Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Rais Jacob Zuma

Bwana Jacob Zuma, amebwaga manyanga ya Urais baada ya kukumbwa na tuhuma za rushwa na ufisadi!

Bwana Jacob Zuma, amebwaga manyanga ya Urais wa Afrika ya Kusini baada ya kukumbukwa na shutuma za rushwa na ufisadi wa mali ya umma.

Bwana Jacob Zuma abwaga manyanga ya Urais Afrika ya Kusini!

15/02/2018 13:06

Bwana Jacob Zuma aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini katika kipindi chake kifupi cha uongozi ameandamwa sana na kashfa ya rushwa na ufisadi wa mali ya umma, shutuma ambazo amekuwa akizikana, lakini, hatimaye baada ya shinikizo la A.N.C. hatimaye amejiuzuru kwa manufaa ya umma na Bunge limekubali.

 

Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika ya Kusini linamwomba Rais Zuma kung'atuka madarakani kwa ajili ya mafao ya umma.

Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika ya Kusini lina mshauri rais Jacob Zuma kufanya maamuzi magumu ya kung'atuka kutoka madarakani kwa ajili ya mafao ya umma kwani kwa sasa hali ni tete sana nchini Afrika ya Kusini.

Rushwa na ufisadi vinawapekenya sana wananchi wa Afrika ya Kusini

10/02/2018 17:26

Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika ya Kusini linasema kwamba, hali kwa sasa ni tete sana Afrika ya Kusini kutokana na kashfa pamoja na tuhuma mbali mbali hasa kuhusiana na rushwa na ufisadi wa mali ya umma zinazomwandama Rais Jacob Zuma, kiasi cha wananchi wengi kukosa imani naye!

Rushwa, ufisadi, ukosefu wa ajira na hali mbaya ya uchumi imewafanya wananchi wengi wa Afrika ya Kusini kutoridhika na uongozi wa Rais Jacob Zuma.

Rushwa, ufisadi, ukosefu wa fursa za ajira hasa miongoni mwa vijana wa kizazi kipya na utawala mbaya ni kati ya mambo ambayo yamewachefua sana wananchi wa Afrika ya Kusini kiasi cha kuonesha kutokuwa na imani tena na Rais Zuma.

Bunge Afrika ya Kusini kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais Zuma

20/04/2017 07:38

Hali tete ya kisiasa nchini Afrika ya Kusini imeingia katika awamu mpya baada ya wabunge kuridhia mchakato wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma kutokana na kuandamwa mno na kashfa, ufisadi na utawala mbaya hali ambayo imepelekea maandamano ya wananchi wengi Afrika ya Kusini.

Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika ya Kusini linamshauri Rais Zuma kung'atuka kutoka madarakani kutokana kashfa ya rushwa na ufisadi wa mali ya umma.

Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika ya Kusini lina mshauri Rais Jacob Zuma kuonesha ujasiri na unyenyekevu wa kisiasa kwa kung'atuka kutoka madarakani, ili kutoa nafasi kwa Afrika ya Kusini kuganga na kuponya saratani ya rushwa na ufisadi unaoendelea kusababisha hali ngumu ya uchumi nchini humo!

Maaskofu Afrika ya Kusini: Rais Zuma usiogope kung'atuka!

06/04/2017 15:02

Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika ya Kusini linamshauri Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini kuonesha ujasiri na unyenyekevu wa kisiasa kwa kung'atuka kutoka madarakani baada ya kuandamwa na kashfa ya rushwa na ufisadi wa mali ya umma ili kutoa mwanya wa kuganga na kutibu saratani ya rushwa!

 

Maelfu ya wananchi wa Cuba, Jumatano tarehe 30 Novemba 2016 yalijipanga barabrani ili kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu Fidel Castro wa Cuba.

Maelfu ya wananchi wa Cuba, Jumatano tarehe 30 Novemba 2016 yalijipanga barabrani kutoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu Fidel Castro wa Cuba aliyefariki dunia hivi karibuni akiwa na umri wa miaka 90.

Komrade Fidel Castro alikuwa ni mtetezi na rafiki wa nchi maskini duniani!

30/11/2016 16:01

Rais Fidel Castro wa Cuba licha ya kuwa chini ya vizuizi vya kiuchumi kwa muda wa takribani miaka 54 lakini aliiwezesha Cuba kuchangia kwa hali na mali katika harakati za kupigania uhuru, utu na heshima kwa nchi maskini zaidi duniani, akaonesha mshikamano katika huduma ya elimu na afya!

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Kusini mwa Afrika linaitaka Serikali ya Afrika ya Kusini kushughulikia changamoto za nchi kwa ujasiri mkuu!

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Kusini mwa Afrika linaitaka Serikali kushughulikia changamoto za kitaifa kwa ujasiri na umakini mkubwa!

SACBC: Huduma ya afya ipewe kipaumbele cha kwanza na wala si silaha!

04/05/2016 07:25

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Kusini mwa Afrika linaloundwa na Maaskofu kutoka Swaziland. Botswana na Afrika ya Kusini, SACBC linaitaka Serikali ya Afrika ya Kusini kushughulikia kwa ujasiri na uzalendo changamoto zinazoendelea kuitikisa Afrika ya Kusini kwa nyakati hizi ili kulinda amani!

 

Rais John Pombe Magufuli akitia sahihi kwenye viapo vyake.

Rais John Pombe Magufuli akitia sahihi kwenye viapo vyake vya Urais, tarehe 5 Novemba 2015.

Mwanasheria mkuu George Mcheche Masaju, Kikao cha Bunge 17 Nov; Waziri mkuu?

06/11/2015 09:56

Rais John Pombe magufuli amemteua George Mchche Masaju kuwa Mwanasheria mkuu wa Tanzania na tarehe 17 Novemba, 2015 Kikao cha kumi na moja cha Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Taifa litaanza kikao chake! Hadi kufikia tarehe 19 Novemba 2015 Waziri mkuu mteule atakuwa amepatikana.