
Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 19 Machi 2018 amesikiliza na kujibu maswali tete kutoka kwa vijana wanaoshiriki katika maadhimisho ya utangulizi wa Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana.
Vijana "wamtwanga" maswali mazito na tete Baba Mtakatifu Francisko!
Baba Mtakatifu anasema, Kanisa linapaswa kujenga utamaduni na sanaa ya kuwasikiliza vijana! Vijana wamepata nafasi ya kuuliza maswali mazito na tete kuhusu biashara ya binadamu na utumwa mamboleo, kutopea kwa imani; umuhimu wa elimu, majiundo ya wakleri na "makombo" ya elimu kwa watawa!
Mitandao ya kijamii: