Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Rais Sergio Mattarella

Papa Francisko ametuma salam na matashi mema kwa viongozi mbali mbali wa dunia wakati akirejea mjini Vatican.

Papa Francisko ametuma salam na matashi mema kwa viongozi wa nchi na wakuu wa Serikali wakati akirejea mjini Vatican, Jumatatu, tarehe 11 Septemba 2017.

Papa Francisko: Salam na matashi mema kwa wakuu wa nchi na serikali

11/09/2017 14:07

Baba Mtakatifu Francisko wakati akirejea kutoka Colombia kwa hija yake ya kitume, ametuma salam na matashi mema kwa viongozi wakuu wa nchi na Serikali ya: Colombia, Netherland, Marekani, Ureno, Hispania, Ufaransa na Italia. Amewashukuru wananchi wa Colombia kwa mapokezo makubwa!

Papa Francisko akiwa njiani kuelekea Colombia ametuma salam na matashi mema kwa viongozi wakuu wa nchi alimopitia!

Papa Francisko akiwa njiani kuelekea nchini Colombia ametuma salam na matashi mema kwa wakuu wa nchi alimopitia.

Papa Francisko atuma salam na matashi mema kwa viongozi wakuu wa nchi

06/09/2017 14:26

Baba Mtakatifu Francisko katika hija yake ya kitume kuelekea nchini Colombia Jumatano tarehe 6 Septemba 2017 ametuma sala na matashi mema kwa viongozi wakuu wa nchi akiwatakia heri, baraka, ustawi, maendeleo na amani! Kwa namna ya pekee amewakumbuka wananchi wa Venezuela!

Rais Sergio Mattrella wa Italia anawataka wanasiasa na watunga sera kuwezeka zaidi kwa vijana katika elimu na ajira.

Rais Sergio Mattarella wa Italia anawataka wanasiasa na watunga sera kuwekeza katika elimu makini miojngoni mwa vijana pamoja na kuwapatia fursa za ajira.

Rais Sergio Mattarella: wekezeni kwa vijana katika elimu na ajira

21/08/2017 09:27

Rais Sergio Mattarella wa Italia anawataka wanasiasa, wachumi na wadau mbali mbali kuhakikisha kwamba, wanawekeza katika vijana kwa kuwapatia elimu makini na endelevu ili kupambana na changamoto za maisha sanjari na kuwapatia fursa za ajira ili kuwa na matumaini yaliyo bora zaidi.

Biashara haramu ya binadamu na mifumo yote ya utumwa mamboleo ni uhalifu dhidi ya utu na heshima ya binadamu!

Biashara haramu ya binadamu na mifumo yote ya utumwa mamboleo ni uhalifu dhidi ya utu na heshima ya binadamu aliyeumbwa kwa sura namfano wa Mungu.

Papa Francisko: Biashara ya binadamu na utumwa mamboleo ni uhalifu!

31/07/2017 08:59

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wadau mbali mbali kusimama kidete kupinga na hatimaye kukomesha kabisa biashara ya binadamu na mifumo yote uìya utumwa mamboleo kwani huu ni uhalifu dhidi ya utu wa binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Watu wasiifanye kuwa ni mazoea!

Ujumbe wa vatican umetembelea Ikulu ya Italia, tarehe 10 Juni 2017.

Ujumbe wa Vatican umetembelea Ikulu ya Italia, tarehe 10 Juni 2017.

Ujumbe wa Vatican watembelea Ikulu ya Italia!

10/06/2017 16:03

Ujumbe mzito kutoka Vatican umemtembelea Rais Sergio Mattarella wa Italia aliyekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko kwanza kwa faragha na hatimaye, wote kwa pamoja wakatoa hotuba zao mbele ya ujumbe wa Vatican na Serikali ya Italia inayoongozwa na Rais Sergio Mattarella.

 

Papa Francisko asema, Kanisa litaendelea kushirikiana na Serikali ya Italia kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi!

Papa Francisko asema, Kanisa litaendelea kushirikiana na kushikamana na Serikali ya Italia kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Vatican kuendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Italia!

10/06/2017 15:46

Baba Mtakatifu Francisko anasema, changamoto zinazoikabili Italia kwa sasa zinapaswa kushughulikiwa kwa njia ya ushirikiano na mshikamano na wote, ili kuwajengea vijana matumaini ya leo na kesho iliyo bora zaidi; kwa kujikita katika utajiri na amana za maisha ya kiroho na kiutu nchini Italia.

Papa Francisko tarehe 10 Juni 2017 anatembelea Ikulu ya Italia ili kukutana na kuzungumza na Rais Mattarella wa Italia.

Papa Francisko tarehe 10 Juni 2017 anatarajia kukutana na kuzungumza na Rais Sergio Mattarella wa Italia.

Papa Francisko kutembelea Ikulu ya Italia tarehe 10 Juni 2017

16/05/2017 09:29

Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa hapo tarehe 10 Juni 2017 kutembelea rasmi Ikulu ya Italia ili kukutana na kuzungumza na Rais Sergio Mattarella wa Italia kama njia ya kukuza na kudumisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Italia na Vatican na kuendeleza ushirikiano wa kitaifa na kimataifa.

Baba Mtakatifu anaishukuru Familia ya Mungu nchini Ureno kwa ukarimu na mapokezi makubwa waliyomwonesha!

Baba Mtakatifu anaishukuru Familia ya Mungu nchini Ureno kwa ukarimu na mapokezi makubwa waliyomfanyia!

Papa Francisko anawashukuru wote waliofanikisha hija yake ya kitume!

15/05/2017 10:32

Baba Mtakatifu Francisko amejijengea utamaduni wa kuomba na kushukuru kabla na baada ya hija zake za kitume! Ameendeleza utamaduni wa kuwatakatia heri na matashi mema wakuu wa Nchi ambamo anapitia wakati wa kwenda na kurejea kutoka katika hija zake za kitume! Amefanya hivi hata wakati huu!