Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Rais John Pombe Magufuli

Uzinduzi wa Parokia mpya ya Theresa wa Mtoto Yesu, Jimbo kuu la Dodoma unapania kusogeza huduma za kichungaji kwa waamini.

Uzinduzi wa Parokia mpya ya Theresa wa Mtoto Yesu unalenga kusogeza huduma za kichungaji kwa familia ya Mungu katika eneo hili anasema Askofu mkuu Beatus Kinyaiya.

Parokia ya Theresa wa Mtoto Yesu, Jimbo kuu Dodoma: kitovu cha utume!

11/10/2017 07:38

Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya wa Jimbo kuu la Dodoma, hivi karibuni amezindua Parokia mpya ya Theresa wa Mtoto Yesu inayopaswa kuwa ni kitovu cha maisha na utume wa Kanisa katika maadhimisho ya Sakramenti za Kanisa, Katekesi, Tafakari na Matendo ya huruma: kiroho na kimwili!

Serikali ya Rais Magufuli ina wizara 21 kwa sasa kutoka wizara 19 zilizokuwepo hapo awali.

Serikali ya Rais Magufuli wa Tanzania kwa sasa ina jumla ya wizara 21 ikilinganishwa na wizara 19 zilizokuwepo hapo awali lengo ni kuboresha tifa, ufanisi na huduma kwa watanzania.

Rais John Pombe Magufuli aliapisha Baraza Jipya la Mawaziri

09/10/2017 11:46

Rais John Magufuli baada ya kusoma alama za nyakati amefanya mabadiliko makubwa katika Baraza lake la Mawaziri kwa kiongeza wizara ili kuboresha tija na ufanisi; kwa kuwateua mawaziri na naibu mawaziri wapya ambao wameapishwa. Serikali sasa ina wizara 21 kutoka wizara 19 zilizokuwepo hapo awali!

 

Shirika la Umoja wa Mataifa  kusaidia wakimbizi linatoa taarifa kuwa katika kanda za nchi ya Tanzania, wapo wakimbizi 243,565, kutoka Burundi

Shirika la Umoja wa Mataifa kusaidia wakimbizi linatoa taarifa kuwa katika kanda za nchi ya Tanzania, wapo wakimbizi 243,565, pamoja na hayo pia wapo zaidi ya wakimbizi 162,000 kutoka Burundi waliokimbia nchi yao tangu 1972.

Nchi ya Tanzania itatoa uraia kwa wakimbizi wa Burundi waliofika tangu 1972

28/08/2017 15:52

Tanzania itatoa uraia wa wakimbizi kutoka Burundi waliofika zaidi ya miaka 45.Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia wakimbizi zinaonesha kuwa kanda za nchi ya Tanzaniawapo wakimbizi 243,565,pia wapo zaidi ya wakimbizi 162,000 kutoka Burundi walifika tangu1972.

 

Rais Magufuli wa Tanzania anaishukuru Uingereza kwa kuchangia maendeleo ya Tanzania na kuwataka watanzania kujenga utamaduni wa kulipa kodi.

Rais John Magufuli wa Tanzania anaishukuru Serikali ya Uingereza kwa kusaidia kuchangia ustawi, maendeleo na mafao ya wengi nchini Tanzania, lakini anawataka watanzania kujenga utamaduni wa kulipa kodi kuchangia mchakato wa maendeleo yao wenyewe.

Rais Magufuli awataka watanzania kujenga utamaduni wa kulipa kodi

24/08/2017 09:21

Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa kuchangia ustawi, maendeleo na mafao ya watanzania na kuwataka watanzania kujenga na kukuza na utamaduni wa kulipa kodi kama sehemu ya mchakato wa kuchangia maendeleo yao ili kupunguza utegemezi wa nje!

 

Watanzania wanaosoma nchini Cuba wametakiwa kujifunza kwa bidii, juhudi na maarifa ili hatimaye, wanapomaliza masomo yao, wachangie maendeleo ya watu.

Watanzania wanaosomo nchini Cuba wametakiwa kujifunza kwa bidii, juhudi na maarifa, ili wanapohitimu masomo yao, waweze kusaidia mchakato wa maboresho ya maisha ya watanzania wengi.

Watanzania jengeni umoja, mshikamano na imarisheni uzalendo!

22/08/2017 07:30

Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozo madhubuti wa Rais John Pombe Magufuli, inawataka watanzania kujizatiti katika ujenzi wa umoja na mshikamano wa kitaifa, sanjari na kudumisha uzalendo ili kuendeleza fursa mbali mbali za ustawi, maendeleo na mafao ya watanzania wengi zaidi.

 

Tanzania na Cuba ni nchi ambazo zimekuwa na ushirikiano mkubwa katika medani mbali mbali za maisha ya mwanadamu!

Tanzania na Cuba ni nchi ambazo zimekuwa na uhusiano mkubwa wa kidiplomasia katika medani mbali mbali za maisha.

Tanzania ina thamini uhusiano na mchango wa Cuba kwa watanzania!

21/08/2017 11:33

Tanzania na Cuba ni nchi ambazo zimekuwa na uhusiano wa kidiplomasia kwa muda mrefu tangu uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hadi wakati huu wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli. Cuba imechangia sana katika sekta ya afya, siasa na maendeleo jamii.

 

Askofu mkuu Marek Solcynski, Balozi wa Vatican nchini Tanzania amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania.

Askofu mkuu Marek Solcynski, Balozi wa Vatican nchini Tanzania, amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania, tarehe 1 Agosti 2017.

Askofu mkuu Marek Solczyński, awasilisha hati za utambulisho Tanzania

07/08/2017 14:00

Askofu mkuu Marek Solczynski, Balozi wa Vatican nchini Tanzania ni kati ya Mabalozi watano ambao hivi karibuni wamewasilisha hati zao za utambulisho kwa Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania ambaye amekazia kwa namna ya pekee, diplomasia ya uchumi ili kukuza ushirikiano katika uchumi. 

 

Tanzania na Uganda zimezindua ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania.

Tanzania na Uganda zimezindua ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi, EAC, wazinduliwa Tanga!

07/08/2017 11:58

Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Jumamosi, tarehe 5 Agosti 2017 wamezindua ujenzi wa mradi wa bomba na mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi banadari ya Tanga nchini Tanzania. Ujenzi utakamilika Mwaka 2020.