Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Sakramenti ya ndoa

Papa Francisko afungisha Sakramenti ya Ndoa kwa wafanyakazi wa ndege walioshindwa kuadhimisha ndoa yao Kanisa kutokana na tetemeko la ardhi mwaka 2010

Papa Francisko amefungisha Sakramenti ya Ndoa kwa wafanyakazi wa Shirika la Ndege walioshindwa kuadhimisha Sakramenti hii Kanisani kutokana na tetemeko la ardhi lililoikumba Chile kunako mwaka 2010. Wanatumwa kuwa ni mashuhuda wa Injili ya ndoa na familia kwa jirani na wafanyakazi wenzao!

Papa Francisko afungisha ndoa angani wakati akielekea Jimboni Iquique

19/01/2018 09:00

Baba Mtakatifu Francisko baada ya kusikiliza historia na maelezo yaliyotolewa na wachumba wawili Bi Paula Podesà na Bwana Carlos Cuffando Elorriaga wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Latam 124b, ameamua kuwafungisha ndoa na kuwataka wawe ni mashuhuda wa Injili ya familia kwa jirani zao!

Sherehe ya Noeli na Mwaka Mpya 2018 iwe ni fursa ya kukazia misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu!

Sherehe ya Noeli na Mwaka 2018 iwe ni fursa ya kukazia misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu wa Mataifa.

Familia ya Mungu nchini Tanzania dumisheni: haki, amani na maridhiano

30/12/2017 14:39

Kipindi cha Noeli na Mwaka Mpya 2018 iwe ni fursa kwa familia ya Mungu kujenga na kudumisha utamaduni wa haki, amani na maridhiano; mambo msingi katika kusimamia haki msingi za binadamu, umoja na mshikamano wa kitaifa, chachu muhimu sana katika mchakato mzima wa maendeleo ya watu!

 

Watakatifu, mashuhuda na wandani wa matumaini kuishi utakatifu

Watakatifu, mshuhuda na wandani wa kuishi utakatifu.

Watakatifu, Mashuhuda na wandani wa matumaini

21/06/2017 13:12

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake siku ya Jumatano, amewaalika waamini kuwa jasiri wa imani na wenye matumaini thabiti katika kuchuchumilia utakatifu, wakikumbuka wanao watakatifu wanaowaombea na kuwasindikiza katika hija ya maisha na kwamba, utakatifu unawezekana!

Sheria za Kanisa kuhusu ndoa zinasaidia kurahisisha maisha ya waamini kadiri ya mafundisho ya Kanisa

Sheria za Kanisa kuhusu ndoa zinasaidia kurahisisha maisha ya waamini na sio nyenzo ya kubatilisha ndoa

Taratibu mpya za kesi za ndoa, nyenzo kuboresha maisha ya waamini

15/06/2017 14:34

Kitabu chachapishwa na majarimu wawili wa Chuo kikuu cha kipapa cha Lateran, kuelezea namna ya kufungua kesi za ndoa, uendeshwaji wake, na mambo muhimu ya kuzingatia kadiri ya taratibu mpya za sheria kanuni za kanisa zilizomo kwenye Mitis Iudex Dominus Iesus.

 

Vijana, Imani na Mang'amuzi ya Miito & Furaha ya upendo ndani ya famili; ni msingi wa Sinodi ya Maaskofu 2018.

Vijana, Imani na Mang'amuzi ya Miito ni msingi wa maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu wa Vijana kwa mwaka 2018, ili kuwasaidia vijana kufanya maamuzi magumu katika maisha yao"!

Kardinali Baldisseri: maadhimisho ya Sinodi kwa jicho la kichina!

18/05/2017 10:27

Wosia wa Kitume wa Baba Mtakatifu Francisko "Furaha ya upendo ndani na familia" na Kauli mbiu ya maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana yaani "Vijana, Imani na Mang'amuzi ya Miito" ni nyenzo msingi katika maandalizi ya maisha na utume wa vijana wa kizazi kipya kwa sasa!

Mwaka wa huruma ya Mungu umewawezesha waamini wengi kuguswa na upendo na huruma ya Mungu katika maisha yao, kiasi cha kutubu na kuongoka!

Mwaka wa huruma ya Mungu umewawezesha waamini wengi kutubu na kumwongokea Mungu kwa kuacha njia zao mbaya.

Mashuhuda wa mwaka wa huruma ya Mungu Jimbo kuu la Mwanza!

21/04/2017 12:32

Maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu imekuwa ni fursa ya kutubu na kumwongokea Mungu; nafasi ya kujipatanisha na Mungu pamoja na jirani; muda muafaka wa kurekebisha maisha ya Kikristo ili kuambata rehema na neema za Mwaka wa Jubilei ya huruma ya Mungu!

Familia bado ni sehemu ya Habari Njema ya Wokovu kwa walimwengu anasema Papa Francisko!

Familia bado ni sehemu ya Habari Njema ya Wokovu anasema Papa Francisko katika barua yake kwa Maaskofu Katoliki sehemu mbali mbali za dunia kama sehemu ya maandalizi ya Siku ya Tisa ya Familia Duniani, itakayoadhimishwa mwaka 2018 huko Dublin, nchini Ireland.

Iweni mashuhuda na vyombo vya Injili ya familia duniani!

20/04/2017 08:45

Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kuwamasisha waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kutambua kwamba, familia bado ni sehemu muhimu sana ya Habari Njema inayopaswa kutangazwa na kushuhudiwa ulimwenguni kwa kujikita katika tunu msingi za maisha ya kifamilia!

Papa Francisko amewaruhusu Mapadre wa Udugu wa Mtakatifu Pio X kuadhimisha Sakramenti ya Upatanisho na Ndoa kwa masharti maalum.

Papa Francisko amewaruhusu Mapadre wa Udugu wa Mtakatifu Pio X kuadhimisha Sakramenti ya Upatanisho na Ndoa kwa masharti maalum.

Papa: Udugu wa Mtakatifu Pio X: Sakramenti ya Upatanisho na Ndoa

04/04/2017 13:00

Baba Mtakatifu Francisko analitaka Kanisa kuwa kweli ni shuhuda na chombo amini cha huruma ya Mungu ili kuwahamasisha watu kuiona njia inayowaelekeza kwa Baba wenye huruma. Kwa mantiki hii amewaruhusu Mapadre wa udugu wa Mtakatifu Pio X kutoa Sakramenti ya Upatanisho na Ndoa.