Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

SECAM

Askofu mkuu Protase Rugambwa: AMECEA msikubali kutumbukia katika ukabila na udini usiokuwa na mvuto wa mashiko kwa maendeleo ya watu wa Mungu.

Askofu mkuu Protase Rugambwa: Amewataka Mababa wa AMECEA kutokubali kutumbukizwa katika sera za ukabila na udini usiokuwa na mvuto wala mashiko kwa ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu Barani Afrika.

AMECEA: Msikubali ukabila na udini viwapekenyue na kusababisha maafa

17/07/2018 14:00

Askofu mkuu Protase Rugambwa, amewataka Mababa wa AMECEA kujenga na kudumisha umoja, udugu na mshikamano kama dira na mwongozo wa watu wa Mungu Barani Afrika. Usawa na utofauti kati ya watu ni sehemu ya mpango wa Mungu, ili kutajirishana na kushirikishana: karama, fadhila na wema!

AMECEA inaadhimisha Mkutano mkuu wa 19 huko Addis Ababa, Ethiopia kuanzia tarehe 13-23 Julai 2018.

AMECEA inaadhimisha Mkutano mkuu wa 19 huko Addis Ababa nchini Ethiopia kwa kukazia hadhi sawa, umoja na amani ndani ya Mwenyezi Mungu kwenye Kanda ya AMECEA.

Mkutano Mkuu wa 19 wa AMECEA kutimua vumbi Addis Ababa, Ethiopia

11/07/2018 08:23

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati, AMECEA kuanzia tarehe 13-23 Julai 2018 linafanya mkutano wake mkuu wa 19 huko Addis Ababa nchini Ethiopia kwa kuongozwa na kauli mbiu "tofauti mtetemo, hadhi sawa, umoja wa amani ndani ya Mungu kwenye Kanda ya AMECEA.

Papa Francisko amekutana na kuzungumza na Baraza la Maaskofu Katoliki Uganda wakati wa hija yao ya kitume mjini Vatican, 2018.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na Baraza la Maaskofu Katoliki Uganda wakati wa hija yao ya kitume mjini Vatican kwa mwaka 2018.

Baraza la Maaskofu Katoliki Uganda: maisha, utume na changamoto zake

19/06/2018 07:14

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu, tarehe 18 Juni 2018 alikutana na kuzungumza na Baraza la Maaskofu Katoliki Uganda ambalo kwa sasa liko mjini Vatican kama sehemu ya utekelezaji wa hija ya kitume inayofanyika walau mara moja kila baada ya miaka mitano! Ni nafasi ya kusali na kutafakari.

Utandawazi usiokuwa na mashiko ni kichaka cha uchu wa mali na madaraka; biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo!

Utandawazi usiokuwa na mvuto wala mashiko ni kichaka cha uchu wa mali na madaraka, biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo, mambo yanayodhalilisha utu na heshima ya binadamu!

Utandawazi wa mshikamano katika maisha na utume wa Kanisa!

25/04/2018 07:16

Utandawazi ni mchakato unaogusa maisha ya mtu mzima: kiroho na kimwili; unagusa na kutikisa maisha ya mtu binafsi, familia na jamii katika ujumla wake. Utandawazi una tabia ya kujielekeza zaidi katika maisha ya kitamaduni, kiuchumji, kisiasa na hata kidini. Utandawazi wa mshikamano unahitajika!

SECAM na CCEE yanajadili kuhusu changamoto za utandawazi, utu, heshima ya binadamu na ekolojia.

SECAM na CCEE yanajadili kuhusu athari za utandawazi, utu na heshima ya binadamu pamoja na ekolojia.

SECAM na CCEE yanajadiliana kuhusu changamoto za utandawazi!

12/04/2018 06:58

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM pamoja na Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Ulaya, CCEE yanadiliana kwa kina na mapana kuhusu changamoto za utandawazi, wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji, utu na heshima ya binadamu pamoja na ekolojia!

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya, CCEE na Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM yanakutana nchini Ureno.

Shirikisho la Mabara ya Maaskofu Katoliki Ulaya pamoja na Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM yanakutana nchini Ureno.

Semina mpya ya SECAM na CCEE kufanyika nchini Ureno: 12-15 Aprili

06/04/2018 15:52

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya (CCEE)  na Afrika ya Mashariki na Madagascar (SECAM-SCEAM) watafanya semina kuhusu matokeo ya utandawazi kwa Kanisa na kwa ajili ya utamaduni Ulaya na Afrika. Itafanyika huko Fatima nchini Ureno kuanzia tarehe 12-15 Aprili 2018.

 

Mabaraza ya Maaskofu ya Afrika Mashariki (Secam)  na  Comece (Ulaya) wametoa wito kwa viongzo wakuu wa nchi kuhusu ajira endelevu kwa jamii

Mabaraza ya Maaskofu ya Afrika Mashariki (Secam) na Comece (Ulaya) wametoa wito kwa viongzo wakuu wa nchi kuhusu ajira endelevu kwa jamii katika mkutano wao 29-30 Novemba 2017 Abidjan Ivory Coast

SECAM NA COMECE kwa Pamoja waomba Viongozi kutengeneza ajira endelevu!

30/11/2017 09:58

Maaskofu Katoliki wa Afrika ya Afrika(SECAM) na Ulaya (COMECE), kwa pamoja wametoa wito kwa viongozi wa kisiasa Ulaya na Afrika, kutengeneza ajira endelevu kwa ajili ya kuwanusuru vijana wa Afrika wanaoteswa na umaskini. Ujumbe huo umetolea katika Mkutano wa Viongozi huko Abidjan.

 

 

Wito wa pamoja wa SECAM na COMECE kwa Wakuu wa Umoja wa Afrika katika mkutano utakao anza Ivory Coast tarehe 28-29 Novemba 2017.

Wito wa pamoja wa SECAM na COMECE kwa Wakuu wa Umoja wa Afrika katika mkutano utakao anza Ivory Coast tarehe 28-29 Novemba 2017.

Wito wa pamoja wa SECAM na COMECE kwa Wakuu wa Umoja wa Afrika na Ulaya!

10/11/2017 09:54

"Tunaomba haki na usawa katika biashara ya bidhaa na huduma, lakini hasa kuhusiana na rasilimali za asili, ambazo huchukuliwa kila mwaka kutoka Afrika. Ni maneno yanayothibitishwa na Maaskofu wa Afrika na Ulaya katika Waraka wa pamoja wa Tume ya Mabaraza ya Maaskofu Ulaya na SECAM