Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Sherehe ya Yesu Kristo Mfalme wa Ulimwengu

Siku kuu ya Yesu Kristo Mfalme wa Ulimwengu imefunga pia Siku ya Kwanza ya Maskini Duniani kwa mwaka 2017

Siku kuu ya Yesu Kristo Mfalme wa Ulimwengu imefungsa pia Siku ya kwanza ya Maskini Duniani kwa Mwaka 2017.

Yesu Kristo ni Mfalme wa: Kweli, Uzima, Utakatifu, Neema, Haki & Amani

26/11/2017 15:29

Ufalme wa Kristo Yesu ni ufalme kweli na uzima; Ufalme wa utakatifu na wa neema; Ufalme wa haki,  mapendo na amani!! Haya ni mambo msingi yanayopaswa kuvaliwa njuga na waamini kama sehemu ya mchakato wa ujenzi wa Ufalme wa Mungu hapa duniani! Kila mwamini anawajibika haswa!

 

Kipindi cha Majilio, Kanisa linakumbuka, Neno wa Mungu alipofanyika mwili na Siku ya atakapokuja kuwahukumu wazima na wafu!

Kipindi cha Majilio, Kanisa linakumbuka, Neno wa Mungu alipofanyika mwili na kukaa kati ya watu wake na Siku ya Mwisho, atakapokuja kuwahukumu wazima na wafu na wala ufalme wake hautakuwa na mwisho!

Ni kipindi cha Majilio: Fumbo la Umwilisho na Hukumu ya Mwisho!

26/11/2017 11:32

Kipindi cha Majilio ni fursa nyingine kwa waamini kukumbuka huruma na upendo wa Mungu kwa binadamu uliomsukuma hata akamtuma Mwanaye wa Pekee, ili aje kuwakomboa wanadamu kutoka katika lindi la dhambi na mauti! Atakuja tena kuwahukumu wazima na wafu na ufalme wake hauna mwisho!

 

Yesu ni Kristo Mfalme, anakuja kwetu na Ufalme wake hauna mwisho

Yesu ni Kristo Mfalme, anakuja kwetu na Ufalme wake hauna mwisho

Ukarimu wetu kwa wenzetu ni kibali cha kushiriki karamu ya Ufalme wa Kristo!

25/11/2017 14:19

Leo ni Dominika ya 34 ya Mwaka A wa Kanisa, Dominika ya mwisho katika Mwaka wa Kanisa ambapo tunapata fursa ya kumshangilia Bwana wetu Yesu Kristo Mfalme.Liturujia ya Mwaka wa Kanisa imefumbatwa na utimilifu wa fumbo la Kristo ambaye ni tumilifu wa Ukombozi wetu wanadamu.

 

 

Siku ya Maskini Duniani Kwa Mwaka 2017: " Kauli mbiu: Tusipende kwa neno bali kwa tende"

Siku ya Maskini Duniani Kwa Mwaka 2017: Kauli mbiu " Tusipende kwa neno bali kwa tendo".

Ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya Kwanza ya Maskini Duniani 2017

13/06/2017 15:34

Siku ya kwanza ya Maskini Duniani iliyoanzishwa na Baba Mtakatifu Francisko kama sehemu ya mwendelezo wa maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu itaadhimishwa hapo tarehe 19 Novemba 2017. Kauli mbiu "Tusipende kwa neno bali kwa tendo".

Mwaka wa huruma ya Mungu umewawezesha watu wengi kuguswa na huruma na upendo wa Mungu kutoka kwa Kristo  na Kanisa lake!

Mwana wa huruma ya Mungu umewawezesha watu wengi kuguswa na huruma na upendo wa Mungu unaobubujika kutoka kwa Kristo Yesu na Kanisa lake anasema Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi wa Jimbo kuu la Mwanza, Tanzania.

Matunda ya Maadhimisho ya Mwaka wa huruma, Jimbo kuu la Mwanza!

20/04/2017 11:00

Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi wa Jimbo kuu la Mwanza, Tanzania anasema, baada ya familia ya Mungu Jimbo kuu la Mwanza kukitumia vyema kipindi cha maadhimisho pamoja na nyongeza yake, Jumapili ya huruma ya Mungu, tarehe 23 Aprili 2017 wanaufunga rasmi mwaka wa huruma, lakini...!

Waraka wa Kitume: "Misericordia et misera": Mamlaka ya Mapadre wote kuondoa dhambi ya utoaji mimba; Siku ya Maskini Duniani!

Waraka wa Kitume: "Misericordia et misera": Papa Francisko anatoa mamlaka ya kuwaondolea watu dhambi ya utoaji mimba kwa mapadre wote. Anaanzisha pia Siku ya Maskini Duniani.

Jubilei ya Mwaka Mtakatifu wa huruma ya Mungu!

22/11/2016 08:33

Mwaka wa huruma ya Mungu umewawezesha waamini kutoa kipaumbele cha kwanza katika sala, tafakari na maisha yao kwa huruma ya Mungu kiini cha imani na utambulisho wa Kanisa. Mapadre wote wamepewa uwezo wa kuondolea dhambi ya utoaji mimba! Kanisa kuadhimisha Siku ya Maskini Duniani.

Lango kuu la huruma ya Mungu, yaani Moyo Mtakatifu wa Yesu, litaendelea kuwa wazi daima, ili kuchota, huruma, upendo na msamaha!

Lango kuu la huruma ya Mungu, yaani Moyo Mtakatifu wa Yesu, litaendelea kuwa wazi, ili waamini waendelee kuchota huruma, upatanisho na msamaha wa Mungu.

Msifunge kamwe malango ya huruma, upatanisho na msamaha!

20/11/2016 09:18

Baba Mtakatifu Francisko anawataka waamini kamwe kutofunga malango ya huruma, upatanisho na msamaha kwa kuwapatia jirani zao nafasi ya matumaini kwani Moyo Mtakatifu wa Yesu ni lango kuu la huruma na upendo wa Mungu kwa waja wake, lang ambalo liko wazi tangu kutobolewa kwa mkuki ubavuni!

Yesu Kristo ni Mfalme wa ulimwengu na ufalme wake ni wa milele unaofumbata: ukweli, uzima, utakatifu, neema, haki, mapendo na amani.

Yesu Kristo ni Mfalme wa ulimwengu na ufalme wake ni wa milele unaombata ukweli na uzima, utakatifu na neema; haki, amani na mapendo.

Mtazameni Mfalme wenu anavyoning'inia Msalabani!

18/11/2016 15:52

Leo Mama Kanisa anaadhimisha kilele cha Mwaka wa Kanisa Kiliturujia kwa Sherehe ya Yesu Kristo Mfalme wa Ulimwengu. Huyu ni Mfalme ambaye sherehe yake ya kuapishwa inafanyika Msalabani, Kiti chake cha kifalme ni Msalaba; mashuhuda wake ni wale majambazi wawili! Sipati picha!