Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Rais Juan Manuel Santos Calderon

Papa Francisko akiwa njiani kurejea mjini Vatican ametuma salam na matashi mema kwa viongozi wakuu wa nchi na serikali alimopitia.

Papa Francisko akiwa njiani kurejea mjini Vatican baada ya kuhitimisha hija yake ya kitume huko Amerika ya kusini, Jumatatu tarehe 22 Januari 2018 amewatumia wakuu wa serikali na nchi salam na matashi mema.

Papa Francisko atuma salam na matashi mema kwa wakuu wa nchi

23/01/2018 13:54

Baba Mtakatifu Francisko akiwa njiani kurejea tena mjini Vatican mara baada ya kuhitimisha hija yake ya kitume, amewatumua ujumbe wa amani na matashi mema wakuu mbali mbali wa nchi ambamo amepitia wakati akirejea kutoka huko Amerika ya Kusini ambako ameshuhudia imani katika matendo!

Papa Francisko ametuma salam na matashi mema kwa viongozi mbali mbali wa dunia wakati akirejea mjini Vatican.

Papa Francisko ametuma salam na matashi mema kwa viongozi wa nchi na wakuu wa Serikali wakati akirejea mjini Vatican, Jumatatu, tarehe 11 Septemba 2017.

Papa Francisko: Salam na matashi mema kwa wakuu wa nchi na serikali

11/09/2017 14:07

Baba Mtakatifu Francisko wakati akirejea kutoka Colombia kwa hija yake ya kitume, ametuma salam na matashi mema kwa viongozi wakuu wa nchi na Serikali ya: Colombia, Netherland, Marekani, Ureno, Hispania, Ufaransa na Italia. Amewashukuru wananchi wa Colombia kwa mapokezo makubwa!

Wosia wa Papa Francisko nchini Colombia: jitahidini kupiga hatua ya kwanza katika amani na upatanisho!

Wosia wa Papa Francisko nchini Colombia: kila mtu apige hatua ya kwanza katika amani na upatanisho wa kitaifa.

Wosia wa Papa Francisko kwa familia ya Mungu nchini Colombia

11/09/2017 13:46

Baba Mtakatifu Francisko kabla ya kuanza safari ya kurejea tena mjini Vatican baada ya kukamilisha hija yake ya kitime nchini Colombia, amewaachia wananchi wa Colombia ujumbe mzito sana, akimtaka kila mwanchi kuanza kupiga hatua ya kwanza katika mchakato wa amani na upatanisho wa kitaifa.

Papa Francisko akiwa kwenye Kanisa kuu la Jimbo kuu la Bogotàa aliwabariki waamini na kuwataka kuwa ni vyombo na mashuhuda wa amani na upatanisho.

Papa Francisko akiwa kwenye Kanisa kuu la Jimbo kuu la Bogotà, nchini Colombia aliwataka waamini kuwa ni vyombo vya amani na upatanisho.

Papa Francisko anawataka vijana kuwa ni vyombo vya haki na amani!

08/09/2017 11:12

Baba Mtakatifu Francisko anawataka vijana kurutubisha furaha iliyomo ndani mwao baada ya kukutana na Kristo Yesu anayewahamasisha kumpenda Mungu na jirani! Waguswe na mateso na mahangaiko ya ndugu na jirani zao; wajitose bila ya kujibakiza kwa ajili ya huduma makini, haki, amani na upatanisho!

Papa Francisko amewasili nchini Colombia tayari kuanza hija ya amani na upatanisho kati ya watu wa Colombia!

Baba Mtakatifu Francisko amewasili nchini Colombia tayari kuanza hija ya amani na upatanisho miongoni mwa wananchi wa Colombia!

Baba Mtakatifu Francisko "atinga timu" nchini Colombia!

07/09/2017 12:16

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika wananchi wa Colombia kuwa ni mashuhuda wa furaha na matumaini na kamwe wasiwaruhusu wajanja wachache kuwapoka furaha yao; wajielekeze sasa katika mchakato wa haki, amani na maridhiano yanayofumbatwa katika msamaha na upatanisho wa kweli!

Papa Francisko aanza hija yake ya kitume nchini Colombia kwa kujikabidhi chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria, Afya ya Warumi!

Papa Francisko aanza hija yake ya kitume nchini Colombia kwa kujikabidhi ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria, Afya ya Warumi!

Papa Francisko "ang'oa majembe" kuelekea Colombia!

06/09/2017 11:01

Baba Mtakatifu Francisko ameanza hija yake ya kitume ya 20 nje ya Italia kwa kujikabidhi chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria, Afya ya Warumi! Anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kumsindikiza katika hija hii kwa sala na sadaka zao, ili izae matunda ya amani na upatanisho.