Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Shirika la Wamisionari wa Damu Azizi ya Yesu

Tasaufi ya Damu Azizi ya Kristo Yesu ni dira na mwongozo wa maisha ya Mkristo!

Tasaufi ya Damu Azizi ya Kristo Yesu ni dira na mwongozo wa maisha ya Mkristo!

Tasaufi ya Damu Azizi ya Kristo na maisha ya Mkristo!

21/07/2018 08:01

Tasaufi ya Damu Azizi ya Kristo Yesu ni dira na mwongozo wa maisha ya Kikristo yanayojikita katika uhusiano na mafungamano kati ya Mwenyezi Mungu na jirani. Tasaufi hii inajengwa katika misingi ya Neno la Mungu, Mapokeo ya Kanisa, Ushuhuda na Mafundisho ya Watakatifu, Liturujia na Sakramenti.

Papa Francisko asema, mtindo wa maisha ya kimisionari una kiini chake ambacho ni Kristo Yesu na sura yake ambayo ni ushuhuda wa unyenyekevu.

Papa Francisko asema, mtindo wa maisha ya kimisionari una kiini chake ambacho ni Kristo Yesu na unafumbatwa katika ushuhuda wenye mvuto na mashiko katika hali ya unyenyekevu.

Papa Francisko: Mtindo wa maisha ya kimisionari una kiini na sura yake

16/07/2018 09:43

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili ya XV ya Kipindi cha Mwaka wa Kanisa amesema, mtindo wa maisha ya kimisionari una kiini chake ambacho ni Kristo Yesu aliyeteswa, akafa na kufufuka kwa wafu na sura yake ni unyenyekevu unaofumbatwa katika ushuhuda!

Damu Azizi ya Kristo Yesu ni mto wa rehema: shule ya huruma, msamaha, upatanisho, upendo na utakatifu wa maisha!

Damu Azizi ya Kristo Yesu ni mto wa rehema, shule ya huruma, msamaha, upatanisho, upendo na utakatifu wa maisha!

Tasaufi ya Damu Azizi ya Yesu ni shule ya huruma, msamaha na upendo!

02/07/2018 07:21

Tasaufi ya Damu Azizi ya Yesu ni shule ya huruma ya Mungu kwa binadamu; msamaha ulioletwa na Kristo Yesu kwa kumwaga damu yake Azizi Msalabani na hivyo ikawa ni sadaka ya upatanisho kati ya Mungu na binadamu! Damu Azizi ya Kristo ni mto wa rehema na upendo wa Mungu kwa binadamu!

Familia ya Damu Azizi ya Yesu inakutana na Papa Francisko, tarehe 30 Juni 2018 tayari kwa maadhimisho ya Mwezi wa Ibada kwa Damu Azizi ya Yesu!

Familia ya Damu Azizi ya Yesu inakutana na Papa Francisko tarehe 30 Juni 2018 tayari kwa maandalizi ya Mwezi Julai, uliotengwa na Mama Kanisa kwa ajili ya Ibada kwa Damu Azizi ya Yesu.

Familia ya Damu Azizi ya Yesu inakutana na Papa Francisko Vatican!

29/06/2018 07:47

Tasaufi ya Damu Azizi ya Kristo Yesu ni chemchemi ya huruma na upendo wa Mungu kwa mwanadamu! Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 30 Juni 2018 anakutana na familia ya Damu Takatifu ya Yesu inayoundwa na Mashirika mbali mbali! Tukio hili linatanguliwa na katekesi na baadaye mkesha!

Papa Francisko anayashukuru Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume yanayoendelea kutoa huduma ya tafiti, tiba na kinga kwa wagonjwa duniani.

Papa Francisko anayashukuru Mashirika ya Kitawa na Kazi za kitume kwa huduma ya utafiti, tiba na kinga kwa wagonjwa sehemu mbali mbali za dunia.

Hospitali ya Mtakatifu Gaspar, Itigi, chombo cha huduma kwa wagonjwa

10/02/2018 09:11

Baba Mtakatifu Francisko anayapongeza Mashirika ya Kitawa na Kazi za kitume kwa kuendeleza huduma na utume wa uponyaji uliotekelezwa na Kristo Yesu katika maisha yake. Anayataka Mashirika haya kuendelea kupyaisha huduma hii, kwa kuzingatia haki msingi za binadamu, utu na heshima ya wagonjwa!

Parokia ya Kupaa Bwana Mbinguni, Manyoni, Jimbo Katoliki Singida inaadhimisha Jubilei ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.

Parokia ya Kupaa Bwana Mbinguni, Manyoni, Jimbo Katoliki Singida inaadhimisha Jubilei ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.

Jubilei ya Miaka 50 ya Parokia ya Manyoni, Jimbo Katoliki Singida

17/10/2017 10:33

Jubilei ya Miaka 50 Parokia ya Kupaa Bwana Mbinguni, Manyoni, Jimbo Katoliki Singida inaongozwa na kauli mbiu "Jubilei Manyoni, Imani na Matendo". Huu ni muda wa kupyaisha na kuimarisha imani katika matendo; Jumuiya ndogo ndogo za Kikristo; kanuni maadili na utu wema; miundo mbinu na uongozi.