Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Siku kuu ya Pentekoste

Waamini na watu wote wenye mapenzi mema mema wanapaswa kubomoa kuta za utengano kwa njia ya toba na msamaha wa kweli!

Waamini na watu wote wenye mapenzi mema wanaweza kubomoa kuta za utengano kwa njia ya toba na msamaha wa dhambi zao.

Msamaha na upatanisho wa kweli uvunje kuta za utengano kati ya watu!

08/06/2017 12:12

Waamini wanapaswa kumwomba Roho Mtakatifu ili aweze kuwakirimia ujasiri na kipaji cha nguvu ili kuvunjilia mbali kuta za utengano zinazoendelea kujengwa miongoni wa watu wa mataifa kutokana na vita, kinzani na mipasuko ya kidini, kisiasa, kikabila na kijamii, inayojenga hofu na mashaka!

Karama zote za Roho Mtakatifu ni kwa ajili ya umoja na huduma kwa familia ya Mungu!

Karama zote za Roho Mtakatifu ni kwa ajili ya umoja wa Kanisa na huduma kwa familia ya Mungu.

Yote ni kwa ajili ya umoja na huduma katika Roho Mtakatifu

07/06/2017 09:10

Maadhimisho ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican yaliliwezesha Kanisa kushuhudia kwa namna ya pekee uwepo wa Roho Mtakatifu miongoni mwa watoto wake! Huu ukawa ni mwanzo wa kuibuka kwa vyama mbali mbali vya kitume ili kushuhudia imani inayomwilishwa katika: Neno na Huduma makini!

Wakristo hawana budi kumwachia nafasi Roho Mtakatifu ili aweze kuwafunda, kuwatakasa, kuwaongoza na kuwakumbusha mambo msingi katika utume wa Kanisa.

Wakristo hawana budi kumwachia Roho Mtakatifu nafasi ya kuwakumbusha, kuwaongoza, kuwafunda na kuwafundisha mammbo msingi katika maisha na utume wa Kanisa.

Majadiliano ya kiekumene yanapaswa kujikita katika ushuhuda wa pamoja!

05/06/2017 07:53

Roho Mtakatifu ni mhusika mkuu katika kuwafunda na kuwaunda Wakristo, changamoto na mwaliko kwa Wakristo kumwachia nafasi Roho Mtakatifu ili aweze kuwafundisha, kuwakumbusha, kuwatakasa na kuwaongoza katika mambo msingi ya maisha na utume wa Kanisa, kielelezo cha ushuhuda makini.

Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 3 Juni 2017 ameongoza mkesha wa kiekumene mjini Roma

baba Mtakatifu Francisko, tarehe 3 Juni 2017 ameongoza mkesha wa kiekumene duniani.

Mkesha wa kiekumene, ushuhuda wa nguvu ya Roho Mtakatifu Kanisani!

04/06/2017 15:09

Baba Mtakatifu Francisko kwa kuungana na viongozi wakuu wa Chama cha Udugu wa Kikatoliki Duniani, Huduma ya Uamsho wa Kikatoliki pamoja na viongozi mbali mbali wa Makanisa na Madhehebu ya Kikristo, wameongoza bahari ya Wakristo kutangaza na kushuhudia kwamba, Kristo ni Bwana!

Roho Mtakatifu ni zawadi ya Kristo Mfufuka inayopyaisha maisha na utume wa Kanisa!

Roho Mtakatifu ni zawadi ya Kristo Mfufuka inayopyaisha maisha na utume wa Kanisa kwa kufumbata umoja katika utofauti wake.

Roho Mtakatifu ni kiungo cha umoja wa Wakristo katika utofauti wao!

04/06/2017 14:05

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Roho Mtakatifu ni Muumbaji kwani anapyaisha maisha na utume wa Kanisa; anawajalia Mitume uwezo wa kuunganishwa katika mawasiliano ili kutangaza na kushuhudia imani yao kwa Kristo Yesu, aliyeteswa, akafa na kufufuka kwa wafu!

Papa Francisko anawapongeza viongozi wa Makanisa kwa kujenga na kudumisha majadiliano ya kiekumene katika sala na huduma!

Papa Francisko anawapongeza na kuwashukuru viongozi wa Makanisa na madhehebu ya Kikristo kwa kujenga na kudumisha majadiliano ya kiekumene katika sala, huduma, maisha ya kiroho na ushuhuda wa damu!

Roho Mtakatifu awasaidie Wakristo kujenga na kudumisha umoja!

03/06/2017 17:36

Baba Mtakatifu Francisko anawapongeza na kuwashukuru viongozi mbali mbali wa Makanisa na Madhehebu ya Kikristo wanaohudhuria kilele cha maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Uhamsho wa Kikristo Duniani, chombo imara katika majadiliamo ya kiekumene!

 

Roho Mtakatifu anawajalia waamini kuwa ni mashuhuda na vyombo vya uinjilishaji hadi miisho ya dunia.

Roho Mtakatifu anawajalia waamini kuwa ni mashuhuda na vyombo vya Uinjilishaji hadi miisho ya dunia. Roho Mtakatifu ndiye mhimili mkuu wa maisha na utume wa Kanisa.

Roho Mtakatifu ndiye nguzo msingi ya Uinjilishaji kwa nyakati zote!

01/06/2017 15:10

Baba Mtakatifu Francisko anasema, furaha ya Injili huijaza mioyo na maisha ya wote wanaokutana na Yesu. Wale walioikubali zawadi yake ya ukombozi wanawekwa huru kuondokana na dhambi, uchungu, utupu wa ndani na upweke! Roho Mtakatifu anawawezesha waamini kuwa mashuhuda wa imani!

 

Pentekoste ni siku ya kuzaliwa kwa Kanisa, siku ambayo mitume walitoka kimasomaso kutangaza na kushuhudia kuhusu: mateso, kifo na ufufuko wa Yesu.

Pentekoste ni siku ya kuzaliwa kwa Kanisa, siku ambayo Mitume walishukiwa na Roho Mtakatifu, wakatoka kimasomaso kutangaza na kushuhudia kwamba, Kristo Yesu aliyeteswa, akafa amefufuka kwa wafu! Hiki ni kiini cha imani na matumaini ya Kanisa.

Siku kuu ya Pentekoste, Siku ya kuzaliwa kwa Kanisa!

01/06/2017 14:40

Pentekoste ni Siku ambayo Kanisa linaadhimishwa kuzaliwa kwake kwa njia ya Roho Mtakatifu kuwashukia Mitume na hivyo kuwapatia nguvu, ujasiri, ari na moyo mkuu wa kuweza kutoka kifua mbele kutangaza na kushuhudia kwamba, Yesu aliyeteswa, akafa, akafufuka amepaa mbinguni! Kiini cha imani yetu!