Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Sakramenti ya Upatanisho

Papa Francisko asema: huruma, msamaha na upatanisho ni kati ya mafundisho makuu ya Kristo Yesu kwa wafuasi wake.

Papa Francisko asema: huruma, msamaha na upatanisho ni kati ya mafundisho makuu ya Kristo Yesu kwa wafuasi wake.

Papa Francisko: huruma na msamaha ni mafundisho makuu ya Yesu

18/09/2017 10:09

Baba Mtakatifu Francisko anasema, huruma, msamaha na upatanisho ni kati ya mafundisho makuu ya Yesu yanayopatika kwa muhtasari katika Sala kuu ya Baba Yetu! Huu ni mwaliko kwa wale wote walionja huruma na upendo wa Mungu kuwa ni mashuhuda na vyombo vya huruma ya Mungu kwa jirani zao!

Waamini wanahamasishwa kukimbilia katika Mahakama ya huruma ya Mungu  ili kupata maondoleo ya dhambi, huruma, faraja na mapendo!

Waamini wanahamasishwa kukimbilia kwenye Mahakama ya huruma ya Mungu: inayotakasa, huruma inayofariji, huruma inayosamehe na kupyaisha upya!

Msamaha na upatanisho katika kweli na haki ni chemchemi ya furaha!

16/09/2017 09:23

Huruma na msamaha ni utambulisho wa watoto wa Mungu na ushuhuda wa upendo. Msamaha una nguvu inayoleta uponyaji wa ndani katika maisha ya mwamini. Msamaha humweka mtu huru na kuanza mchakato wa ujenzi wa misingi ya haki, amani, upendo na mshikamano katika ukweli na matumaini!

Sakramenti ya upatanisho ni mahakama ya huruma ya Mungu inayofariji, samahe na kuuhisha!

Sakramenti ya Upatanisho ni mahakama ya huruma ya Mungu inayotakasa, fariji, samahe na kuuisha!

Iweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni!

14/09/2017 11:19

Mama Kanisa anafundisha kwamba, huruma, upendo na haki ni fadhila ambazo inapaswa kumiminika kutoka katika kilindi cha moyo wa mwamini, ili hatimaye, kushuhudia: utakatifu, huruma na mapendo kutoka kwa Mwenyezi Mungu yaliyofunuliwa na Kristo Yesu katika ile sala kuu ya Baba Yetu!

 

Kusamehe waliokukosea kunakufungulia neema na baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu!

Kusamehe waliokukosea kunakufungulia neema na baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe jirani zetu!

14/09/2017 10:07

Waamini wanapoonesha ugumu na ukakasi wa kukataa kuwasamehe ndugu zao waliowakosea, mioyo yao inafungwa, ugumu wake unaifanya mioyo hii isipenywe na mapendo ya Baba mwenye huruma. Kwa kuungama dhambi na kusamehe jirani, miyo ya waamini inafungukia neema ya Mungu inayokoa!

Waamini wanahamasishwa na Mama Kanisa kujikosoa, kukosoana na hatimaye kujipatanisha na Mungu ili kuonja ukuu wa huruma yake!

Waamini wanahamasishwa na Mama Kanisa kujikosoa, kukosoana katika upendo na udugu, ili hatimaye, kujipatanisha na Mwenyezi Mungu ili kuonja ukuu wa huruma na upendo wake usiokuwa na kifani!

Umuhimu wa kukosoana kidugu!

06/09/2017 15:44

Kukosa na kukoseana ni jambo la kawaida katika maisha ya mwanadamu, lakini kusamehe na kupatana ni njia inayomwelekeza mwamini katika utimilifu wa maisha! Baba Mtakatifu Francisko anakazia umuhimu wa Sakramenti ya Upatanisho inayomwezesha mwamini kugusa ukubwa wa huruma ya Mungu!

 

Wema na ubaya duniani ni sawa na chanda na pete, Mungu peke yake ndiye anayeweza kutenganisha mambo haya siiku ya mwisho anasema Yesu!

Wema na ubaya duniani ni sawa na chanda na pete ni ukweli usioweza kutengenishwa isipokuwa na Mwenyezi Mungu nyakati za hukumu ya mwisho!

Papa Francisko: Asiyekuwa na dhambi anyooshe mkono!

24/07/2017 09:55

Kristo Yesu ni hekima ya Mungu iliyomwilishwa, awasaidie waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kutambua kwamba: wema na uzuri; ubaya na dhambi ni mambo ambayo kamwe hayawezi kutambulikana kwa kuzingatia mipaka ya kijiografia au makundi ya watu; yako ndani ya moyo wa mtu!

Papa Francisko anawataka waamini kung'oa vilema vya maisha kwa toba na wongofu wa ndani; kwa Sakramenti ya Upatanisho, Sala na Matendo ya huruma!

Papa Francisko anawataka waamini kung'oa vilema katika maisha yao kwa toba na wongofu wa ndani; kwa kukimbilia huruma na upendo kwa njia ya Sakramenti ya Upatanisho; kwa sala na matendo ya huruma.

Papa Francisko: Ng'oeni vilema, ili Neno lipate kuzaa matunda!

17/07/2017 09:08

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kung'oa vilema katika maisha yao ya kiroho, ili kweli Neno la Mungu lililopandwa ndani ya mioyo yao liweze kuzaa matunda ya toba, wongofu wa ndani na utakatifu wa maisha kwa kuambata Sakramenti ya Upatanisho.

Kanisa linawahitaji mashuhuda wa imani, utu wema na maadili ili kuyachachua malimwengu!

Kanisa linawahitaji mashuhuda wa imani, maadili na utu wema ili kuyachachua malimwengu!

Kanisa linawahitaji mashuhuda wa imani, maadili na utu wema!

24/06/2017 17:23

Waamini wanakumbushwa kwamba, katika maisha na utume wao hapa duniani watakumbana na changamoto nyingi sana, lakini jambo la msingi ni kusimama kidete katika misingi ya uadilifu, ukweli, uwazi na utakatifu wa maisha kama mashuhuda wa imani, utu wema na maadili!