Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Sakramenti za Kanisa

Sherehe ya Noeli na Mwaka Mpya 2018 iwe ni fursa ya kukazia misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu!

Sherehe ya Noeli na Mwaka 2018 iwe ni fursa ya kukazia misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu wa Mataifa.

Familia ya Mungu nchini Tanzania dumisheni: haki, amani na maridhiano

30/12/2017 14:39

Kipindi cha Noeli na Mwaka Mpya 2018 iwe ni fursa kwa familia ya Mungu kujenga na kudumisha utamaduni wa haki, amani na maridhiano; mambo msingi katika kusimamia haki msingi za binadamu, umoja na mshikamano wa kitaifa, chachu muhimu sana katika mchakato mzima wa maendeleo ya watu!

 

Waamini wanapaswa kushikamana na Kristo katika sala na huduma kama ushuhuda wa imani tendaji!

Waamini wanapaswa kushikamana na Kristo Yesu katika sala na huduma kama kielelezo cha ushuhuda wa imani tendaji!

Mbinu mkakati wa uinjilishaji mpya unaojikita katika ushuhuda makini!

28/12/2017 07:51

Ili kuweza kujenga na kudumisha mchakato wa uinjilishaji mpya wenye tija na mafanikio makubwa kuna haja kwa Wakristo kufahamu mafundisho tangu ya Kanisa; kujikita katika umoja, upendo na mshikamano katika sala na huduma inayomwilishwa katika matendo ya huruma: kiroho na kimwili hasa kwa maskini!

Papa Francisko: Jengeni utamaduni wa kusikiliza na kukutana na watu, ili kuwaonjesha furaha ya Injili!

Papa Francisko: Jengeni utamaduni wa kukutana na watu ili kuwaonjesha furaha ya Injili!

Jengeni utamaduni wa kusikiliza kwa makini, ili mtende kwa haki!

28/12/2017 07:31

Baba Mtakatifu Francisko anaitaka familia ya Mungu kujenga utamaduni wa kusikiliza na kusikilizana kwa makini, ili kuguswa na mahangaiko ya jirani, tayari kujibu kilio na mahangaiko haya kwa njia ya ushuhuda wa haki, amani, upendo na mshikamano; nguzo thabiti za haki msingi za binadamu!

Askofu mkuu Anthony Muheria wa Jimbo Kuu la Nyeri, Kenya anawataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kudumisha upendo, umoja na amani!

Askofu mkuu Athony Muheria wa Jimbo Kuu la Nyeri, Kenya anawataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kujenga na kudumisha umoja, upendo, mshikamano na amani kama njia muafaka ya kuadhimisha Noeli ya Bwana!

Ujumbe wa Noeli kwa Mwaka 2017 kutoka kwa Askofu mkuu Muheria, Kenya

23/12/2017 08:49

Katika Sherehe ya Noeli, Mama Kanisa anaadhimisha kwa shangwe kubwa Fumbo la Umwilisho, Neno wa Mungu, Nafsi ya Pili ya Fumbo la Utatu Mtkatifu alipofanyika mwili kwa njia ya Roho Mtakatifu kwake Bikira Maria. Huu ni muungano wa ajabu wa asili ya Kimungu na asili ya kibinadamu ndani ya Kristo Yesu

Waamini wana hamasishwa na Mama Kanisa kushikamana na Kristo Yesu katika maisha yao, kamwe wasijitafute wenyewe na kusahau uwepo wa Kristo!

Waamini wana hamasishwa na Mama Kanisa kujishakamanisha na Kristo Yesu katika hija ya maisha yao na kamwe wasijitafute wenyewe watazama ndani ya tumbo la maji kama risasi.

Usiposhikamana na Kristo Yesu, utazama kama jiwe majini!

09/08/2017 13:23

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya XIX ya Mwaka A wa Kanisa ni mwaliko kwa waamini kujishikamanisha na Kristo Yesu, aliye njia, ukweli na uzima! Pale wanaposhindwa kumwambata Kristo, watazama majini na kutoweka kama ndoto ya mchana! Kwa kushikamana na Yesu, amani inapatikana!

Wito na maisha ya kipadre yamehifadhiwa katika chombo cha udongo!

Wito na maisha ya kipadre yamehifadhiwa kwenye chombo cha udongo!

Alessandro Manzi, C.PP.S apewa Daraja Takatifu ya Upadre!

24/07/2017 10:53

Mapadre katika maisha na utume wao, wanaendelea kuulizwa swali la msingi na Kristo Yesu ikiwa kama wanampenda Kristo katika Sala, Neno la Mungu, Sakramenti za Kanisa na Mafundisho Tanzu sanjari na sadaka ya maisha inayotolewa kwa ajili ya wokovu wa watu wa Mungu!

 

Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu imetengwa maalum kwa ajili ya kuombea Utakatifu wa Mapadre Duniani.

Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu ni siku maalum iliyotengwa na Mama Kanisa kwa ajili ya kuombea Utakatifu wa Mapadre Duniani.

Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu: Siku ya kutakatifuza Mapadre

22/06/2017 07:17

Moyo Mtakatifu wa Yesu ni chemchemi ya huruma, faraja na upendo wa Mungu kwa binadamu! Ni kisima cha neema, baraka na Sakramenti za Kanisa! Kwani Moyo Mtakatifu wa Yesu, uliotobolewa kwa mkuki, humo ilitoka damu na maji, alama ya Sakramenti ya Ubatizo na Ekaristi Takatifu.

Sinodi ya kwanza ya Jimbo kuu la Tabora ilikuwa ni nafasi ya kutembea pamoja kama familia ya Mungu ili kujadiliana sera na mikakati ya kichungaji.

Sinodi ya kwanza ya Jimbo kuu la Mwanza ilikuwa ni nafasi ya familia ya Mungu kutembea kwa pamoja, ili kujadiliana sera na mikakati ya shughuli za kichungaji.

Jimbo kuu la Tabora na changamoto za Chama cha Wakarismatiki!

05/06/2017 07:26

Askofu mkuu Paul Ruzoka wa Jimbo kuu la Tabora anasema, Sinodi ya Jimbo imekuwa ni fursa muafaka wa kutembea pamoja kama familia ya Mungu Jimboni humo na hivyo kupata kujadili kwa kina na mapana: utume na maisha ya Kanisa; changamoto na matarajio ya Jimbo kuu la Tabora.