Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu anaendelea kujifunua katika Maandiko Matakatifu, Sakramenti za Kanisa, na katika maisha na utume wa Kanisa.

Roho Mtakatifu anaendelea kujifunua kwa njia ya Maandiko Matakatifu, Sakramenti za Kanisa na kwa namna ya pekee kabisa Sakramenti ya Kipaimara na katika maisha na utume wa Kanisa.

Pentekoste ni nafasi ya kumtafakari Roho Mtakatifu!

18/05/2018 15:35

Roho Mtakatifu, Nafsi ya Tatu katika Fumbo la Utatu Mtakatifu ndiye anayelitakatifuza Kanisa na kwamba, anayo nafasi muhimu sana katika maisha na utume wa Kanisa. Ni tunda la upendo wa Baba na Mwana! Roho Mtakatifu ni moyo wa Kanisa na kifungo cha umoja na kikolezo cha ushuhuda wa imani!

Pentekoste ni utimilifu wa Pasaka ya Kristo Yesu na ufunuo mkamilifu wa Fumbo la Utatu Mtakatifu.

Pentekoste ni utimilifu wa Pasaka ya Kristo Yesu na ufunuo mkamilifu wa Fumbo la Utatu Mtakatifu.

Sherehe ya Pentekoste: Utatu Mtakatifu unafunuliwa kikamilifu!

17/05/2018 07:00

Mababa wa Kanisa wanafundisha na kusadiki kwamba, Sherehe ya Pentekoste ni utimilifu wa Pasaka ya Kristo kwa kummimina Roho Mtakatifu, ambaye ametolewa na kushirikishwa kama nafsi ya Mungu. Hii ni siku ambayo Fumbo la Utatu Mtakatifu limefunuliwa kikamilifu, tayari kutangaza Ufalme wa Mungu.

Roho Mtakatifu ni paji la Mungu. Anatakasa, anahuisha, anatakasa Kanisa na ni Sakramenti ya umoja wa Utatu Mtakatifu na wa watu.

Roho Mtakatifu ni paji la Mungu. Anajenga, anahuisha na kulitakasa Kanisa; ni Sakramenti ya umoja wa Utatu Mtakatifu na wa watu!

Sherehe ya Pentekoste, kuzaliwa kwa Kanisa!

16/05/2018 15:44

Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Bwana mleta uzima: atokaye kwa Baba na Mwana. Anayeabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana: aliyenena kwa vinywa vya Manabii. Hii ndiyo imani ya Kanisa juu ya Roho Mtakatifu, Nafsi ya Tatu katika Fumbo la Utatu Mtakatifu; Sakramenti ya Umoja!

 

Papa Francisko analihamasisha Kanisa kujenga utamaduni wa kuwasikiliza, kuwajali na kuwasindikiza vijana katika hija ya maisha yao hapa duniani.

Papa Francisko analihamasisha Kanisa kujenga utamaduni wa kuwasikiliza, kuwathamini, kuwajali na kuwasindikiza vijana katika hija ya maisha yao hapa duniani.

Baba Mtakatifu Francisko kukutana na vijana wa Italia, Agosti, 2018

12/05/2018 07:53

Baba Mtakatifu Francisko katika kipindi cha miaka miwili, amewahamasisha viongozi mbali mbali wa Kanisa kujenga na kudumisha utamaduni wa kuwasikiliza, kuwathamini pamoja na kuwasindikiza vijana katika hija ya maisha yao ya kiroho, ili waweze kufanya maamuzi magumu na yenye busara.

Sherehe ya Kupaa Bwana Mbinguni inawaachia wakristo wajibu wa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu!

Sherehe ya Kupaa Bwana Mbinguni inawachia Wakristo wajibu na dhamana ya kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu hadi miisho ya dunia.

Leo mnatumwa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu!

11/05/2018 16:11

Ee Mungu Mwenyezi, utufanye tuwe na furaha takatifu na shukrani; kwa maana kupaa kwake Kristo Yesu, Mwanaoni mfano wetu; na huko alikotangulia yeye kichwa chetu, ndiko tunakotumaini kufika sisi tulio mwili wake. Leo ubinadamu wetu umetukuzwa mbinguni!

Yesu alipaa mbinguni, amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi.

Yesu alipaa mbinguni, amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi.

Kristo Yesu akishakuinuliwa juu, atawavuta wote kwake!

10/05/2018 16:31

Kristo Yesu peke yake ndiye aliyetoka kwa Baba na anaweza kurudi tena kwa Baba. Hakuna mtu aliyepaa mbinguni ile Yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani Mwana wa mtu! Ubinadamu ukiachiwa katika nguvu zake za maumbile hauwezi kufika kwenye nyumba ya Baba, kwenye uzima na furaha ya milele!

 

Sherehe ya Kupaa Bwana Mbinguni

Sherehe ya Kupaa Bwana Mbinguni.

Sherehe ya Bwana Kupaa Mbinguni!

10/05/2018 15:23

Mama Kanisa anasadiki na kufundisha kwamba, Yesu alipaa mbinguni, amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi, atarudi kuwahukumu wazima na wafu na wala ufalme wake hautakuwa na mwisho: Ubinadamu wa Yesu unamficha mbele ya macho ya watu. Yesu amewatangulia waja wake katika Ufalme wa utukufu

Leo Mama Kanisa anapenda kuwarejesha tena watoto wake kwenye shule ya upendo mkamilifu!

Leo Mama Kanisa anapenda kuwarejesha watoto wake kwenye shule ya upendo mkamilifu unaopata chimbuko lake kwa Mungu Baba ambaye ni upendo wenyewe!

Leo Mama Kanisa anawarudisha watoto wake kwenye shule ya upendo!

05/05/2018 07:30

Katika historia, Mwenyezi Mungu amejifunua kwa watu wake kwa sababu ya upendo wake mkuu usiokuwa na kifani; akawachagua kati ya mataifa kwa sababu ya upendo huo huo, akawakoa kutokana na ukaidi wao kwa sababu ya upendo! Kwa hakika, Mungu ni upendo na upendo wake ni wa milele!