbo ya Kanisa

06/01/2018 12:00

Sherehe ya Tokeo la Bwana ni ufunuo wa Mtoto Yesu aliyezaliwa na Bikira Maria kuwa ni Mwana wa Mungu, Masiha na Mwanga wa Mataifa. Katika maadhimisho haya, Mama Kanisa anatangaza Mbiu ya Mwaka wa Bwana kwa kutaja tarehe za maadhimisho ya Mafumbo makuu ya Kanisa kwa Mwaka!

Shirika la Utoto Mtakatifu linaadhimisha kumbu kumbu ya miaka 175 tangu kuanzishwa kwake!

Shirika la Utoto Mtakatifu linaadhimisha miaka 175 tangu kuanzishwa kwake.

Siku ya Utoto Mtakatifu Duniani: Jengeeni watoto moyo wa kimissionari

06/01/2018 10:16

Mama Kanisa mwaka 2018 anaadhimisha Kumbu kumbu ya Miaka 175 tangu Shirika la Utoto Mtakatifu lilipoanzishwa kunako mwaka 1843 na Askofu Toussaint de Forbin wa Nancy, Ufaransa ili kukuza na kudumisha utamaduni wa sala, upendo, mshikamano na moyo wa kimissionari miongoni mwa watoto.

Sherehe ya Tokeo la Bwana, maarufu kama Epifania ni ufunuo wa Kristo Yesu: Mwanga wa Mataifa, Mfalme na Mkombozi wa ulimwengu.

Sherehe ya Tokeo la Bwana, maarufu kama Epifania ni ufunuo wa Kristo Yesu kama Mwanga wa Mataifa, Mfalme na Mkombozi wa Ulimwengu.

Kristo Yesu ni Mwanga wa Mataifa, Mfalme na Mkombozi wa Ulimwengu

05/01/2018 06:45

Maadhimisho ya Liturujia ya Sherehe ya Tokeo la Bwana ni ufunuo wa Kristo Yesu, Mwanga wa Mataifa, Mfalme na Mkombozi wa ulimwengu; dhamana na utume wake unaojionesha hasa kwenye hazina ambayo Mamajusi kutoka Mashariki ya mbali walimtolea Mtoto Yesu: Dhahabu, Uvumba na Manemane!

Sherehe ya Tokeo la Bwana ni Siku kuu ya Kristo Mwanga unaofunuliwa kwa watu wa Mataifa!

Sherehe ya Tokeo la Bwana ni Siku kuu ya Mwaga, ambao ni Kristo anayejifunua kwa watu wa Mataifa.

Sherehe ya Tokeo la Bwana ni Siku kuu ya ufunuo wa mwanga wa Kristo!

03/01/2018 14:24

Yesu Kristo ni Mwanga wa Mataifa unaofunuliwa kwa watu wa mataifa yote wanaowakilishwa na Mamajusi kutoka Mashariki ya mbali, ni watu wa mazingira na dini ya kipagani, lakini wanaifuata Nyota ya Daudi, Mfalme wa Mataifa, Mwana wa Mungu na Mkombozi wa Ulimwengu. Epifania ni sherehe ya umoja!

 

Sherehe ya Tokeo la Bwana: Zawadi: Ubani, dhahabu na manemane yaani: Umungu, Ufalme na Ubinadamu wa Kristo Yesu.

Sherehe ya Tokeo la Bwana: Zawadi: Ubani, Dhahabu na Manemane maana yake ni: Umungu, Ufalme na Ubinadamu wa Kristo Yesu, Mwanga wa Mataifa.

Sherehe ya Tokeo la Bwana! Kristo Yesu ni Mwanga wa Mataifa!

02/01/2018 13:49

Mamajusi kutoka Mashariki ya mbali huku wakiongozwa na nyota walifika mjini Bethlehemu, wakamsujudu Bwana na kumtolea zawadi kuu tatu zinazofafanua maana na utume wa Kristo Yesu: Ubani ni Umungu wa Kristo; Dhahabu: Ufalme wa Kristo na Manemane ni Ubinadamu wa Kristo utakaopambana na kifo!